Hongera Jerry Muro. Sasa tuambie hili!

Hongera Jerry Muro. Sasa tuambie hili!

Huyo Banyimwa anaonekana ni mbumbumbu wa sheria. Kama Jerry Muro hakustahili kumiliki pingu basi atunukulie vifungu vya sheria na siyo kutujazia thread bila sababu. Au aende kule maeneo ya Kisutu kwenye maduka ya wahindi atakuta wahindi wanazitumia ku secure generators zao wakati wa umeme unapokuwa umekatika
 
kasomeni sheria acheni kuwa kama waswahili una uhakika gani ahkimu alihongwa?
hakuna kesi ngumu kama za jinai kwani hakimu akishakuwa na mashaka ni bora kumwachia
ni bora kuachiwa watuhumiwa kumi kuliko kumfunga mtu mmoja asie na hatia
hakimu hatumii siasa kufunga anatumia sheria,kazi ya jamhuri ni kuthibitisha mashtaka kama wameshindwa hakimu afanyeje? mkikuwa mahakamani mkarekodi ushahidi mkaona kuwa ushahidi haukuwa na mashaka?
wabongo bwana mtu akiachiwa hakimu kala rushwa mtu akifungwa wanasema hakimu kamuonea au kahongwa ili amfunge
kumiliki pingu bostola sio kosa hakuna sheria inayokataza mtu binafsi kumiliki pingu kama iko iweke hapa
kama alivosema sita sita kuwa open kama una ushahidi
Kama una uhakika na Habari Hizi tafadhali BE OPEN;
 
Kwanza nikupongeze Jerry Muro kwa kushinda kesi yako dhidi ya Jamhuri, na baadae kujipatia tuzo ya ubora wa kazi zako na kile kilichoitwa ujasiri wako katika kufichua maovu yaliyopo ndani ya jamii.

Sasa baada ya habari hizi njema, ni wakati muafaka sasa kuueleza umma wa watanzania matumizi ya zile pingu ulizokiri kuzimiliki na hata kutuonyesha stakabadhi ya manunuzi ya pingu hizo. Tunakuomba ufanye hivyo kwa sababu wewe Jerry Muro sasa umeingia kwenye rekodi za dunia kama mwandishi pekee wa habari duniani mwenye kumiliki kifaa ambacho ni vyombo vya ulinzi na usalama pekee ndiyo wana mamlaka ya kumiliki na matumizi. Au unataka kutuambia kwamba kazi zako za uandishi zinahitaji kujihami na wakati mwingine ku-effect arresting powers za wahalifu mbalimbali? Je, mamlaka hii umeipata wapi wakati hata Polisi waliostahili kukukasimu wamekukana na kukuchukulia hatua?

Bila majibu fasaha, sitashangaa siku nyingine nikisikia unamiliki mahakama (lakini siyo hii iliyokuachia huru katika mazingira ya utata) na hata magereza na vituo vyako vya polisi.

Muro please, come out clean!
kabla ya kuandika kitu jaribu kusoma sheria za nchi zinasemaje
hivi unadhani kumiliki pingu na bastola ni kosa?kama ni kosa mahakama ingeshalifanyia kazi hilo swala
vitu hivyo vipo dukani vinauzwa kama bidhaa nyingine
 
Kila mtu ana kitu kinachoitwa citizen power of arrest! Sasa Kama wengine hatuna pingu, si tatizo wengine wakiwa nazo maana hii ndo inaonyesha kazi harisi ya polisi jamii!!

Kwanza nikupongeze Jerry Muro kwa kushinda kesi yako dhidi ya Jamhuri, na baadae kujipatia tuzo ya ubora wa kazi zako na kile kilichoitwa ujasiri wako katika kufichua maovu yaliyopo ndani ya jamii.

Sasa baada ya habari hizi njema, ni wakati muafaka sasa kuueleza umma wa watanzania matumizi ya zile pingu ulizokiri kuzimiliki na hata kutuonyesha stakabadhi ya manunuzi ya pingu hizo. Tunakuomba ufanye hivyo kwa sababu wewe Jerry Muro sasa umeingia kwenye rekodi za dunia kama mwandishi pekee wa habari duniani mwenye kumiliki kifaa ambacho ni vyombo vya ulinzi na usalama pekee ndiyo wana mamlaka ya kumiliki na matumizi. Au unataka kutuambia kwamba kazi zako za uandishi zinahitaji kujihami na wakati mwingine ku-effect arresting powers za wahalifu mbalimbali? Je, mamlaka hii umeipata wapi wakati hata Polisi waliostahili kukukasimu wamekukana na kukuchukulia hatua?

Bila majibu fasaha, sitashangaa siku nyingine nikisikia unamiliki mahakama (lakini siyo hii iliyokuachia huru katika mazingira ya utata) na hata magereza na vituo vyako vya polisi.

Muro please, come out clean!
 
