Profesa Buchwe napenda kukupongeza kwa dhati kabisa kwa kuteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya TIB.
Sina wasiwasi na weledi, utendaji wako na taaluma yako ndani ya nchi hii. Tanzania inajivunia kuwa na Profesa wa Chemistry ambaye amewahi kumsimamia (supervise) mwanafunzi wa PhD katika idara ya Kemia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye leo ni Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Si kazi rahisi kushape mwanafunzi wa PhD hadi anapita viva vos katika kutetea thesis yake lakini iliwezekana.
Natambua kazi hii uliifanya kama timu wakati Mkuu wa Idara ya Kemia akiwa Dr. Mubofu ambaye leo ni Mkurugenzi Mkuu mpya wa TBS baada ya aliyekuwa katika nafasi hiyo (Joseph Masikitiko) kusimamishwa kazi pamoja Mkurugenzi wake wa Fedha. Masikitiko hakuwa hata na taaluma ya sayansi lakini alikuwa akisimamia shirika ambalo utendaji wake wa kila siku ulihitaji maarifa ya sayansi - maajabu ya nchi yetu, lakini bora alitumbuliwa.
Binafsi najivunia kuwa alumini wa Idara ya Kemia, UDSM, Idara ambayo imemfunza Rais wa nchi katika mchepuo wa Kemia kwa kiwango cha PhD.
Kazi njema Profesa.