Hongera kwa Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu)

Mkiulizwa kwanini majimbo ya cdm hayana maendeleo mnasema maendeleo yanaletwa na serikali, barabara zikijengwa mnasema wamejenga wabunge wenu.
Haya basi, Sugu amejenga barabara na mnyika lini atatekeleza ahadi yake ya maji?
 
Dar es Salaam zinjengwa hayuko Sugu, Dodoma zinajengwa hayuko Sugu, Arusha .................
Ni mpango wa WB kuboresha miji mtoa uzi usidanganyike. Pia lazima ujenzi uwemo kwenye bajeti ya mwaka wafedha na sio vinginevyo. Sugu anatetea haki za wasanii.

wewe acha zako hata WB wanatoa fedha mbona hua zinaliwa tu? na hakuna cha maana kinacho endelea? kama hakuna mbunge anayefuatilia na kuibana serikali hakuna jambo la maana linaloweza kufanikiwa...
 
Niko mikononi mwa polisi maisha kwangu bado ni mikosi afandeee!
 
Sisi hatuhitaji vyeti hapa ni utekelezaji tuu. CCM mbona kuna vyeti kibao lakini utafikiri walikuwa wanasomea wizi.
 
Dar es Salaam zinjengwa hayuko Sugu, Dodoma zinajengwa hayuko Sugu, Arusha .................
Ni mpango wa WB kuboresha miji mtoa uzi usidanganyike. Pia lazima ujenzi uwemo kwenye bajeti ya mwaka wafedha na sio vinginevyo. Sugu anatetea haki za wasanii.

haya bana;na meli ziwa vikitoria,kigoma kuwa dubai lini?
 
Sugu alituahidi atadeal na suala la barabara na sasa takribani barabara saba hapa jjn mbeya ziko katika matengeneneza katika kiwango cha rami. Mpesya(mbunge wa zamani wa ccm) ilikuwa ni kitendawili kwake.

thats WOW!
 
Naanza kutafakari mara mbili niliambiwa miongoni mwa wabunge wa CDM walio na hali ngumu kurudi jimboni huyu ni mmoja wapo ila kwa haya ngoja nitafakari tena
 
Naanza kutafakari mara mbili niliambiwa miongoni mwa wabunge wa CDM walio na hali ngumu kurudi jimboni huyu ni mmoja wapo ila kwa haya ngoja nitafakari tena

mkuu sema tu cm yangu haiaplodi ningeupload ujione watu walivyo busy
 
Sugu mjanja sana. Kawaambia vinega wafanye matamasha pesa zinazopatikana zipelekwe kuwanunulia chakula wakazi wa jimbo lake. Very creative...

mzee unaota nini? au umekurupuka kutoka usingizini? Mbeya hakuna shida ya chakula,na kama ikitokea mbeya kuna shida ya chakula basi sehemu zingine za Tanzania mtakuwa mmeanza kufa njaa. Mbeya is the leading producer of food crops in EAST AFRICA.
 
Dar es Salaam zinjengwa hayuko Sugu, Dodoma zinajengwa hayuko Sugu, Arusha .................
Ni mpango wa WB kuboresha miji mtoa uzi usidanganyike. Pia lazima ujenzi uwemo kwenye bajeti ya mwaka wafedha na sio vinginevyo. Sugu anatetea haki za wasanii.
Kuwa makini unapozungumza, Hata kama mpango ungetoka mbinguni kama wasimamiaji ni wazembe hakuna kitachofanyika. Mbeya ni zaidi ya miaka kumi hakuna hata kilometa moja ya barabara ya lami iliyojengwa, zaidi hata zile zilizokuwepo pia hali yake ni taabani. Kwa wale waliopo Mbeya watakubaliana na mimi barabara nyingi za mbeya zilivyodhoofu kipindi chote cha miaka 10 mheshimiwa yule alipokuwa mbunge. Mpesya alikuwa anayaona hayo? Lakini muheshimiwa kaingia tunaona mambo yanaenda vizuri kwa ufuatiliaji wake na wanambeya.
 
Unapaswa kutoa data kuwa Mwaka ...... zilitoka fedha kiasi ...... zikaliwa na ........
Hapo nitakuelewa.
Nitatoa mfano chuo kikuu UDOM wazo lilianza na Mkapa na michoro iliandaliwa kazi ika take over 2007 na anayesifiwa kukijenga ni Raisi Kikwete. Ukweli ni kuwa huwezi kusimamia kama hakuna mpango.
Pili wananchi wa Mbeya wameonyesha bayana kuichukia CCM hivyo CCM inajaribu kuwabembeleza kama vile kuwahonga ili warudishe mapenzi yao lakini sio kama dhana walioyonayo watu wengi kuwa sababu ya Mbunge. Mpesya ni kweli alikuwa hana hoja yenye mshiko, lakini sio sababu ya kutufanya tupofuke macho. Tukalitia maji tembo
 
Ugonile ndaga. Utwa mbombo? Mkasaniege fijo amendeleo gafike mpaka Kwisyeye. Lakini mshirikiane, mtu mmoja peke yake hawezi kuleta maendeleo.
 
Nitaandika kama ninavyofikiri mimi tofauti na unavyofikiri wewe. Niataandika kwa staha kadri ya malezi yangu, nakuomba na wewe uandike kwa mtazamo wako unavyofikiri. Lakini ufahamu JF inahitaji hoja za watu makini kwa hoja sio kwa matusi. Ingalikuwa JF ni uwanja wa matusi watu makini wasingechangia. Ninaiheshimu JF ila wewe binafsi nakuvumilia. Inaelekea mawazo yako haya ni ya hasira na hasira kwa muujibu wa vitabu vitakatifu hukaa kifuani pa wapumbavu
 

Mazee mbona hili liko clear unapataje shida kulielewa?
Hao waathirika wa mafuriko walikuwa na chakula chao wenyewe, mafuriko yakaja yakachukua kila kitu kuanzia makazi yao na vyakula vyao kwahiyo mbunge wao kuwasaidia chakula lilikuwa ni jambo la kawaida kama ambavyo tumewachangia vyakula waathirika wa mafuriko dsm mwezi december mwaka jana, ambao sasahivi wamehamishiwa mabwepande.

Kama kusingetokea mafuriko ni dhahiri kwamba wananchi hao wasingehitaji msaada wa chakula, na sikumbuki ni lini wananchi wa mkoa wa mbeya walipata msaada wa chakula kwakuwa tu wameshindwa kuzalisha chakula kwa sababu iwayo yoyote.
 
Back
Top Bottom