TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 31,588
- 18,741
katumia general concept ili amalizie kuandika post yake..
kumbe issue ilikua ni kumaliza post na sio kufikisha ujumbe sahihi
OK
katumia general concept ili amalizie kuandika post yake..
Siyo swali langu lakini kwa hakika hii haijawahi kusikika popote. Jamaa alikuwa akitumia pingu kutapelia halafu watu wanamchekea. Tuache kuchekelea mmomonyoko wa maadili na waandishi wanaoamini katika blackmail.
kwani ni kosa kumiliki hivyo vitu yaani pingu na bastola na kama ni kosa kwanini duka la silaha pale upanga wanaviuza?
Mate, watu hawajui kuwa pingu ni kifaa murua sana kwenye mapenzi.....mie nina pingu, lakini sijawahi kutishia mtu wala sijawahi kuchekewa na mtu yoyote na wala sijawahi kutapeli, naitumia kwenye satisfactions zangu nyumbani,
unaamini kila mwenye pingu anfanya uliyoandika?
Hahahaah...babu hapa unaua! Ushaanza uchakachuzi wa hii sredi!Mate, watu hawajui kuwa pingu ni kifaa murua sana kwenye mapenzi.....
Kwangu mie naona bastola ni hatari zaidi ya pingu. Sasa kama bastola inauzwa inakuwaje pingu zisiuzwe? Mabomu yangekuwa yanauzwa ningeogopa lakini pingu? khaa! watu wanafungana pingu wakati wanamegana kwa raha zao bana!Hahahaah...babu hapa unaua! Ushaanza uchakachuzi wa hii sredi!
Yawezekana....labda ni usalama wa taifa!
afadhali hata hayo mabomu kamanda........ utu unauzwa siku hizi, tena kwa bei ya chee!!! we angalia wanasiasa wanavyonunuliwa kwa bei ya baiskeli ya swalaKwangu mie naona bastola ni hatari zaidi ya pingu. Sasa kama bastola inauzwa inakuwaje pingu zisiuzwe? Mabomu yangekuwa yanauzwa ningeogopa lakini pingu? khaa! watu wanafungana pingu wakati wanamegana kwa raha zao bana!
Mnachoshangaa Jerry kumililiki pingu na bastola ni nini?au mleta thread hii ni mwathirika wa vipindi alivyowahi kuvirusha Jerry na vikawaumbua?tujiulize kidogo kwa makini,hizi pingu zinauzwa kisheria au si kisheria na kama ni kisheria sheria hiyo iliwekwa na Muro?na kama si kisheria kwa nini mahakama imeamua arudishiwe pingu zake?
Na kama haziuzwi kisheria hao wanaoziuza kwa nini hawachukuliwi hatua?wewe kama hupendi kumiliki pingu usioanishe dislike zako na za Muro kisha ukataka humu jamnvini ushawishi watu kujengea wasiwasi Muro.Juu ya hukumu yake ya rushwa sina cha kujadili maadam mahakama imeshatoa hukumu, lakini hoja ya pingu na bastola ni ufinyu wa fikra kulazimisha kusa wakati zinauzwa kwa kila anaehitaji ili mradi tu atimize matakwa ya kuuziwa.
Leo Muro kama anapenda kumiliki pingu ni hiari yake na mwingine anapenda kula kitimoto ni hiari yake anaependa kugonga castle bariki ruksa leo tukianza kuulizana eti tuambie unapokunywa bia ni za nini,tutakuwa tunaingilia uhuru binasfi,na Jerry kwa kuwa pingu zinauzwa kisheria na alizinunua kisheria hiyo sasa inatosha.
Na hata hivyo kama mtu anaandika habari za kiuchunguzi kwa mtazamo wangu ni mtu ambaye anatazamiwa kukutana na changamoto nyingi katika utendaji wake. Sasa kama lizinunua kwa ajili ya kujihami sioni ajabu maana mbona huwa tunawafunga kamba wahalifu kisha tunawapeleka vituoni,japo kuna wakati mwingine raia wanajichukulia sheria mkononi kwa kuwachoma moto.hatujawahi kushuhudia watu wakiwafunga kamba wahalifu?
