Hongera rais Magufuli kuwapa vyeo vya utendaji walimu wa vyuo vikuu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Kitendo cha Rais kuwapa vyeo vya utendaji walimu wa vyuo vikuu kuna faida kubwa sana

1.Kuwapa nafasi ya kuyatumia yale waliyokuwa wakifundisha kwa vitendo.Wana uelewa mpana wa mambo mengi kuwateua katika nafasi mbali mbali za utendaji kutawapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao na nchi kuweza kupiga hatua.

2.Kunatoa nafasi ya wengine kupanda ili kuchukua nafasi zao.Akiondoka mmoja mwingine anasogea pale alipokuwa aliyeondoka.Hivyo mfumo huo unakuwa unasaidia kutengeneza viongozi wengi zaidi kwa ajili ya Taifa

3.Ni njia ya kuingiza mawazo mapya katika maeneo wanayoenda ambayo mengine unakuta walikuwa wamezoea kufanya kazi kimazoea.Akiletwa msomi mpya anaweza INJECT mawazo mapya kule aendapo na yule ambaye atachukua nafasi yake pale alipotoka aweza pia kuja na mikakati na mawazo mapya na hivyo kuzifanya sehemu zote kule alikotoka na kule alikoenda kuwa na tija mpya.

4.Kunaongeza ari na mori wa utendaji kazi.Akienda eneo jipya anakuwa na ari na mori wa kazi mpya na yule aliyepanda cheo anachochewa mori na ari ya kazi hivyo uzalishaji kuongezeka

5.Staili hii ya kuwateua inawafanya wafanye kazi walipo kwa moyo wakijua kuwa kazi yao yaweza onekana na raisi akawapa madaraka makubwa zaidi

6.Inasaidia kuongeza ajira.Mtu akiondoka lazima kutakuwa na nafasi ya kazi hapo moja itakayokuwa imezaliwa.

Napendekeza iundwe timu ya kusaka walimu wazuri wa vyuo ambao waweza kubaliana na kuendana na kasi ya Magufuli wasakwe kila kona na wapewe majukumu ya kitaifa.Watafutwe walimu watendaji sio wale akina yakhe ambao kutwa ni kupinga tu kila kitu anachofanya rais.
 
Mh. RAIS yupo SERIOUS kuifanya hii nchi kuwa katika level nyingine kabisa , hata kama hali ya maisha si nzuri kivilee ila WANANCHI tunaridhika na UTENDAJI WAKE ,huwezi kuifananisha tanzania na ZIMBABWE ya kwanza kwa dhahabu AFRICA.
 
haaaa haaa sasa nani atafundisha, aseeee nyie mnajitoa akili

Nyerere alipoondoka kufundisha kwenda kuwa raisi shule zilikosa walimu??? Wewe vipi? Wakiondoka wanakuja wengine kwani umeona Raisi anaenda anachukua walimu wote na kukiacha chuo kitupu hakina walimu? Hivi nyie UKAWA mmerogwa? Hata vitu vidogo hivi ni kupinga tuuuuu!! LOOOOO.

Roho zinawauma kwa kulia wivu.
 
Kitendo cha Raisi kuwapa vyeo vya utendaji walimu wa vyuo vikuu kuna faida kubwa sana

1.Kuwapa nafasi ya kuyatumia yale waliyokuwa wakifundisha kwa vitendo.Wana uelewa mpana wa mambo mengi kuwateua katika nafasi mbali mbali za utendaji kutawapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao na nchi kuweza kupiga hatua.

2.Kunatoa nafasi ya wengine kupanda ili kuchukua nafasi zao.Akiondoka mmoja mwingine anasogea pale alipokuwa aliyeondoka.Hivyo mfumo huo unakuwa unasaidia kutengeneza viongozi wengi zaidi kwa ajili ya Taifa

3.Ni njia ya kuingiza mawazo mapya katika maeneo wanayoenda ambayo mengine unakuta walikuwa wamezoea kufanya kazi kimazoea.Akiletwa msomi mpya anaweza INJECT mawazo mapya kule aendapo na yule ambaye atachukua nafasi yake pale alipotoka aweza pia kuja na mikakati na mawazo mapya na hivyo kuzifanya sehemu zote kule alikotoka na kule alikoenda kuwa na tija mpya.

4.Kunaongeza ari na mori wa utendaji kazi.Akienda eneo jipya anakuwa na ari na mori wa kazi mpya na yule aliyepanda cheo anachochewa mori na ari ya kazi hivyo uzalishaji kuongezeka

5.Staili hii ya kuwateua inawafanya wafanye kazi walipo kwa moyo wakijua kuwa kazi yao yaweza onekana na raisi akawapa madaraka makubwa zaidi

6.Inasaidia kuongeza ajira.Mtu akiondoka lazima kutakuwa na nafasi ya kazi hapo moja itakayokuwa imezaliwa.

Napendekeza iundwe timu ya kusaka walimu wazuri wa vyuo ambao waweza kubaliana na kuendana na kasi ya Magufuli wasakwe kila kona na wapewe majukumu ya kitaifa.Watafutwe walimu watendaji sio wale akina yakhe ambao kutwa ni kupinga tu kila kitu anachofanya raisi (domokaya)
Tatizo wasomi wetu ni waganga njaa.

Mhe. Dr. Mwakyembe katika thesis yake iliyompelekea kupata PhD alisapoti serikali tatu. Leo hii kapewa Uwaziri kabadilika na kuwa muumini wa serikali mbili.

Hao wasomi waliowekwa kwenye System hawatabadilisha lolote. Watafanya matakwa ya CCM na rais wake
 
Lumumba kumejaa mavijana yasiyokuwa na akili hata chembe! Walimu wa vyuo vikuu hawana weledi katika maswala ya uongozi, pia usikariri eti kile wanachofundisha kule kinaweza kubadili hali ya mambo kule waendako! Horrible way of thinking! Maghembe amefanya nini cha maana pamoja na kuwekwa kwenye eneo alilosomea? Huu ni ujinga wa fikra!
 
Mwalimu anatakiwa azalishe waalimu chini yake ili ufundishaji uwe endelevu... Siyo mtu akiondoka na ufundishaji unakufa. Kwani angefariki nani angefundisha?

Mkuu UKAWA hawaelewi kuandaa viongozi na huwa hawawaandai ndio maana hata mgombea uraisi miaka yote walikuwa hawajamwandaa wa kwao wakabeba mtu wa kuja Lowasa.Ukiwauliza hapo CHADEMA Mbowe akiondoka nani atashika nafasi utaona wanatoa mimacho tu na kuanza kufoka ohhh akitoka chama kitakufa hamna kutoka.Ukiwauliza SEIF SHARIF hamad ataachia nani huo ukatibu mkuu wa CUF utakuta wanafoka Maali hawezi toka ng`ooo.Hawaandai viongozi hao.Kwa hiyo kumwelewesha kuwa Mwalimu aweza tolewa na mambo yakaendelea kama kawaida kuelewa kwake inakuwa vigumu!! MSamehe bure mkuu.Alipo hivyo vitu havipo.
 
Tatizo wasomi wetu ni waganga njaa.

Mhe. Dr. Mwakyembe katika thesis yake iliyompelekea kupata PhD alisapoti serikali tatu. Leo hii kapewa Uwaziri kabadilika na kuwa muumini wa serikali mbili.

Hao wasomi waliowekwa kwenye System hawatabadilisha lolote. Watafanya matakwa ya CCM na rais wake
kwa hiyo mkuu ndo kusema mwakembe alidanganya katika ile thesis yake?.hua inafika mahali naaimini kua msomi wa kweli hawezi kukubali hivi vyeo vya kupewa kama peremende.kwasababu mwanataaluma wa ukweli hukisimamia anacho kiamini mpaka kufa kwake.sio hawa popo wa siku hizi inafika mahali tunashindwa kuwaamini wanataaluma wetu maana leo ataongea hivi na kesho atayakana aliyo yaongea.naomba aliye wahi kumsikia mwakyembe akieleza sababu za kukipinga alicho kitetea atuambie
 
Job k, kama walimu wa vyuo vikuu hawana weledi wanaweza vipi kuondaa vijana ambao wanaweledi unaotakiwa? Inaonekana hujaenda shule au chuo hata kidogo tu
 
kwa hiyo mkuu ndo kusema mwakembe alidanganya katika ile thesis yake?.hua inafika mahali naaimini kua msomi wa kweli hawezi kukubali hivi vyeo vya kupewa kama peremende.kwasababu mwanataaluma wa ukweli hukisimamia anacho kiamini mpaka kufa kwake.sio hawa popo wa siku hizi inafika mahali tunashindwa kuwaamini wanataaluma wetu maana leo ataongea hivi na kesho atayakana aliyo yaongea.naomba aliye wahi kumsikia mwakyembe akieleza sababu za kukipinga alicho kitetea atuambie

Hili ndo taifa la wasomi waganga njaa
 
Walimu wa vyuo vikuu hawana weledi katika maswala ya uongozi,

Kwa hiyo weledi ni CHADEMA walioshindwa uchaguzi? CHADEMA wangekuwa weledi si wangetoa raisi au spika!! Mbona wameishia kufunga matambara tu midomoni bungeni
 
Katika nchi yenye upungufu wa wahadhiri wa vyuo vikuu kama hii sidhani kama hilo linafaa kupongezwa ukizingatia na kasi ya ukwapuaji inayoendelea. Anaweza kuwatumia kama washauri zaidi kuliko utendaji.
 
Nchi ili iendelee inahitaji watu wenye akili nyingi wakae kila sekta sio vyuo vikuu pekee!!! Vyuo vikuu huwa vina best Brains ambao ni walimu.Wakirundikana sehemu moja haifai.Wanatakiwa wasambazwe kila kona wakatumie hizo akili nyingi walizonazo.Na ndicho Raisi anachofanya.Kulikuwa na ombwe la viongozi wenye akili nyingi maeneo mbalimbali.Vyuo panatakiwa pawe mahali pa kuzalishia na kukomaza mtu akikomaa anapelekwa sehemu nyingine sio pawe mahali pa mtu kuzaliwa na kufia hapo kama mwalimu
 
Back
Top Bottom