Hongera rais Magufuli kuwapa vyeo vya utendaji walimu wa vyuo vikuu

Tatizo wasomi wetu ni waganga njaa.

Mhe. Dr. Mwakyembe katika thesis yake iliyompelekea kupata PhD alisapoti serikali tatu. Leo hii kapewa Uwaziri kabadilika na kuwa muumini wa serikali mbili.

Hao wasomi waliowekwa kwenye System hawatabadilisha lolote. Watafanya matakwa ya CCM na rais wake
Nilicheka sana Siku mwakyembe
anakana nukuu za kwenye kitabu chake
Ndio nikaamini ukishakuwa ccm huwez fanya lolote kwa manufaa ya nchi
 
Maprofesa na Doctors hawatakiwi kuwa kwenye teuzi za kisiasa. Ni kudumaza sekta ya elimu na utafiti
 
Maprofesa na Doctors hawatakiwi kuwa kwenye teuzi za kisiasa. Ni kudumaza sekta ya elimu na utafiti
Wanapelekwa kwenye maeneo ya kutumia utaalamu sio kwenye ofisi ya siasa kama akina profesa baregu,Profesa Lipumba na Profesa SAFARI!! Wote walioteuliwa na Magufuli umeona kuna aliyeteuliwa kuwa kiongozi wa CCM?

TAFITI ZAO WATAENDA KUZIFANYA KWENYE MAENEO WAENDAYO KUONA KWA NINI YAKO HIVI NA NINI KIFANYIKE YAFANYE VIZURI.

Majibu watakayopata kwenye hizo tafiti watayafanyia kazi badala ya kuyaweka maktaba vyuoni kwao na kulalamika kuwa wanafanya tafiti nyingi na hazifanyiwi kazi na watendaji.
 
Nilicheka sana Siku mwakyembe
anakana nukuu za kwenye kitabu chake
Ndio nikaamini ukishakuwa ccm huwez fanya lolote kwa manufaa ya nchi

Mwalimu Nyerere ambaye tunamuheshimu sana katika siasa za nchi Hii Alikuwa muasisi wa Chama kimoja. Lakini yeye ndiye pia alibadilisha mtazamo na mwelekeo wa siasa nchi Hii na kuingia vyama vingi. Politics is dynamic ...
 
It's a shame wasomi kuwa watumwa wa siasa. Na hichi ndo kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi

Sio watumwa walisoma ili wawatumikie wananchi.Magufuli anawapa nafasi waeende kuwatumikia wananchi moja kwa moja badala ya kujifungia madarasani na projector wakifundisha
 
Kitendo cha Rais kuwapa vyeo vya utendaji walimu wa vyuo vikuu kuna faida kubwa sana

1.Kuwapa nafasi ya kuyatumia yale waliyokuwa wakifundisha kwa vitendo.Wana uelewa mpana wa mambo mengi kuwateua katika nafasi mbali mbali za utendaji kutawapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao na nchi kuweza kupiga hatua.

2.Kunatoa nafasi ya wengine kupanda ili kuchukua nafasi zao.Akiondoka mmoja mwingine anasogea pale alipokuwa aliyeondoka.Hivyo mfumo huo unakuwa unasaidia kutengeneza viongozi wengi zaidi kwa ajili ya Taifa

3.Ni njia ya kuingiza mawazo mapya katika maeneo wanayoenda ambayo mengine unakuta walikuwa wamezoea kufanya kazi kimazoea.Akiletwa msomi mpya anaweza INJECT mawazo mapya kule aendapo na yule ambaye atachukua nafasi yake pale alipotoka aweza pia kuja na mikakati na mawazo mapya na hivyo kuzifanya sehemu zote kule alikotoka na kule alikoenda kuwa na tija mpya.

4.Kunaongeza ari na mori wa utendaji kazi.Akienda eneo jipya anakuwa na ari na mori wa kazi mpya na yule aliyepanda cheo anachochewa mori na ari ya kazi hivyo uzalishaji kuongezeka

5.Staili hii ya kuwateua inawafanya wafanye kazi walipo kwa moyo wakijua kuwa kazi yao yaweza onekana na raisi akawapa madaraka makubwa zaidi

6.Inasaidia kuongeza ajira.Mtu akiondoka lazima kutakuwa na nafasi ya kazi hapo moja itakayokuwa imezaliwa.

Napendekeza iundwe timu ya kusaka walimu wazuri wa vyuo ambao waweza kubaliana na kuendana na kasi ya Magufuli wasakwe kila kona na wapewe majukumu ya kitaifa.Watafutwe walimu watendaji sio wale akina yakhe ambao kutwa ni kupinga tu kila kitu anachofanya rais.
Kwa hiyo huko vyuoni nani wanafundisha. Tumepiga kelele kila siku kuwa tuna upungufu wa waalimu, leo waalimu wanabebana kuwa viongozi wa serikali kuu na pengine na za mitaa. Halafu tuendelee kudanganyana kuwa elimu itakuwa nzuri, kwa vipi?
 
Sio watumwa walisoma ili wawatumikie wananchi.Magufuli anawapa nafasi waeende kuwatumikia wananchi moja kwa moja badala ya kujifungia madarasani na projector wakifundisha
sasa mbona hawayatendi waliokuwa wanayafundisha darasani?
 
Nchi ili iendelee inahitaji watu wenye akili nyingi wakae kila sekta sio vyuo vikuu pekee!!! Vyuo vikuu huwa vina best Brains ambao ni walimu.Wakirundikana sehemu moja haifai.Wanatakiwa wasambazwe kila kona wakatumie hizo akili nyingi walizonazo.Na ndicho Raisi anachofanya.Kulikuwa na ombwe la viongozi wenye akili nyingi maeneo mbalimbali.Vyuo panatakiwa pawe mahali pa kuzalishia na kukomaza mtu akikomaa anapelekwa sehemu nyingine sio pawe mahali pa mtu kuzaliwa na kufia hapo kama mwalimu
Kwa hiyo akili nyingi wanazo wahadhiri pekee nchi hii?
 
Nyerere alipoondoka kufundisha kwenda kuwa raisi shule zilikosa walimu??? Wewe vipi? Wakiondoka wanakuja wengine kwani umeona Raisi anaenda anachukua walimu wote na kukiacha chuo kitupu hakina walimu? Hivi nyie UKAWA mmerogwa? Hata vitu vidogo hivi ni kupinga tuuuuu!! LOOOOO.

Roho zinawauma kwa kulia wivu.
Hawana jema aalofanya Rais ukweli tumewachoka. Jamani asante Mungu watu hawa hawakupewa madaraka maana hata hawajui wafanyalo.Ingekuwa Urais wa kujaribishwa wangeopewa mwaka mmoja tutuwaone wangefanya nini. Go Magufuli go. Watu walizoea Viongozi wenye elimu ndogo!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom