Hongera Kikwete kwa hili la Kigamboni

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
5,271
5,366
Hakika wana kigamboni na viunga vyake watakukumbuka daima,leo nimesema nifanye ziara fupi ya kushtukiza nilichokiona nimefurahi na kufarijika sana na kwa mwendo huu TZ yangu naiona inapaa,itakua si busara kuacha kukupongeza mh wetu pamoja na yote tunayoyasikia lakini ulikua na nia ya dhati ya kuwasaidia watanzania,hongera sana kwa niaba ya wapenda maendeleo.
 
Hongera mkuu ulie maliza muda wako, kwakweli hongera maana umetusahaulisha hata majiraha na machungu uliyo tuachia kwa hili daraja, hata kama machungu hayalipiki ila asant kwa hili daraja.
 
Hongera JK huku Msimamiz Mkuu Dr Dau mnamtukana...wanadam viumbe wa ajabu sana
Nime attach hapa Picha nne za Daraja La Dr Dau Kigamboni, ama kweli limebadilisha sura ya Dar.

1460839968056.jpg
1460839975085.jpg
1460839980385.jpg
1460839984745.jpg
 
hiyo ni kazi yake kama rais sidhani kama anahitaji pongezi,Ila zile deal alizopiga na mwendo wa uongozi wake ulivyokuwa lazima nimponde.
 
Yaani kama UDOM,ilivyo but Dau haonekani na jema hata! Hizi chuki hizi aliyezianzisha Mungu atamlipa anachostahili!
Siku zote pongezi hutolewa mtu anapofanya vizuri kwenye wajibu wake, ukiitunza vizuri familia yako utapongezwa, mtu huyo huyo akiacha familia yake Na kuhudumia familia nyingine ambayo sio wajibu wake atalaumiwa na jamii. Watu hupongezwa makazini mwao kufanya kazi viizuri, ingawa wajibu wao na wanalipwa kwa kazi hiyo. Sababu wakupongezana Ni sababu kila anahusika alitaliwa apafikie ulipofikia, lakini wengine hawakupafikia. Aidha kwa Bahati mbaya, uzembe, mfano mtu ananunua gari, akijenga nyumba hupongezwa ingawa Ni wajibu wake maana vinansaidia yeye. Na hakuna utakae kupongeza eti uache kwenda kazini kwako alafu uende ukafanye kazi sizokuhusu Ili upongezwe.
 
Namimi iko siku ntakuwa mkuu katika nchii hii, piga dili mwanzo mwisho ukikaribia kutema funguo za white house unamalizia na barabara ya kilomita 5, tuone wasikuabudu kwa kukushukuru na kukisahau kile ulicho watendea.
Hata nyerere hakua msafi 100%nae alikua na madhaifu yake,sio yeye tu wote waliofuatia nao wanamapungufu yao,hata mwenyekiti wenu nae anamapungufu yake ya kiuongozi,acha chuki.
 
hiyo ni kazi yake kama rais sidhani kama anahitaji pongezi,Ila zile deal alizopiga na mwendo wa uongozi wake ulivyokuwa lazima nimponde.
Hujui maana ya neno pongezi,jukumu la mshambuliaji uwanjani ni kufunga goal akifunga kwanini tunamshangilia kwa pongezi za hali ya juu?
 
Back
Top Bottom