Hongera kwa Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu)

Sasa mshaurini angalau asafishe cheti chake cha Form 4 basi. Kuwa na mbunge aliyepata pointi 33 nayo si kitu kizuri kwa kweli. Kama mnampenda kweli basi jaribuni kumpa ushauri kwa hili.
 
Sugu mjanja sana. Kawaambia vinega wafanye matamasha pesa zinazopatikana zipelekwe kuwanunulia chakula wakazi wa jimbo lake. Very creative...
 
Sugu alituahidi atadeal na suala la barabara na sasa takribani barabara saba hapa jjn mbeya ziko katika matengeneneza katika kiwango cha rami. Mpesya(mbunge wa zamani wa ccm) ilikuwa ni kitendawili kwake.

Nyinyi mko very interesting!!! Umeme ukikatika mnamlaumu Kikwete, barabara zikijengwa mnampongeza Sugu...
 
Sasa mshaurini angalau asafishe cheti chake cha Form 4 basi. Kuwa na mbunge aliyepata pointi 33 nayo si kitu kizuri kwa kweli. Kama mnampenda kweli basi jaribuni kumpa ushauri kwa hili.

Sasa kuwa na kiongozi dr ambaye hafanyi lolote bungeni kuna manufaa gani?
 
Usifikiri watu hawana kumbukumbu. Asilimia 33 ya gross income ya tamasha la Mbeya imeenda jimboni kwa Sugu. Tamasha lipi lililofanyika bure?

matamasha mawili yamefanyika pale uwanja wa dr. Slaa (zamani CCM). Album za Anti virus Mixed tape ni buuuureee!
Hata hivyo, mbeya hatuna shida ya chakula! Na kwa iyo unakubali kuwa Sugu ni zaidi ya mbunge wa Mbeya sio?
 
Dar es Salaam zinjengwa hayuko Sugu, Dodoma zinajengwa hayuko Sugu, Arusha .................
Ni mpango wa WB kuboresha miji mtoa uzi usidanganyike. Pia lazima ujenzi uwemo kwenye bajeti ya mwaka wafedha na sio vinginevyo. Sugu anatetea haki za wasanii.

Kwani huko nyuma zilikuwa hazitoki fedha kutoka kwa wafandili???? Kama Arusha ndio usiseme. Lakini sasa naona upinzani umepamba moto angalao wanajitahidi kujenga barabara.....tutafika tuuu.....
 
Aliahidi kuboresha michezo,juzi baada ya miaka mitatu,wanambeya wameiona Yanga!SUGU,MDOGO MDOGO TUTAFIKA!
 
Kwa barabara za ndani mara nyingi zinakuwa zipo chini ya manispaa hapo kuna kuwa na budget yake kwenye halmshauri chini ya mkurugenzi ambapo fedha hizo uidhinishwa kupitia vikao vya baraza la madiwani na mwenyekiti wa halmashauri kwahiyo mbunge makini lazima atafuatilia ilo kwa kuwa karibu na mkurugenzi ili kutengeneza hizo barabara
 
Dar es Salaam zinjengwa hayuko Sugu, Dodoma zinajengwa hayuko Sugu, Arusha .................
Ni mpango wa WB kuboresha miji mtoa uzi usidanganyike. Pia lazima ujenzi uwemo kwenye bajeti ya mwaka wafedha na sio vinginevyo. Sugu anatetea haki za wasanii.

kwa miaka yote hiyo mipango ya WB haikuwepo?
 
Back
Top Bottom