Hongera Lowassa: Wewe ni bingwa wa siasa za Tanzania | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Lowassa: Wewe ni bingwa wa siasa za Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by idawa, Oct 1, 2015.

  1. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #1
    Oct 1, 2015
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    Nimeamini Lowassa ni bingwa wa siasa za Tanzania, na anastahili heshima,huyu mtu anajua kucheza na siasa zetu hadi maadui zake anawageuza na kuwafanya wafuasi wake watiifu.

    Nani alitegemea Toka kashifa ya Richmond baada ya miaka nane Lowassa angekuja kuwa mkuu wa siasa za upinzani Tanzania, Mkuu wa wanasiasa wa upinzani Tanzania , Mkuu wa vyama vya upinzani Tanzania , Mkuu wa wale makamanda hatari wa kupiga vita ufisadi Tanzania ,Mbaya zaidi mgombea wao pekee na aliepita Bila kupingwa.?

    Nani alitegemea leo Mbowe, Msigwa, Mdee na Lema wangepangiwa cha kuongea kwenye majukwaa ya kisiasa na Lowassa, nani alitegemea angetoa amri wafunge midomo kuhusu ufisadi na wakatii Bila shuruti, kwa hili Lowassa anastahili heshima ya kipekee hapa nchini.

    Amewafanya maadui zake wamwombe radhi, wamsafishe , wamsujudu, wamtetemekee kiasi kwamba akitoa kauli inakuwa ndio sheria,na wanatiii Bila shuruti.

    Hakuna heshima kubwa kama kumgeuza adui yako mkuu awe mfuasi wako mtiifu na mwaminifu kwako.

    Naamini Lowassa alivyokatwa Dodoma alikata tamaa kabisa na siasa za Tanzania hasa kwenye URAIS,

    Ila swala moja lilikuwa linamuumiza ni vipi atasafisha Jina Lake kupitia upinzani hasa Chadema ya Mbowe na Dr.Slaa, ili atakavyotulia kwenye ranch zake anakula mafao na wajukuu zake zisiwepo kelele za kumghasi.

    Ndipo akajitoa mzima mzima kwenda Chadema kwa gharama zake na jamaa zake ambao amekuwa akichafuliwa nao siku zote. Lengo kumsafisha yeye na binafsi na jamaa zake hasa Rostam , Chenge, Karamagi nk.

    Na kwa hilo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, japo itamuuma sana kumkosa mpiganaji namba moja wa ufisadi Tanzania Dr.Slaa, na huyu ndio lilikuwa lengo lake kuu, hakika Dr. Slaa angenasa kwenye mtego huu Lowassa angekua na amani maisha yake yote yaliyobaki duniani bahati mbaya Dr.slaa akashituka mapema.

    Ila kwa sasa Lowassa ni kama ameteka kambi nzima ya maadui, ila kiongozi mkuu wa waasi Dr.Slaa ametoroka dakika za mwisho.

    Baada ya Octoba 25 Lowassa atastaafu siasa na kwenda kupumuzika kwenye ranch zake na mahoteli yaliyoenea nchi nzima, huku akiwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulipa kisasi na kuacha majeraha makubwa ndani ya Chadema na siasa za upinzani kwa ujumla.

    Hongera Lowassa, Hatimaye sasa utapumzika kwa amani Bila bugudha, huku siasa za upinzani hasa Chadema zikiendelea kukupigia magoti kwa maumivu makali ya kutoaminika tena kwa wananchi hasa wapenda mabadiliko ya ukweli.!
     
  2. m

    mangatara JF-Expert Member

    #41
    Oct 1, 2015
    Joined: Jul 6, 2012
    Messages: 10,018
    Likes Received: 5,615
    Trophy Points: 280
    Bayona;
    Usimwonee mtu, uwe mkweli tu na mengine yoote yatajisema tuu. Tangu lini Lowasa akatekeleza kitu?? Wali mkata kwa sababu aliwaambia kuwa akishika atatenda tofauti na sera zao.
    ccm hawajawahi kutaka kuuondoa umasikini kwani wanajua watu wakiondokewa na umasikini hawatawachagua tena. Ndo maana tunakuambia chagua UKAWA uone MABADILIKOOOOOO. Usiwasikilize ccm ati nao wanasema wataleta mabadiliko. Wenyewe wanaimba kuwa ccm ni ile ile hivyo ukiwachagua usijelia kama hakuna mabadiliko
     
  3. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #42
    Oct 1, 2015
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    Mkuu umesahau kuwa Lowassa alikuwa waziri wa maji Enzi za Mkapa, je alilifanyia nini Taifa na kero ya maji.!
     
