Hongera Rais Samia kwa zoezi la Sensa linaloendelea nchini

Fukua

JF-Expert Member
Jun 1, 2022
546
479
Salaam wanajukwaa na watanzania wote.

Kwanza, nimshukuru Mungu muumba kwa uzima na afya tele NAMI nimeiona siku ya leo.

Pili, Nimshukuru Rais wetu Mpendwa Mama msikivu, mnyenyekevu, mpole, mchapakazi, na mwenye mapenzi mema na nchi yetu, Mama SAMIA kwa kuendelea kuiongoza nchi yetu kwa weledi wa Hali ya juu kabisa.

Kama Amir JESHI MKUU, watanzania tuko salama salimini, kama mfariji mkuu hujaacha kutufariji, kama kiongozi mkuu unatuongoza katika njia yenye mafanikio kabisa, kama mwakilishi wetu kimataifa umeirudisha heshima ya Tanzania kimataifa na kama Mama unatulea katika maadili mema ya kiutu,kistaarabu na kwa upendo wa agape.

Tatu, ninakupongeza mama kwa juhudi na maarifa kuundaa,kuuratibu,na kuusimamia huu mchakato/ zoezi la SENSA YA WATU NA MAKAZI, watanzania wenye akili tunafahamu halikua jambo rahisi, haukulala.

Na wasaidizi wako wameifanya kazi usiku na mchana kwa mioyo Yao yote na kwa mapenzi kwa nchi Yao na kwako pia kama Mama na kiongozi wetu, hakika mpaka mchakato kufikia hapa hawajakuangusha maana sisi raia na wananchi wa kawaida tunaona juhudi zao na namna wanavyoifanya kazi uliyowatuma kwa nguvu na akili zao ZOTE.

Nne, Ninatambua kwamba zoezi Bado linaendelea lkn dalili ya mvua ni mawingu makarani wengi wamemaliza kuchukua taarifa Tena kwa usahihi kabisa hivyo tukutoe wasiwasi zoezi litakuwa na ufanisi sana maana limeratibiwa kitaalamu na wataalamu wako field kukamilisha machache sana yaliyobakia.

Tano, Eeee Mama baadhi ya wanao ni wakorofi, wachonganishi, wakosoaji wasio na adabu, wavivu kufikiri na wapingaji wa Kila jema ulifanyalo wewe na hata sisi wadogo zao kwenye Yale utuagizayo kuyafanya kwa ajili ya familia yetu TANZANIA.

Zoezi hili watalipinga, hawatayaona mafanikio na juhudi zako, na Mbaya zaidi watatukana Na kututukana sisi wadogo zao, watatunga uongo yaani Kila njia Mbaya ili tu kuonyesha haujafanya lolote la maana, tunakuomba uendelee kuwavumilia ni ndugu zetu hatuna namna tutaishi nao, tutawaelimisha kwa upendo mpaka wataelewa tu.

SITA, hivi mama kazi hili ikifikia ukomo hivi vishkwambi hauwezi kuwaachia wanao wa mwisho (MAKARANI) Ambao wengi ni waalimu Ili kuboresha elimu maana vinawapendezea kwelikweli😁😄😁😄😁😄😁

Mwisho, HONGERA HONGERA HONGERA SANA MAMA WEWE NI JEMBE HASWAA
###2020-2025 unatosha ### 2025-2030 ni wewe tu.
 
Aisee chief unatumia nguvu nyingi sana na naona ”Kurugenzi Shauri ya Ikulu” siku hizi hawapiti humu.

Nakushauri ingia kwenye website ya ikulu tafuta namba za Zuhra Yunus atakusaidia kuwasiliana na mama ili angalao upewe hata kazi ya ufagizi.
 
Nasisitiza tu kwamba Huwa siandiki jambo ili kupata teuzi ndugu ni kwa mapenzi kwa nchi yangu na raisi wangu ninamkubali kwa uongozi wake
 
Nasisitiza tu kwamba Huwa siandiki jambo ili kupata teuzi ndugu ni kwa mapenzi kwa nchi yangu na raisi wangu ninamkubali kwa uongozi wake
Watanzania wengi ni wanafiq.

Nimekwambia njia nzuri ya kupunguza njaa yako lakini bado unasema hufanyi kwa sababu ya njaa wakati wewe una njaa tu kama wengine.
 
Kitendo Cha Kamanda Mbowe kuwa Kimya toka Mama amtoe Lupango ni Ushahidi tosha kuwa Mama ni jembe ...!
Kamanda Kweli Wa Kuonekana mpaka misiba itokee..,?

ili Hali tozo imetamalaki Kila Kona?
ili Hali Lita Ya fuel bei haishikiki.?
ili Hali misaada Ya Kovidi tumepokea miujiza inaishia Wapi ndo hatuelewi.....!
ili Hali....

Enzi zile Sa' ivi angekuwa Yupo Mwanza au namtumbo Songea au Namanyele Kuongoza Kongamano La Kwanini ,Sembe bei'Juu wakati KATIBA BADO NI ILE ILE....!
Kweli Mama Jembe...!
 
Anatosha sana ila ni muhimu awadhibiti wabadhirifu na majizi ya pesa za umma ambayo yanadhani Mama ukimsifia tu basi inatosha !!
 
Kwani ndugu shibe ndio inamfanya mtu asipongeze jema? Au njaa ndio inamfanya mtu ajipendekeze? Kama ndiyo upinzani wanaokosoa wote ni matajiri? Au wote wapongezao serikali na raisi wake Wana njaa?
 
Aisee chief unatumia nguvu nyingi sana na naona ”Kurugenzi Shauri ya Ikulu” siku hizi hawapiti humu.

Nakushauri ingia kwenye website ya ikulu tafuta namba za Zuhra Yunus atakusaidia kuwasiliana na mama ili angalao upewe hata kazi ya ufagizi.

Kama wadau wa substance abuse...
Ahsante kwa kunidharau mkuu Sina Cha kusema nakutakia uvutaji mwema wa sigara BWEGE😆😆😆
 
Watanzania wengi ni wanafiq.

Nimekwambia njia nzuri ya kupunguza njaa yako lakini bado unasema hufanyi kwa sababu ya njaa wakati wewe una njaa tu kama wengine.
Sawa mkuu nimekuelewa hebu niwekee hiyo website ya ikulu hapa nichangamkie fursa
 
Kitendo Cha Kamanda Mbowe kuwa Kimya toka Mama amtoe Lupango ni Ushahidi tosha kuwa Mama ni jembe ...!
Kamanda Kweli Wa Kuonekana mpaka misiba itokee..,?

ili Hali tozo imetamalaki Kila Kona?
ili Hali Lita Ya fuel bei haishikiki.?
ili Hali misaada Ya Kovidi tumepokea miujiza inaishia Wapi ndo hatuelewi.....!
ili Hali....

Enzi zile Sa' ivi angekuwa Yupo Mwanza au namtumbo Songea au Namanyele Kuongoza Kongamano La Kwanini ,Sembe bei'Juu wakati KATIBA BADO NI ILE ILE....!
Kweli Mama Jembe...!
👍👏
 
Back
Top Bottom