Elections 2010 Hongera mh. Dk. Jakaya M. Kikwete

Mwanamageuko kwani wewe ni ridhiwani au mtoto wa kambo wa kikwete, mbona unamwita kikwete baba?
Remoteattacks hivi baba yako akikuita baba huwa umekuwa baba yake???:smile-big: wapo wanaoita watu wakombozi na ilhali wao hawajakombolewa inakuwaje hapo??? yapo maandiko; wala msimwite mtu baba duniani... lakini leo hii kuna mababa wangapi? na tena hao wanaoitwa ma-baba hata wake hawana huwa wamewazaa???
 
Kiherehere chako! Hupati promotion Ng'0!!!! Unajipendekeza utadhani sijui nini.

SEMA ANDIKA TUKANA HUWEZI BADILI MATOKEO MIMI MWANMGEUKO NAMUUNGA MKONO RAIS NDO HUYO ALIYETUKANWA PALE MWEMBE YANGA TANDIKA NA MWANA CHADEMA KAMA WEWE NEMBO YAKO HAIJIFICHI NAKUPA MWAKA NA CHAMA CHAKO ww ndo watakupa promotion uwe mstaarabu na lugha
 
Mungi tizama ukweli acha kupinga kila kitu, wewe vp aisee ?
:cool2: Jiniazbrein, wala usichukie pale unapoziona lugha tofauti zimetumika, bali wapaswa kuzijua lugha hizo zatokana na nini .... :gossip: ukishalijua hilo NDIPO WAPATA PICHA HII: TUKIWA NA MATATIZO YA MENO, TWAONA Dentist, IKIWA UONI WETU wa MACHO NI HAFIFU TWAWAONA MA-Optometrist. sasa kwa makini sana zingatia hili neno (tafakari ukiwa peke yako maana watu wanaeza kujiuliza unacheka nini na kompyuta yako) MTU AKIWA NA TATIZO LA UONI HAFIFU huitiwa Neurologists!! Ndio maana nilisema tutafute darubini ili tuone mbali... Uoni wetu bado ni hafifu na hatujui kama hatuoni :smile-big: Mkuu Jiniaz, hapo umenipata???:smile-big:
 
Hongera baba kwa kuchaguliwa, kuteuliwa kisha kuapishwa kwako kuwa rais wa hii Jamhuri yetu ya Tanzania,
Hatuna Rais mwingine badala yako, kwenye ile hotuba fupi uliwaasa WAANDISHI na wale wamiliki VITANGAZIO, baba napenda kukukumbusha ulisahau WALE MAFARISAYO NA MASADUKAYO wanaotuhudumia sie tulio chini. Hususan wale wanaokaa kule kuitwako TAAHAMSEMI. Huko ndiko majeraha yatakosiginwa na kutiwa chumvi, ee baba ujue ufalme wako hautaishia hapo MAGOGONI, upitepite Manzese kama upitavyo Kariakoo na kwengine kama alivopitaga hayati Sokoine, Ninajua majukumu yako mengi na nchi ni kubwa lakini hii leo si kubwa kama wakati ule wa usafiri wa tabu (kutoka Mwanza kwenda Shinyanga siku nzima, wachilia mbali Dar kwenda Mtwara kwa barabara. Upite hata kule Lipumba alikopita akakwama na kule Slaa alikokuta watu wanaishi mashimoni kama... na kwenye tembe karne hii. Baba si vibaya ukawatuma hata WATANI zako wa KISIASA kwa kufanya kwao MIKUTANO ya hadhara huko mikoani UTAWEZA kupata kero za WANANCHI kuliko kusubiri kuambiwa na BABA yetu MAKAMBA kila kitu kiko shwari. Nayasema hayo kwa SABABU ni RAHISI kwa WATANI wako KUONANA na WANANCHI kuliko wewe KWA MAANA WANAFUNZI WAKO HUWAZUILIA NJIA WANAOKUFUATA. Ndio maana wao HUKUCHAGULIA MAGAZETI YA KUSOMA na YALE MENGINE UNAYOYAPENDA HUTAKA KUYAFUNGIA. Hii ni nchi yetu sote ndio maana kina sisi tulibaki hatukujilipua kama walivyojilipua wale wenzetu. Wataalamu waliopo Tanganyika wathaminike kama walivyothaminika wa Zanzibar kwani mchango wao ni mkubwa. Wasithaminike wale watoto wa waliokaribu ya ufalme wake kwa maana hawakusomea maarifa bali vyeti. Ili waliojilipua warudi na kujenga nchi hii... Mungu Ibariki Tanzania.

Niishie hapa nisikuchoshe kwa leo,

Wasalaam,

Wako katika ujenzi wa Taifa.

Mwanamageuko.

Kweli wewe ni "Shake well"
 
Back
Top Bottom