Uko sahihi mno. Itikadi ya Mtu ni kama spiritual beliefs. Hailazimishwi kwa kusikia redioni.Hivi hawa viingozi wetu hawaoni aibu kulazimisha mapenzi ya mtu kwa chama fulani au kwa mgombea?
Hata wakizuia habari zinazomhusu Lissu zisitangazwe au kuandukwa gazetini, bado wenye mapenzi na Chadema ama Lissu wataendelea kumuunga mkono. Wakae wakilijua hill.
Tangu Lissu afike ni gazeti pekee lililojitahidi kumuandika front page mara kadhaa hata alipokuwa Ubelgiji walikuwa wanamuhoji nafikiri watawala hawafurahia habari hii.Wanachokitafuta watakipata lakini historia itawakumbuka
Hujamsikia IGP? Inaonekana wasio julikana ni Lissu maana polisi wana mtafuta. Watampata akisha pitishwa kugombea Urais maana atakuwa na ulinzi wa polisi.Huenda wameanza kugundua hatari ya kumlamba miguu Bwana yule.
Hata hivyo,huenda gazeti likaadhibiwa kwa kuandika habari hii bila ku-balance story kwa kuwahoji watu wasiojulikana!