Kwanza nikupongeze Jerry Muro kwa kushinda kesi yako dhidi ya Jamhuri, na baadae kujipatia tuzo ya ubora wa kazi zako na kile kilichoitwa ujasiri wako katika kufichua maovu yaliyopo ndani ya jamii.
Sasa baada ya habari hizi njema, ni wakati muafaka sasa kuueleza umma wa watanzania matumizi ya zile pingu ulizokiri kuzimiliki na hata kutuonyesha stakabadhi ya manunuzi ya pingu hizo. Tunakuomba ufanye hivyo kwa sababu wewe Jerry Muro sasa umeingia kwenye rekodi za dunia kama mwandishi pekee wa habari duniani mwenye kumiliki kifaa ambacho ni vyombo vya ulinzi na usalama pekee ndiyo wana mamlaka ya kumiliki na matumizi. Au unataka kutuambia kwamba kazi zako za uandishi zinahitaji kujihami na wakati mwingine ku-effect arresting powers za wahalifu mbalimbali? Je, mamlaka hii umeipata wapi wakati hata Polisi waliostahili kukukasimu wamekukana na kukuchukulia hatua?
Bila majibu fasaha, sitashangaa siku nyingine nikisikia unamiliki mahakama (lakini siyo hii iliyokuachia huru katika mazingira ya utata) na hata magereza na vituo vyako vya polisi.
Muro please, come out clean!