Elections 2015 Hongera Lowassa: Wewe ni bingwa wa siasa za Tanzania

Nimeamini Lowassa ni bingwa wa siasa za Tanzania, na anastahili heshima,huyu mtu anajua kucheza na siasa zetu hadi maadui zake anawageuza na kuwafanya wafuasi wake watiifu.

Nani alitegemea Toka kashifa ya Richmond baada ya miaka nane Lowassa angekuja kuwa mkuu wa siasa za upinzani Tanzania, Mkuu wa wanasiasa wa upinzani Tanzania , Mkuu wa vyama vya upinzani Tanzania , Mkuu wa wale makamanda hatari wa kupiga vita ufisadi Tanzania ,Mbaya zaidi mgombea wao pekee na aliepita Bila kupingwa.?

Nani alitegemea leo Mbowe, Msigwa, Mdee na Lema wangepangiwa cha kuongea kwenye majukwaa ya kisiasa na Lowassa, nani alitegemea angetoa amri wafunge midomo kuhusu ufisadi na wakatii Bila shuruti, kwa hili Lowassa anastahili heshima ya kipekee hapa nchini.

Amewafanya maadui zake wamwombe radhi, wamsafishe , wamsujudu, wamtetemekee kiasi kwamba akitoa kauli inakuwa ndio sheria,na wanatiii Bila shuruti.

Hakuna heshima kubwa kama kumgeuza adui yako mkuu awe mfuasi wako mtiifu na mwaminifu kwako.

Naamini Lowassa alivyokatwa Dodoma alikata tamaa kabisa na siasa za Tanzania hasa kwenye URAIS,

Ila swala moja lilikuwa linamuumiza ni vipi atasafisha Jina Lake kupitia upinzani hasa Chadema ya Mbowe na Dr.Slaa, ili atakavyotulia kwenye ranch zake anakula mafao na wajukuu zake zisiwepo kelele za kumghasi.

Ndipo akajitoa mzima mzima kwenda Chadema kwa gharama zake na jamaa zake ambao amekuwa akichafuliwa nao siku zote. Lengo kumsafisha yeye na binafsi na jamaa zake hasa Rostam , Chenge, Karamagi nk.

Na kwa hilo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, japo itamuuma sana kumkosa mpiganaji namba moja wa ufisadi Tanzania Dr.Slaa, na huyu ndio lilikuwa lengo lake kuu, hakika Dr. Slaa angenasa kwenye mtego huu Lowassa angekua na amani maisha yake yote yaliyobaki duniani bahati mbaya Dr.slaa akashituka mapema.

Ila kwa sasa Lowassa ni kama ameteka kambi nzima ya maadui, ila kiongozi mkuu wa waasi Dr.Slaa ametoroka dakika za mwisho.

Baada ya Octoba 25 Lowassa atastaafu siasa na kwenda kupumuzika kwenye ranch zake na mahoteli yaliyoenea nchi nzima, huku akiwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulipa kisasi na kuacha majeraha makubwa ndani ya Chadema na siasa za upinzani kwa ujumla.

Hongera Lowassa, Hatimaye sasa utapumzika kwa amani Bila bugudha, huku siasa za upinzani hasa Chadema zikiendelea kukupigia magoti kwa maumivu makali ya kutoaminika tena kwa wananchi hasa wapenda mabadiliko ya ukweli.!

Upinzani si kuchukiana, bali ni kuicheki serikali kama inafanya kazi sawa. Kama inafanya vizuri wapinzani waiunge mkono, Na kama inakosea basi wanaikosowa kwa mawazo ya kusaidia. Mbowe na Lissu ni matusi kwa kutumia jina demokrasia, demokrasia gani hiyo? Watabaki wawili kwenye chama kila mtu ananyatuka
 
Hatimaye yametimia, wengine tuliyaona toka awali kuwa jamaa amekuja kulipa kisasi tu.... Na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa laana imwandame Mbowe.
 
Hili Kaburi pia ni chungu sana kwa Makarai Kama lile pia Pasco alilotabiri kuwa Edward angegombea kupitia Ukawa?

Chadema wamefundishwa Siasa na CCM Safari Hii!
Hatimae jamaa kaacha majereha makubwa sana kwenye siasa za upinzani Tanzania.
 
