Uzuri Tanzania mwizi anaonekana mjanja badala ya mhalifu,utasikia''jamaa kapiga dili customs kalipa ushuru mdogo'' bila kujua madhara yake....sasa Rais nae kaiba kura watu wanampongeza
Safari_ni_Safari
Naomba uwache TUHUMA zisizo Kichwa wala miguu.
Nec ni CHOMBO MAKINI chini ya uongozi adilifu wa Jaji Mstaafu Lewis Makame.
Kitendo cha kuzua kuwa Rais ameiba kura ni kusema kuwa alishirikiana na NEC, taasisi yenye utashi na uadilifu mkubwa.
Aidha ni kusema kuwa Election Observers wa Ndani na Nje ni wazandiki. Mie ninachoona ni tabia ya kutokubali MATOKEO; na nawaasa kuwa na MOYO wa kukubali matokeo.
Dkt WPS amejitahidi, amepata 3.5 times ya Lipumba; na 22 Seats; that is REMARKABLE.
Sasa tuangalie yaliyo mbele yetu.
wewe ni makame lewis wa tume au huyo ni baba yako? Lazima usheherekee kwa fungu alilochukua. Ndiyo maan hata mbwa akishiba huwa mkali kumlinda bwana wake kama alivyokuwa mbwa NEC kumlinda bwana wake JiKE (JK).
Kusema NEC ni chombo kiadilifu hayo ni mawazo yako, lakini matendo yake wakati wa kuhesabu kura hasa za raisi imeonyesha kinyume cha hapo. Kurudia rudia maneno ambayo siyo sahihi kila mara ili baada ya muda watu waamini ni kweli ni mbinu ambayo inatumiwa na spin doctors kuvuruga ukweli. Nina imani kuwa wapo wengi kama mimi ambao wana mashaka na uadilifu wa nec. Hoja kama yangu zimeshatolewa na vyombo mbalimbali ambavyo vilikuwa vinafuatilia uchaguzi.Safari_ni_Safari
Naomba uwache TUHUMA zisizo Kichwa wala miguu.
Nec ni CHOMBO MAKINI chini ya uongozi adilifu wa Jaji Mstaafu Lewis Makame.
Kitendo cha kuzua kuwa Rais ameiba kura ni kusema kuwa alishirikiana na NEC, taasisi yenye utashi na uadilifu mkubwa.
Aidha ni kusema kuwa Election Observers wa Ndani na Nje ni wazandiki. Mie ninachoona ni tabia ya kutokubali MATOKEO; na nawaasa kuwa na MOYO wa kukubali matokeo.
Dkt WPS amejitahidi, amepata 3.5 times ya Lipumba; na 22 Seats; that is REMARKABLE.
Sasa tuangalie yaliyo mbele yetu.
bwana makame rais kishatangazwa na leo anaapishwa, kwa maana hiyo hakuna budi kuachana na marumbano tena na kuangalia yajayo, NACHOKUOMBA BWANA MAKAME mwambie mheshimiwa huku uswahilini kwetu hali ni ngumu kwelkwel maisha magumu kupindukia vilevile bwana makame mkumbushe rais afanye kama alivyokuwa akifanya mwaka wa mwanzo wa urais wake kutembelea masoko ya uswahilini kama tandale na kwingineko labda itasaidia kujua hali zetu.. yawezekana hajui hii hali kwan wote mnaomzunguka hamu-ishi uswaz wala hamuendi magengeni nyie masupamarkiti tu kutokana na kipato chenu, si anawalipa vizuri kwa kuongopa kwamba watanzania wapo shwaaaari mkuu.
KWANINI NASEMA NEC NI TAASISI ADILIFU?
1. Kiongozi wake ni Jaji Mstaafu Lewis Makame. Ni mtu safi, hana upendeleo na amejaaliwa maadili ya hali ya juu kabisa.
2. Observers wa ndani na Nje wametoa ripoti zinazoipa sifa stahiki NEC. Hawajasema hata mara moja kuwa NEC ni wezi wa KURA. Spin Doctors ndio wamefanikiwa kuiteka Jamii hii kwa kuwafanya waamini kuwa NEC, CCM, na wasimamizi wa Uchaguzi ni Wachakachuaji.
3. Wagombea wengi, wakiwemo wale wa Urais wamekubali matokeo na kueleza kuwa uchaguzi ulikuwa HURU na HAKI.
NEC ina miongozo, sheria na taratibu za Uchaguzi; na hiyo inafuatwa kwa NUKTA.
NEC imekuwa ikikiri mapungufu yaliyojitokeza, na kuyafanyia kazi, UTENDAJI wa NEC umekuwa ukiboreka chaguzi hadi chaguzi.
NEC ina watumishi waliokula kiapo kutumikia Tume kwa uadilifu mkubwa na kulinda maslahi ya taifa.
Wacha niishie hapa.
Wadau, NEC ni chombo chetu; hakuna haja ya kuinyooshea vidole vya kuisuta kwa sababu TULIYEMTAKA sisi hakufanikiwa kupata kura za kutosha.
Hongera kwa utaalamu wa kuchakachua kura!!!
wewe ni makame lewis wa tume au huyo ni baba yako? Lazima usheherekee kwa fungu alilochukua. Ndiyo maan hata mbwa akishiba huwa mkali kumlinda bwana wake kama alivyokuwa mbwa NEC kumlinda bwana wake JiKE (JK).
Mimi nawasilisha hoja OBJECTIVELY, nafahamu kuwa katika ukumbi huu ili mtu aonekane wa maana atukane NEC au Chochote kinachohusu Serikali au CCM. Mie nadhani ipo haja ya kuwasilisha hoja iwapo (a) inaongeza thamani, (b) iko objective na (c) sio matusi.
Kumbukeni kuwa kuna watu mbalimbali wana access na hii website na wanaona yaliyomo. Wasiwasi wangu ni madogo wanaokuwa; wanaona Watanzania wenye dhamana zao wana mtazamo RIGID na wanaporomosha matusi. Sasa JK amekuwa JiKE na ni Mume wa Jaji? Wadau, inalipa zaidi kukaa kimya kuliko kuongea pumba.
Hahahaha
Mzee Mimi ni MTZ wa Usweken, wala huyo Rais hanijui.
Michango yangu ililenga kuonyesha taswira nyengine ya mijadala