Hongera kwa ATCL kwa Kuanzisha Route Mpya za Nje Ya Nchi

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
1,278
1,553
Shirika la ndege la ATC naona limeanza safari za nje. Hii ni hatua nzuri sana lakini wasiwasi wangu ninasita kuamini kwamba wataweza kumudu route za kimataifa.

Moja ya changamoto za route za kimataifa hazihitaji kuahirisha safari wala kuchelewesha. Hiyo inaweza kupelekea kukumbana na penalty kwa baadhi ya abiria makini.
Pili wakianza vibaya wanaweza kupoteza soko kabisa.

Ushauri wangu watoe ajira kwa afisa masoko mwenye uzoefu kwenye mashirika makubwa.
Watoe ajira kwa marubani wenye uzoefu na route ndefu. Ndege za safari ndefu hubeba wastani wa rubani 4 hadi 6 Hii inasaidia kuepusha kuahirisha safari. Hivyo hawa wa kwetu wanaweza kufanya nao ili kujenga uzoefu.

Lakini jambo moja na muhimu ni kuingia mkataba wa kubadilishana abiria pindi inapotokea abiria hawatoshi au kuna dharura.

Jambo lingine wanahitaji kufanya logistics business wasafiri wanaotoka India na China kuja Tanzania ni wachache kuliko wanaotoka Tanzania kwenda nchi hizo.
Hivyo wanatakiwa kufungua vituo vya kuuza ticket Zambia Congo na Kenya ili wawe na ndege ndogo kama bombardier ili wakitoka india na China wakiwafikisha Dar waunganishwe kwenda kwenye nchi zao. Ndiyo maana hata mahusiano mazuri na fast jet yangeifaa sana Air Tanzania. Ukikutana na campuni yenye ufanisi na mikakati ya kibiashara inayokuzidi usifanye hila tafuta ushirikiano.

Biashara ya ndege kwa maana ya soko kwa sasa itawawia vigumu Air Tanzania kufanikisha soko la kimataifa kwa stail hii kama hawatajenga mahusiano mazuri na air line zingine.
Kwasababu soko la ndani lenyewe bado hawajakidhi.

Hivyo kwakuwa lengo ni kusaidia kuingiza wageni ndani, lazima wawe tayari kushirikiana.
 
Ni kazi bure kama hatutawapeleka wachawi wa Gamboshi wakatalii huko ughaibuni, vinginevyo mandege yote yatageuzwa kuwa mabanda ya kuku.
 
Jamani kama mnalolijua semeni moja kwa moja sio kujifanya nice guys. Au wale jamaa wa gambosh waingilie kati kutatua tatizo.

Kumbuka pia serikali ndio mnunuzi mkuu kama akizuia safari jua mukichwa hatumiki vizuri dunia ni duara. Kama mnaua biashara, mnazuia watu wasisafiri then mtasuasua tu.
 
ATCL hawawezi kufanikiwa sababu shirika linaendeshwa kisiasa zaidi
 
Back
Top Bottom