Wengine hatumtetei Jerry bali tunapinga mfumo mzima uliotumika kumshtaki na kumhukumu Jerry ndani na nje ya vyombo vya haki.Wewe kama una uyajuayo kuhusu Crime buster Jerry, mwaga humu usafishe wanaotuhumu Polisi kwa kumfanyizia.Vinginevyo lawama zitaendelea tu.Tunazidi kukosa imani na askari siku hadi siku.Imefkia mahala mtu akiona askari anashtuka na kukimbia kama vile kakutana na jambazi.Hii ni mbaya sana
Kwa maoni yangu mimi siyo suala la kipi ni hatari kuliko kingine. Suala hapa ni nini motive ya mwandishi wa habari kumiliki pingu? Ukiona hilo ni la kawaida, kuna siku tutamkuta na sare za moja kati ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Mbona kumiliki filimbi haijawahi kuwa issue ya ajabu? Ukiona watu wanashangaa ujue this is uncommon!
Kwanza nikupongeze Jerry Muro kwa kushinda kesi yako dhidi ya Jamhuri, na baadae kujipatia tuzo ya ubora wa kazi zako na kile kilichoitwa ujasiri wako katika kufichua maovu yaliyopo ndani ya jamii.
Sasa baada ya habari hizi njema, ni wakati muafaka sasa kuueleza umma wa watanzania matumizi ya zile pingu ulizokiri kuzimiliki na hata kutuonyesha stakabadhi ya manunuzi ya pingu hizo. Tunakuomba ufanye hivyo kwa sababu wewe Jerry Muro sasa umeingia kwenye rekodi za dunia kama mwandishi pekee wa habari duniani mwenye kumiliki kifaa ambacho ni vyombo vya ulinzi na usalama pekee ndiyo wana mamlaka ya kumiliki na matumizi. Au unataka kutuambia kwamba kazi zako za uandishi zinahitaji kujihami na wakati mwingine ku-effect arresting powers za wahalifu mbalimbali? Je, mamlaka hii umeipata wapi wakati hata Polisi waliostahili kukukasimu wamekukana na kukuchukulia hatua?
Bila majibu fasaha, sitashangaa siku nyingine nikisikia unamiliki mahakama (lakini siyo hii iliyokuachia huru katika mazingira ya utata) na hata magereza na vituo vyako vya polisi.
Muro please, come out clean!
Kwamba aliomba rushwa nadhani hayo ni mawazo yako tu. mahakama, baada ya kuisikiliza kesi hii imemuona Jerry na wenzaake kuwa hawana hatia ya kosa lolote waliloshitakiwa nalo, likiwamo hilo la kuomba rushwa.Jerry Muro si investigative journalist wa kwanza nchini na duniani lakini hatujawahi kusikia hiki kituko popote pale. Kuwa investigative journalist si kuwa na vitu ambavyo katika hali ya kawaida watu hawatakiwi kuwa navyo. In this case bwana huyu alikuwa tayari ame-solicit rushwa akijiita ni mwanausalama. Tuwekewe bayana hili siyo kuishi kwa "ifs".
Ulifanikiwa kuwakagua waandishi wote waliokuwa wakiripoti habari za vurugu huko Afrika ya Libya, hasa wa vyombo vya CNN, BBC, Al Jazeera, nadhalika ili kudhibitisha rekodi hii ya Mr. Muro?Jerry Muro sasa umeingia kwenye rekodi za dunia kama mwandishi pekee wa habari duniani mwenye kumiliki kifaa ambacho ni vyombo vya ulinzi na usalama pekee ndiyo wana mamlaka ya kumiliki na matumizi.
Ulifanikiwa kuwakagua waandishi wote waliokuwa wakiripoti habari za vurugu huko Afrika ya Libya, hasa wa vyombo vya CNN, BBC, Al Jazeera, nadhalika ili kudhibitisha rekodi hii ya Mr. Muro?