Hongera Lowassa: Wewe ni bingwa wa siasa za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Lowassa: Wewe ni bingwa wa siasa za Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by idawa, Oct 1, 2015.

 1. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2015
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 19,253
  Likes Received: 12,234
  Trophy Points: 280
  Nimeamini Lowassa ni bingwa wa siasa za Tanzania, na anastahili heshima,huyu mtu anajua kucheza na siasa zetu hadi maadui zake anawageuza na kuwafanya wafuasi wake watiifu.

  Nani alitegemea Toka kashifa ya Richmond baada ya miaka nane Lowassa angekuja kuwa mkuu wa siasa za upinzani Tanzania, Mkuu wa wanasiasa wa upinzani Tanzania , Mkuu wa vyama vya upinzani Tanzania , Mkuu wa wale makamanda hatari wa kupiga vita ufisadi Tanzania ,Mbaya zaidi mgombea wao pekee na aliepita Bila kupingwa.?

  Nani alitegemea leo Mbowe, Msigwa, Mdee na Lema wangepangiwa cha kuongea kwenye majukwaa ya kisiasa na Lowassa, nani alitegemea angetoa amri wafunge midomo kuhusu ufisadi na wakatii Bila shuruti, kwa hili Lowassa anastahili heshima ya kipekee hapa nchini.

  Amewafanya maadui zake wamwombe radhi, wamsafishe , wamsujudu, wamtetemekee kiasi kwamba akitoa kauli inakuwa ndio sheria,na wanatiii Bila shuruti.

  Hakuna heshima kubwa kama kumgeuza adui yako mkuu awe mfuasi wako mtiifu na mwaminifu kwako.

  Naamini Lowassa alivyokatwa Dodoma alikata tamaa kabisa na siasa za Tanzania hasa kwenye URAIS,

  Ila swala moja lilikuwa linamuumiza ni vipi atasafisha Jina Lake kupitia upinzani hasa Chadema ya Mbowe na Dr.Slaa, ili atakavyotulia kwenye ranch zake anakula mafao na wajukuu zake zisiwepo kelele za kumghasi.

  Ndipo akajitoa mzima mzima kwenda Chadema kwa gharama zake na jamaa zake ambao amekuwa akichafuliwa nao siku zote. Lengo kumsafisha yeye na binafsi na jamaa zake hasa Rostam , Chenge, Karamagi nk.

  Na kwa hilo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, japo itamuuma sana kumkosa mpiganaji namba moja wa ufisadi Tanzania Dr.Slaa, na huyu ndio lilikuwa lengo lake kuu, hakika Dr. Slaa angenasa kwenye mtego huu Lowassa angekua na amani maisha yake yote yaliyobaki duniani bahati mbaya Dr.slaa akashituka mapema.

  Ila kwa sasa Lowassa ni kama ameteka kambi nzima ya maadui, ila kiongozi mkuu wa waasi Dr.Slaa ametoroka dakika za mwisho.

  Baada ya Octoba 25 Lowassa atastaafu siasa na kwenda kupumuzika kwenye ranch zake na mahoteli yaliyoenea nchi nzima, huku akiwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulipa kisasi na kuacha majeraha makubwa ndani ya Chadema na siasa za upinzani kwa ujumla.

  Hongera Lowassa, Hatimaye sasa utapumzika kwa amani Bila bugudha, huku siasa za upinzani hasa Chadema zikiendelea kukupigia magoti kwa maumivu makali ya kutoaminika tena kwa wananchi hasa wapenda mabadiliko ya ukweli.!
   
 2. miss chagga

  miss chagga JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2015
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 57,718
  Likes Received: 30,981
  Trophy Points: 280
  mmsalalimie dr
   
 3. SUPER PREDATOR

  SUPER PREDATOR JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2015
  Joined: Apr 29, 2014
  Messages: 2,091
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Umetumwa wewe si bure.
   
