Nadhani hii itakaa vizuri japo kuna sehemu sehemu sijazingatia kanuni za ushairi mtanisameh.....ila magulumangu nimehakikisha vina na mizani imekaa sawa hahahaha.................
AfroDenzi, nakuzimia tangu MWANZONI,
Fikra zake ni huru, pia zina burudani,
Nami ninamshukuru, hachoki tangu zamani,
Yupo dadetu Festiledi, yeye hupenda MAISHA,
Kamwe hawezi kusita, mazuri kutuonesha,
Thanks tele azipata, maana huelimisha,
Michelle yupo, hutaka TUJIELEWE,
Daima aandikapo, vichwa vyetu tusuguwe,
Sifa zake zipo, muhimu apewe,
Mzee Mwanakijiji, MZEE WA CHANGAMOTO,
Haishi kutuambia, mambo yalo motomoto,
Habari hutupatia, yenye midundo mizito,
Kaiza kaka yetu sote, jitu liloshiba,
Mengi hutaka tuyapate, yale yaliyoshiba,
Asichoke asisite, ajaze hata kibaba,
Rose naye ni rafiki, hutumia DARUBINI,
Kazi yake haichoki, popote ulimwenguni,
Kwenye siasa na urafiki, hutujuza kulikoni,
Mwanajamvi Aspirin, hutuonesha MWANGAZA,
Makala zenye hekima, na mambo kuyachunguza,
Kwa ushairi ni vema, post zake zapendeza,
Miss Judith huyo, ana UPANDE MWINGINE,
Yale ayaandikayo, hupendwa nao wengine,
Kwa mawazo si mchoyo, hufanya tushikamane,
MwanajamiiOne pia, hutuambia AMKENI,
Hachoki kutuletea, yatokeayo nchini,
Daima hukumbushia, tutoke usingizini,
October mwenzetu, utujuzaye maisha,
Wewe ni darasa kwetu, maarifa yaso kwisha,
Wafunza juu ya utu, mengi watuelimisha,
Nilham usiyechoka, asubuhi na jioni,
Nyumbani kuwajibika, halafu pia kazini,
Kisha huachi andika, kutujuza kulikoni,
Mwenzetu ni mwanaharakati, daima usiyechoka,
Wautumia wakati, pasipo yoyote shaka,
Maisha kuwa na chati, daraja la uhakika,
Inkoskaz Upo kwenye mapambano, ujenzi walo taifa,
Hujalala kama pono, wastahili nyingi sifa,
Washika yetu mikono, ili tuzizibe nyufa,
Kiraka mwendo ukaze, usiache harakati,
Mawazo uyaeleze, tena kwa kila wakati,
Ili nasi tujifunze, nawe uwe katikati,
Voiceofreason, mapenzi umeandika,
tangu siku za zamani,
Yale yaliyokufika, na yale ya majirani,
Na kwako alozimika,umesema ya moyoni,
Ndugu yetu Preta, kabobea kwa MAVAZI,
Vitu vyake ni vizuri, hilo mbona lipo wazi,
Yupo kwenye mstari, hachoki kufanya kazi,
Fidel80 nayakumbuka, manenoyo jamvini,
Hakika niliridhika, nami nikakuamini,
Kwako hayakufichika, hata yale ya moyoni,
Hashima siku hizi hakuna labda zamani
Invisible tunamjua, mkuu wetu KIJIWENI,
Sheria apambanua, ili asitupige ban,
Sote tukajitambua, tujijue kina nani,
Mkuu Klorokwini, posti zake ni KITAMU,
Hatosahau daima, kutupa yote muhimu,
Ujuzi wake kisima, haisaliti elimu,
Mkuu Kashaijabutenge,nakuheshim zamani na sasa,
Yeye wala hajalala, mengi ameshayaasa,
Kabobea mijadala, ya jamii na siasa,
Magulumangu mshairi, USHAIRI MAMBOLEO,
Mashairiye mazuri, tena yale ya kileo,
Huukuza ushairi, na kuupa mwelekeo,
Na Wiselady, siachi kumsifia,
Elimu kutugawia, na picha kutuwekea,
Mazuri hutuambia, ndani ya hii dunia,
Ndugu yangu Rutashunyuma, sitokuwacha nyuma
Posti zako nii ghali sio kama uji
Zinawakuna wa mbali mbaka Tabora na Ujiji
Mjomba Bujibuji, mwingi wa burudani
Posti zako adhimu, zinatupa burudani
Sina wakufanisha hata na mmoja humu ndani.
Nakumiss mzee wa malivdavi ulie kaburini
Baada ya posti mbili wadau wakakupa bani
Kifo chako historia ndo mana nakutilia ubani
Nami MWAJAMVI MIMI, Mohammed Shossi
Tungo zangu siwanyimi, nawapenda kiukweli,
Tena mara kumi kumi, tena na kwa kila hali,
Ambao sijawataja, lipo shairi jingine,
Sote tungali pamoja, kwa mema tuombeane,
Tusichoke zetu hoja, hivyo na tushikamane,