Hongera Jerry Muro. Sasa tuambie hili!

Hongera Jerry Muro. Sasa tuambie hili!

Mshkaji wangu mmoja Aruasha anapatikana maeneo ya chini ya mti idara ya majianamiliki pingu na bastola kihalali kabisa,JAMANI PINGU INAUZWA KWA MTU YEYOTE YULE TENA KWA BEI BURE KABISA,NAFIKIRI WATANZANIA UOGA UMEKUA NI SEHEMU YA MAISHA YETU MPAKA PINGU TUNAONA NIKITU CHA HATARI SANA,HATA KATIBA YA NCHI NAI UOGA NDIO ULIOFANYA TUSIIJUE NA HATA KUIONA KWANI TULIKUA TUNAIONA KAMA NI NYARAKA ZA SERIKALI KUMBE NI HAKI YA KILA MTU KUIJUAA NA KUIMILIKI HIYO KATIBA.PINGU JAMANI INAUZWA KWA YEYOTE BILA MASHARTI WALA BARAKA KUTOKA KWENYE SERKALI YA MTAA.
 
Kama alinunua, na alituonyesha risiti sasa tumlaumu nani hapo, muuzaji au mnunuaji? Binafsi nilishawahi kuona raia wa kawaida anamiliki pingu, alikuwa akimfunga ndugu yake ambaye ni mgonjwa wa akili. Kwa Jerry siwezi jua alikuwa anaitumiaje, lakini kumiliki siwezi shangaa!
 
hongera Muro,kwa kazi nzuri pambana afu kwa hali uliyoiona nadhan unapata mwelekeo mzur juu ya sheria za nchi yako kama niya kidhalimu sijajua,kama kuna hali fulani umeiona ambayo hukupenda andika waraka popote pale afu tutauchambua na kujaribu kuproject hitma yake...
 
Si bure Umetumwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwanza nikupongeze Jerry Muro kwa kushinda kesi yako dhidi ya Jamhuri, na baadae kujipatia tuzo ya ubora wa kazi zako na kile kilichoitwa ujasiri wako katika kufichua maovu yaliyopo ndani ya jamii.

Sasa baada ya habari hizi njema, ni wakati muafaka sasa kuueleza umma wa watanzania matumizi ya zile pingu ulizokiri kuzimiliki na hata kutuonyesha stakabadhi ya manunuzi ya pingu hizo. Tunakuomba ufanye hivyo kwa sababu wewe Jerry Muro sasa umeingia kwenye rekodi za dunia kama mwandishi pekee wa habari duniani mwenye kumiliki kifaa ambacho ni vyombo vya ulinzi na usalama pekee ndiyo wana mamlaka ya kumiliki na matumizi. Au unataka kutuambia kwamba kazi zako za uandishi zinahitaji kujihami na wakati mwingine ku-effect arresting powers za wahalifu mbalimbali? Je, mamlaka hii umeipata wapi wakati hata Polisi waliostahili kukukasimu wamekukana na kukuchukulia hatua?

Bila majibu fasaha, sitashangaa siku nyingine nikisikia unamiliki mahakama (lakini siyo hii iliyokuachia huru katika mazingira ya utata) na hata magereza na vituo vyako vya polisi.

Muro please, come out clean!
 
Mimi nadhani kumiliki pingu sio kosa la sivyo zingekuwa haziuzwi kwenye maduka ya siraha,je mliwai kuona maduka ya siraha hapa tz yanauza smg? Kwmawazo yangu Pingu ni kama kamba ya kumfungisa mhalifu ila hii ni kamba ya kisasa je, kumilikim kamba nikosa?
 