...hakuna sheria yoyote inayomkataza mtu kumiliki pingu. Kikubwa na procedures za upatikanaji wake,zikiwa zimepatikana kihalali:, si kosa kwa Jerry au mtu mwingine yeyote kuwa nazo
 
Kwa maoni yangu mimi siyo suala la kipi ni hatari kuliko kingine. Suala hapa ni nini motive ya mwandishi wa habari kumiliki pingu? Ukiona hilo ni la kawaida, kuna siku tutamkuta na sare za moja kati ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Mbona kumiliki filimbi haijawahi kuwa issue ya ajabu? Ukiona watu wanashangaa ujue this is uncommon!

kwa upande wangu sioni kama kuna tatizo kwa yeye kumiliki PINGU wala Pisto,kwani Lage anamiliki pisto hivi yeye ni polisi?

najua mimi ni kwamba sheria ya nchi inaruhusu kumiliki vitu vyote hivyo ili mradi tu vipatikane kwa njia halali,kama pingu inge kuwa ni haramu basi Mahakama isinge ruhusu arudishiwe pingu zake

tatizo letu bado hatujui ni vitu gani tunatakiwa kumiliki na vitugani hatutakiwi kumiliki,cha msingi hapa ni kupata wanasheria watakao tueleza juu ya yote hayo

pia kuhusu kurudi TBC ni haki yake kama mtanzania wala haitaji mtu ampigie kifua,jamani ni vyema mkajua haki zenu,pindi mnapokumbwa na matatizo kama hayo,watu wanafikilia kupigiwa kifua mda wote si kweli,

anahaki ya kurudi kazini na kulipwa mishahara yake yooooooooote tangu walipo msimamishia mishahara yake,someni waraka wa serikali
 
unajua hata kamba nayo ni pingu? sasa wewe ukikutwa na kamba mfukoni mwako ni kosa? mbona pingu zinauzwa tu hata yoyote akitaka anauziwa, jaribu kutembelea maduka yanayouza silaha waulize, lakini hawawezi kukuuzia AK 47.
 
Kama bastola na pingu anavimiliki kihalalai kwa nini asirudishiwe? Are you out of your mind?

mkuu,kuna watu humu wanakwenda kama ng'ombe ama mbuzi,yaani mtu afikilii kwanini mahakama iruhusu huyu bwana kurudishiwa vitu vyake,kama ingekuwa si ruhusa kwa yeye kumiliki vitu hivyo basi asingepewa haki ya kumiliki

mbona hata wakulima,walimu,wafanyabiashara wanamiliki vyooote hivyo,ama kwa kuwa yeye ni mwandishi? je hana haki ya kumiliki kwa kuwa ni mwandishi?

Mtanzania yeyote yule anahaki ya kumiliki Pingu na pisto haijarishi mtanzania huyo ni mwalimu,polisi,mwanasiasa,mkulima ama mwandishi wa habari,ilimradi tu matumizi yake yasiwe kinyume na maombi ya awali
 
Kwani Pingu si kamba ya chuma tu iliyo na ufunguo. Kwani pingu na kufuli ya baiskeli tofauti yake nini? manake zinaweza kuwa na kazi ile ile. Hata mimi ninayo pingu na huwa nafungia baiskeli yangu. Ni mawazo finyu kuwa pingu inamilikiwa na askari. Ila huyo aliyeanzisha hii thread anaona ni sawa kumiliki silaha ya moto. Nimwambie tu haya ni mazoea kwamba watu wanamiliki silaha za moto kama bastola na n.k. na kwamba kwa kuwa pingu imezoeleka kushikwa na askari yeye linampa tabu kidogo. Lakini ukweli ni kuwa, PINGU NI KAMBA YA CHUMA ILIYO NA UFUNGUO KAMA KUFULI YA BAISKELI

Mkuu hapa umenena hatuna haja ya kuendelea kuijadili! Muro alinunua baada ya kuona inauzwa bila masharti yoyote tena kwa bei poa! Kama anamiliki bastola wht is pingu??
 
nyie askari wapelelezi na waendesha mashtaka, si mkate rufaa kuliko kuja kulalama hapa?
Siku nyngine mfanye kazi zenu safi/vizuri maana mmezidi kuzembea kazi.acheni kusumbua wananchi,
hasa nyie askari wa barabarani.kama jerry alitoa kitu kidogo, katika nchi ya kitu kidogo na watu wake wadogo, kuna la ajabu lipi ikiwa nanyi mnavutaga kitu kidogo?au kesi hii mliogopa kuvuta?huwa mnashangaza sana.kitu kidogo nyie huwa mnaongoza na hizo mahakama sasa msituletee hapa.

wape vidonge vyao!
 
Kwa maoni yangu mimi siyo suala la kipi ni hatari kuliko kingine. Suala hapa ni nini motive ya mwandishi wa habari kumiliki pingu? Ukiona hilo ni la kawaida, kuna siku tutamkuta na sare za moja kati ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Mbona kumiliki filimbi haijawahi kuwa issue ya ajabu? Ukiona watu wanashangaa ujue this is uncommon!

kama ni pingu hiyo sio ishu njoo huku vijijini .balozi .mw/kiti wa kijiji.afisa mtendaji kila moja ana pingu zake ni jambo la kawaida sana nyie uko mjini kumbe bado washamba !
 
Kwa maoni yangu mimi siyo suala la kipi ni hatari kuliko kingine. Suala hapa ni nini motive ya mwandishi wa habari kumiliki pingu? Ukiona hilo ni la kawaida, kuna siku tutamkuta na sare za moja kati ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Mbona kumiliki filimbi haijawahi kuwa issue ya ajabu? Ukiona watu wanashangaa ujue this is uncommon!

Kwa hiyo kama Jery angekkutwa na kamba ya manila au katani ngumu, usingekuwa na mashaka? Vyote hivi vina uwezo wa kufanaya kazi ya pingu!
 
Back
Top Bottom