Ukitazama kwa namna flani mtoa mada uko sahihi ingawa ukweli unauma na wengi watakupinga..Ila sio kwa kujibu hoja yako
Leo kiko wazi tulichokiongea miaka kadhaa nyuma.
 
Nimeamini Lowassa ni bingwa wa siasa za Tanzania, na anastahili heshima,huyu mtu anajua kucheza na siasa zetu hadi maadui zake anawageuza na kuwafanya wafuasi wake watiifu.

Nani alitegemea Toka kashifa ya Richmond baada ya miaka nane Lowassa angekuja kuwa mkuu wa siasa za upinzani Tanzania, Mkuu wa wanasiasa wa upinzani Tanzania , Mkuu wa vyama vya upinzani Tanzania , Mkuu wa wale makamanda hatari wa kupiga vita ufisadi Tanzania ,Mbaya zaidi mgombea wao pekee na aliepita Bila kupingwa.?

Nani alitegemea leo Mbowe, Msigwa, Mdee na Lema wangepangiwa cha kuongea kwenye majukwaa ya kisiasa na Lowassa, nani alitegemea angetoa amri wafunge midomo kuhusu ufisadi na wakatii Bila shuruti, kwa hili Lowassa anastahili heshima ya kipekee hapa nchini.

Amewafanya maadui zake wamwombe radhi, wamsafishe , wamsujudu, wamtetemekee kiasi kwamba akitoa kauli inakuwa ndio sheria,na wanatiii Bila shuruti.

Hakuna heshima kubwa kama kumgeuza adui yako mkuu awe mfuasi wako mtiifu na mwaminifu kwako.

Naamini Lowassa alivyokatwa Dodoma alikata tamaa kabisa na siasa za Tanzania hasa kwenye URAIS,

Ila swala moja lilikuwa linamuumiza ni vipi atasafisha Jina Lake kupitia upinzani hasa Chadema ya Mbowe na Dr.Slaa, ili atakavyotulia kwenye ranch zake anakula mafao na wajukuu zake zisiwepo kelele za kumghasi.

Ndipo akajitoa mzima mzima kwenda Chadema kwa gharama zake na jamaa zake ambao amekuwa akichafuliwa nao siku zote. Lengo kumsafisha yeye na binafsi na jamaa zake hasa Rostam , Chenge, Karamagi nk.

Na kwa hilo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, japo itamuuma sana kumkosa mpiganaji namba moja wa ufisadi Tanzania Dr.Slaa, na huyu ndio lilikuwa lengo lake kuu, hakika Dr. Slaa angenasa kwenye mtego huu Lowassa angekua na amani maisha yake yote yaliyobaki duniani bahati mbaya Dr.slaa akashituka mapema.

Ila kwa sasa Lowassa ni kama ameteka kambi nzima ya maadui, ila kiongozi mkuu wa waasi Dr.Slaa ametoroka dakika za mwisho.

Baada ya Octoba 25 Lowassa atastaafu siasa na kwenda kupumuzika kwenye ranch zake na mahoteli yaliyoenea nchi nzima, huku akiwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulipa kisasi na kuacha majeraha makubwa ndani ya Chadema na siasa za upinzani kwa ujumla.

Hongera Lowassa, Hatimaye sasa utapumzika kwa amani Bila bugudha, huku siasa za upinzani hasa Chadema zikiendelea kukupigia magoti kwa maumivu makali ya kutoaminika tena kwa wananchi hasa wapenda mabadiliko ya ukweli.!
Niliamua kuachana na siasa rasmi Mh Lowasa alipo jiunga Chadema. Nawahurumia vijana waliojiunga kushabikia siasa na kupoteza wakati na heshima kwenye jamii. Ni muda wa kujitafakari kwa upya. Pole Kaka yangu Mbowe Pole Tanzania.

Ishi halisi
 
Maamuzi ya Mbowe 2015 hayakustahili kuungwa mkono kwa namna yoyote ile, ila mihemko ya kisiasa na uwezo mdogo wa kuona mbali ulifanya watu washangilie ule upuuzi.
 
Acha tu, kwa hali ilivyo akitoka jela aunge mkono juhudi aponde maisha.

Back
Top Bottom