Jerry Muro si investigative journalist wa kwanza nchini na duniani lakini hatujawahi kusikia hiki kituko popote pale. Kuwa investigative journalist si kuwa na vitu ambavyo katika hali ya kawaida watu hawatakiwi kuwa navyo. In this case bwana huyu alikuwa tayari ame-solicit rushwa akijiita ni mwanausalama. Tuwekewe bayana hili siyo kuishi kwa "ifs".
"Aulizaye ataka kujuaatii"

Hivi kama haruhusiwi kumiliki pingu,kwanini aliuziwa? Pili kama mwanajamvi mwingine alivyouliza,kipi na hatari kati ya pingu na Bastola?
Napata picha ya kuwa kunawatu walipania huyu bwana afungwe kwa sababu aliwamulika,lakini pia labda kuna kitu wanakijua hawataki kukisema,wakiweke hadharani.
Mi binafsi nilihisi Jerry Muro kkushinda hii kesi pale wale aliotuhumiwa nao waliposema mahakamani kuwa polisi walipa pesa iliwamuingize mkenge Muro,na namna polisi walivyoshindwa kumkamata Muro akipokea ile pesa.
 
Nina swali. Muro huyu ataendeleza ujasusi wake kwa faida ya jamii au tukate tamaa? Mchango wake kuanika maovu ndani ya jamii haukuwa bila ya matatizo wala vishawishi.
Hili la pingu anawajibika kulitolea maelezo yanayosadikika ili abaki credible mbele ya jamii.
La bastola sina wasiwasi nalo lakini alitolee maelezo kwa ajili ya kuiondoa shaka jamii ambayo ilimkubali na kumuaini.
 
basi kama wewe unajua anatumia si utuambie?watu wanatoa majibu wewe unang'ang'ania kuuliza.Kama wewe ni polisi na deals zenu mnafanya pamja weka hadharani.lakini mimi sioniissue hapa kwasababu Kova aliyemkamata alitakiwa atueleze kama anazifanyia kitu mbaya.
 
Usitulazimishe kuamini unachokiamini, acha chuki binafsi. Huna jeuri ya kubatilisha maamuzi ya mahakama.
 
Kwani Pingu si kamba ya chuma tu iliyo na ufunguo. Kwani pingu na kufuli ya baiskeli tofauti yake nini? manake zinaweza kuwa na kazi ile ile. Hata mimi ninayo pingu na huwa nafungia baiskeli yangu. Ni mawazo finyu kuwa pingu inamilikiwa na askari. Ila huyo aliyeanzisha hii thread anaona ni sawa kumiliki silaha ya moto. Nimwambie tu haya ni mazoea kwamba watu wanamiliki silaha za moto kama bastola na n.k. na kwamba kwa kuwa pingu imezoeleka kushikwa na askari yeye linampa tabu kidogo. Lakini ukweli ni kuwa, PINGU NI KAMBA YA CHUMA ILIYO NA UFUNGUO KAMA KUFULI YA BAISKELI
 
Kumbe bado kuna watu wajinga humu?mnapohoji mtu kumiliki pingu ni kwa nini msihoji kwa nini zinauzwa?kama ni kosa kumiliki ni kwa nini serikali haizuwii uuzwaji?maswali machache tu hayo yanatosha sana kutafakari na kupata majibu,siku zote ukitaka kumchimba mtu anzia chini siyo juu.
 
I stand to be corrected!Kwangu Jerry Muro bado ni mwanahabari mahili aliyeleta habari za uhakika sio zile tulizozoea kuchakachuliwa ili zikidhi matakwa ya watu fulani.Hakuna mtu asiyejua kuwa alikua anaandaliwa mkakati wa kummaliza.Waiouandaa wamechemsha.Na wanaumia kwa sababu huyu bwana katoka.sasa mie nnachosema kama wewe ni great thinker tupe issue unazozijua kuhusiana nae.Lakini vinginevyo haya ni ya mfa maji na natarajia huyu bwana atakuja na issue nyingine dhidi yenu ndio maana mnaanza kutapatapa.Sitaweza kuyaamini maneno yenu.polisi nnayoijua mimi Jerry asingeweza toka salama,angepigwa pini mpaka aeleze maovu yake yote na kwa aliyowatenda asingeweza toka vivihivi.Kwa hiyo tusipotezeane muda.Kama mna issue mwageni humu tuifanyie kazi, lakini kama hamuwezi msimchafue mtu na hayo kwangu ntayachukulia kama majungu.
"poleni sana WAHANGA wa Jerry Muro."
 