 4. W

  Wope Member

  #4
  Oct 1, 2015
  Joined: May 18, 2015
  Messages: 51
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Eddo anakunyima usingiz mtoa post
   
 5. M

  Master plan JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2015
  Joined: Dec 24, 2012
  Messages: 2,965
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  Malizia kwanza ile hadithi yetu. Kumbe kuandika gazeti unamudu lakini kule umechemka! Au umegundua wasomaji wote ni ukawa??
   
 6. d

  droidwallmail JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2015
  Joined: Aug 24, 2015
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  IMG_20150513_192204 copy.jpg
   
 7. m

  makundubhyali JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2015
  Joined: May 26, 2013
  Messages: 2,211
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mleta mada kwa hii hasira na presha uliyonayo usipoangalia kutembea na dawa zako utapoteza maisha.
   
 8. TEK

  TEK Senior Member

  #8
  Oct 1, 2015
  Joined: Jul 13, 2015
  Messages: 181
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Cool tu tatizo ni nini?
   
 9. youngsharo

  youngsharo JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2015
  Joined: Jan 8, 2015
  Messages: 2,483
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Lowassa Atawapasua vichwa magamba.
   
 10. a

  aiai654 JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2015
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,861
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Hujui ulichoandika eti baada ya kukatwa dodoma lowassa alikata tamaa. Kama ni mfuatiliaji wa siasa kwenye magazeti na humu jamvini mkakati wa lowassa kujiunga upinzani endapo angekatwa ulianza toka nyuma ya 2014. Inaelekea umemjua kwenye kutangaza nia ccm
   
 11. 1000GB

  1000GB JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2015
  Joined: Oct 21, 2013
  Messages: 530
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 60
  Naona unatamani kuibadilisha bahari kua nchi kavu.. Kitu ambacho sio chakufikirika kirahic.. Aliekutuma mwambie watanzania wajana sio wa Leo
   
 12. MUSSA ALLAN

  MUSSA ALLAN JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2015
  Joined: Oct 13, 2013
  Messages: 18,960
  Likes Received: 7,722
  Trophy Points: 280
  CCM sina hamu nao..!
  Waondoke kwa Amani tu!
   
 13. KING MAZENGO

  KING MAZENGO JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2015
  Joined: Aug 5, 2015
  Messages: 755
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mama salma toroka uje babu seya soon atakuwa mtaani..
   
 14. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2015
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 12,357
  Likes Received: 8,787
  Trophy Points: 280
  Na sasa hivi atakuwa MKUU WA NCHI....

  Asante kwa mada yako ndefu, tuma salamu!
   
 15. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2015
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Unagani sana, ATAPUMZIKA IKULU rekebisha maeneo hayo
   
 16. GENTAMYCINE

  GENTAMYCINE JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2015
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 26,445
  Likes Received: 29,862
  Trophy Points: 280
  Itapendeza Sana Kwa Moyo Huu Huu Ukituwekea Na Picha Mgombea Wako AKITOA HAJA KUBWA ( AKIUKWEKA ) Ili Watanzania Pia Waweze Kujua Udhaifu Wake Na Yeye Pia. au Huna Picha Ya Tukio Hilo La Aibu TUKUWEKEE?
   
 17. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2015
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,261
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Nani alitegemea Slaa atakuwa mpinga mageuzi.
   
 18. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2015
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 19,253
  Likes Received: 12,234
  Trophy Points: 280
  Sio hasira ndio ukweli, Lowassa yupo Chadema kulipa kisasi.!
  Na kisasi kimetimia.
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2015
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 19,253
  Likes Received: 12,234
  Trophy Points: 280
  Na nani mkuu huo ndio ukweli, na Lowassa kafanikiwa sana kwa hilo, sasa hivi wapinzani wote wanamsujudu yeye.!
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2015
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 19,253
  Likes Received: 12,234
  Trophy Points: 280
  Ndoto ni ile ya usiku ila ya Mchana ni maruweruwe, vumilia kamanda Lowassa alikuja Chadema kwa kazi maalum na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...