Zanzibar 2020 Hongera Hussein Mwinyi kuutangazia Umma kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi

Hongera sana kwa kuutangazia Umma wa Tanzania kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi, ni sawa kwa kuanza kuwatahadharisha wanaopanga kukuharibia pepo yako, ama hapo umetoa kauli nzuri ambayo Inshaallah isiwe na shaka ndani yake.

Huku ni kujipambanua na mbinu zilizokuwa zinatumika kuwaweka viongozi madarakani na kama nilimsikia Magufuli akigusia haki itumike, katika kupata mshindi halali bila ya wizi.

Je, mnajua maana yake watu hawa kujitenga na kura za wezi? Kikinuka watakaobeba msalaba ni tume ya Uchaguzi na viongozi wa vikosi watakaokubali kuingizwa mjini na mitego ya CCM matumbo.


Kakutangazia wewe au alitangaza kupitia Redio na TV za Giningi ??
 
Mtu wa bara hawezi kuwa Rais wa Zanzibar Mkuu ni katiba ya SMZ inasema hivo sio maneno yangu. Baba ake amekuwa Rais wa Zanzibar maana yake na yeye ni Mzanzibari.
Kwa kifupi tu Dr Hussein Mwinyi amewekwa kwa mapenzi na faida ya watawala
 
Huyu JP aliyewaambia watendaji kuwa awape mshahara halafu wamtangaze mpinzani? Huyu aliyefanyia figisu vyama vya upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, au huyu aliyekataza wenzake wasifanye siasa miaka minne hata mikutani ya ndani, huyu anayenunua wabunge wa upinzani. Mmeanza kuogopa sasa, endeleeni
Zile kauli za JPM ni ushahidi, Lissu ameshaukusanya kuendelea na mbele katika kutafuta haki yake.
 
Akikubali na kusimama na msimamo huo. atatokea kuheshimika sana katika jamii na atakuwa muungwana kuliko maraisi wote wa CCM waliopita zanzibar. Historia atayoweka zanzibar atakubalika miongoni mwa jamii yetu. Raisi Shein na Sefu Ali Iddi ni katika viongozi wanao nuka zanzibar wala hawana thamani yoyote kwa wazenji.
 
Lazima atasukumizwa tu na wazee wa kijani kibichi. Alisukumizwa ndio Shein swala tano licha ya kukataa katakata dhuluma.
 
Back
Top Bottom