Nina swali. Muro huyu ataendeleza ujasusi wake kwa faida ya jamii au tukate tamaa? Mchango wake kuanika maovu ndani ya jamii haukuwa bila ya matatizo wala vishawishi.
Hili la pingu anawajibika kulitolea maelezo yanayosadikika ili abaki credible mbele ya jamii.
La bastola sina wasiwasi nalo lakini alitolee maelezo kwa ajili ya kuiondoa shaka jamii ambayo ilimkubali na kumuaini.

Kwani kazi ya pingu ni nini?acha kujidharirisha mbele yetu tunakuona kama juha tu.
 
Nyie askari wapelelezi na waendesha mashtaka, si mkate rufaa kuliko kuja kulalama hapa?Siku nyngine mfanye kazi zenu safi/vizuri maana mmezidi kuzembea kazi.Acheni kusumbua wananchi, hasa nyie askari wa barabarani.Kama Jerry alitoa kitu kidogo, katika nchi ya kitu kidogo na watu wake wadogo, kuna la ajabu lipi ikiwa nanyi mnavutaga kitu kidogo?Au kesi hii mliogopa kuvuta?Huwa mnashangaza sana.Kitu kidogo nyie huwa mnaongoza na hizo mahakama sasa msituletee hapa.
Well said Madam!! Wakate rufaa kama wana ushahidi wa hongo!! They are crying foul because they have been beaten at their own game!!! Shame on them!!!!!
 
mbona unaumizwa na ushindi wa jerry?yaani wewe ulipenda mwenzio awe na matatizo?kama watafuta basha nenda kwa cameron acha na jerry kwanza anamke
yaani pingu ndio imekuuma sana kuliko viongozi wanao miliki migodi ya dhahabu mali ya watanzania!
 
Kama mahakama imeamuru arudishiwe basi Ana haki ya kumiliki, suala la matumizi nyie haliwahusu, kumfunga mtu Kwa pingu Na kumpiga kwa risasi lipi baya? Jamani watu....
 
Sioni shida hata kidogo kumiliki pingu jamani, kwani sheria inasema mtu asimiliki pingu? sielewi eti na matumizi ya pingu anayajua yeye tukumbuke si kila aliye na vidonge vya ARV ameathirika yaweza kuwa anavyo kwa ajili ya kuboost kuku wa mayai eti. Hakimu kaona hana kosa na kama alinunua na rist akapewa kosa liko wapi???????
Kwanza nikupongeze Jerry Muro kwa kushinda kesi yako dhidi ya Jamhuri, na baadae kujipatia tuzo ya ubora wa kazi zako na kile kilichoitwa ujasiri wako katika kufichua maovu yaliyopo ndani ya jamii.

Sasa baada ya habari hizi njema, ni wakati muafaka sasa kuueleza umma wa watanzania matumizi ya zile pingu ulizokiri kuzimiliki na hata kutuonyesha stakabadhi ya manunuzi ya pingu hizo. Tunakuomba ufanye hivyo kwa sababu wewe Jerry Muro sasa umeingia kwenye rekodi za dunia kama mwandishi pekee wa habari duniani mwenye kumiliki kifaa ambacho ni vyombo vya ulinzi na usalama pekee ndiyo wana mamlaka ya kumiliki na matumizi. Au unataka kutuambia kwamba kazi zako za uandishi zinahitaji kujihami na wakati mwingine ku-effect arresting powers za wahalifu mbalimbali? Je, mamlaka hii umeipata wapi wakati hata Polisi waliostahili kukukasimu wamekukana na kukuchukulia hatua?

Bila majibu fasaha, sitashangaa siku nyingine nikisikia unamiliki mahakama (lakini siyo hii iliyokuachia huru katika mazingira ya utata) na hata magereza na vituo vyako vya polisi.

Muro please, come out clean!
 
kwani ni kosa kumiliki hivyo vitu yaani pingu na bastola na kama ni kosa kwanini duka la silaha pale upanga wanaviuza?
Mimi mbona namiliki pingu na bastola ni suala la kufuata taratibu tu, na unayesema mwandishi wa habari kumiliki silaha unashangaa kwa nini?mtu yeyote anaweza kumiliki silaha kama ukitimiza vigezo vinavyotakiwa
 
Back
Top Bottom