Kuelekea 2025 Morris Makoi Vs Prof. Ndakidemi moto utawaka 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ndagullachrles

Senior Member
Jun 20, 2023
139
147
Jumatano wiki hii watanzania watakuwa kwenye zoezi la upigaji kura kuwachagua wenyeviti wa serikali za mitaa,wajumbe wa serikali za mitaa na wenyeviti wa vijiji.

Kutokana na jambo hilo serikali imetangaza jumatano ya Novemba 27 kuwa siku ya mapumziko Ili kutoa nafasi kwa wananchi kushiriki tukio hilo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Baada ya kumalizika kwa tukio hilo ,hapana shaka, macho na masikio ya watanzania sasa yataelekezwa kwenye uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani.

Leo naangazia siasa za Jimbo la moshi Vijijini ambako mbunge wa sasa ni Profesa Patrick Ndakidemi.

Katika uchaguzi ujao hapo mwakani Profesa Ndakidemi anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi Vijijini, Morris Makoi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Okaoni.

Kwenye kura za maoni mwaka 2020 Makoi alishika nafasi ya tatu nyuma ya Deo Mushi na Ndakidemi mwenyewe ambaye aliongoza kwenye kura za maoni .

Wachambuzi wa siasa za Kilimanjaro wanasema Makoi kwa sasa amekuwa na uungwaji mkono na wananchi wengi wa Jimbo la Moshi Vijijini kutokana na kuwa Karibu na wananchi kupitia kofia yake ya mwenyekiti wa Halmashauri .

"Kaka nikuhakikishie tu kwamba mwakani moto utawaka,tunataka mabadiliko,mzee wetu huu ni muda wake wa kupumzika awachie vijana",anasema kada mmoja kutoka Kata ya Old Moshi Mashariki .

Kumekuwepo na changamoto kadhaa kwa wananchi Jimbo hilo hasa ukanda wa chini ikiwamo changamoto ya maji,tatizo la miundombinu ya barabara hasa barabara ya kutoka Geti Fonga, Mabogini hadi Kahe.

Kwa muda mrefu wananchi wa ukanda wa chini wamekuwa wakilalamilikia changamoto hiyo japo kwa sasa ujenzi wa Barbara hiyo umeanza kwa kusuasua.

Changamoto hizo zinatajwa kama kikwazo kwa Profesa Ndakidemi kuweza kutetea Kiti chake kwa kile kinachoelezwa kuwa ameshindwa kizitatua changamoto hizo.

"Nenda kule Chekereni ya Bonite,angalia hiyo barabara yetu,tumepiga kelele mpaka tumeamua kunyamaza,watu wengi wanaua magari yao kutokana na ubovu wa Barbara na mbunge yupo ".anasema mwananchi mmoja .

Kazi ipo
 
Uchaguzi ukifanyika leo huyo Morris Makoyi akitokea akagombea atamshinda ndakidemi .

Makoy Jina lake limekuwa likitajwa sehemu nyingi za akina Mangi hususani Miji ya Dar es salaam na Arusha kuwa jamaa ni mtu wa kazi sana
 
Back
Top Bottom