  4. m

    makundubhyali JF-Expert Member

    #43
    Oct 1, 2015
    Joined: May 26, 2013
    Messages: 2,213
    Likes Received: 100
    Trophy Points: 160
    Kisasi ulimkosea nini mkuu !! leo umenifanya nielewe kwa nini CCM wanapigana kufa na kupona ili wasije shughulikiwa na Lowassa !! asante sana mkuu.
     
  5. m

    mangatara JF-Expert Member

    #44
    Oct 2, 2015
    Joined: Jul 6, 2012
    Messages: 10,018
    Likes Received: 5,615
    Trophy Points: 280
    Bayona;
    Nashukuru umeelewa kuwa alikuwa mtiifu kutekeleza yalokuwa kwenye ilani yao ambayo haya anayotaka kutekeleza hayakuwemo.
    Mpe kura yako this tyme na atakutimizia yote alio nayo kwenye ilani mpya kwani huyu ni mtiifu sana
     
  6. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #45
    Apr 24, 2016
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    Poleni wapinzani
     
  7. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #46
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    Huyo ndio Lowasa bwana
     
  8. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #47
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    Lowasa hatimae kurudi kwao.
     
  9. Msafirishaji

    Msafirishaji JF-Expert Member

    #48
    Jan 9, 2018
    Joined: May 28, 2016
    Messages: 1,102
    Likes Received: 1,341
    Trophy Points: 280
    Mkuu ulisema nini hii 2015
     
  10. Msafirishaji

    Msafirishaji JF-Expert Member

    #49
    Jan 9, 2018
    Joined: May 28, 2016
    Messages: 1,102
    Likes Received: 1,341
    Trophy Points: 280
    Makamanda Wana wayawaya
     
  11. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #50
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    Mkuu vipi kwema lakini.
     
  12. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #51
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    Tuliwaambia hawakuamini sasa wamebaki kulumbana wenyewe kwa wenyewe.
     
  13. Tajirimsomi

    Tajirimsomi JF-Expert Member

    #52
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 12, 2017
    Messages: 4,190
    Likes Received: 4,209
    Trophy Points: 280
    Kuna mwanajamii forum alisema magufuli unaweza kumsema vibaya vyovyote ukiwa mbali ila ukibahatika kukutana naye utajikuta unapata upako wa kumkubali na kunsifia kama alivyofanya lowassa Leo.
     
  14. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #53
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    Nami nasikia Magufuli ni mzuri kumsikia kwenye tv lakini sio live hivi.
    Hata kama ulikuwa na hoja za kumpinga ukikutana nae lazima unywee.
     
  15. Tajirimsomi

    Tajirimsomi JF-Expert Member

    #54
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 12, 2017
    Messages: 4,190
    Likes Received: 4,209
    Trophy Points: 280
    Hahaha kwa kumuogopa au point zinakosa mashiko
     
  16. idawa

    idawa JF-Expert Member

    #55
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 20, 2012
    Messages: 18,520
    Likes Received: 10,438
    Trophy Points: 280
    jamaa anatisha sana ukikaa naye jirani.....ni kama unaongea na Simba.
     
  17. Tajirimsomi

    Tajirimsomi JF-Expert Member

    #56
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 12, 2017
    Messages: 4,190
    Likes Received: 4,209
    Trophy Points: 280
    Mimi nilikuwa simkubali ila nilipokutana naye mwanza kidogo kuna vielement vya kumkubali vilianza kuota kichwani jamaa atakuwa anajipaka mafuta ya simba akichanganya na ya twiga
     
  18. B

    Blac kid JF-Expert Member

    #57
    Jan 9, 2018
    Joined: Apr 1, 2012
    Messages: 3,365
    Likes Received: 130
    Trophy Points: 160
    Kwema kabisa naona unafukua makaburi mie siasa za bongo nimebaki observer tu hahahah!
     
  19. D

    David Mkapa Member

    #58
    Jan 9, 2018
    Joined: Dec 20, 2017
    Messages: 8
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 5
    Punguza hasira mzee
     
  20. Ilankunda1234

    Ilankunda1234 JF-Expert Member

    #59
    Jan 9, 2018
    Joined: Dec 28, 2015
    Messages: 3,289
    Likes Received: 2,371
    Trophy Points: 280
    Yaaani nimecheka mpaka naonekana kitu nilipoulizwa unacheka nini nikawaonyesha mdahalo wenu huu

    Kuna aliecheka mpaka kajamba
     
  21. Tajirimsomi

    Tajirimsomi JF-Expert Member

    #60
    Jan 9, 2018
    Joined: Jan 12, 2017
    Messages: 4,190
    Likes Received: 4,209
    Trophy Points: 280
    Hahah kwanini mkuu ni kweli hata mbowe akikutana naye naamini atamsifia tu
     
Loading...