Zanzibar 2020 Hongera Hussein Mwinyi kuutangazia Umma kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi

Hua Imani na siasa hua haviingiliani kabisa,hapo kama kweli kasema kauli iyo basi ngoja tuone wakati ukifika
 
Hongera sana kwa kuutangazia umma wa Tanzania kuwa hutaki ushindi wa kura za wezi au wizi, ni sawa kwa kuanza kuwatahadharisha wanaopanga kukuharibia pepo yako, ama hapo umetoa kauli nzuri ambayo Inshaallah isiwe na shaka ndani yake.

Huku ni kujipambanua na mbinu zilizokuwa zinatumika kuwaweka viongozi madarakani na kama nilimsikia Magufuli akigusia haki itumike, katika kupata mshindi halali bila ya wizi.

Je, mnajua maana yake watu hawa kujitenga na kura za wezi? Kikinuka watakaobeba msalaba ni tume ya Uchaguzi na viongozi wa vikosi watakaokubali kuingizwa mjini na mitego ya CCM matumbo.
Sidhani kama anakiamini na kukisimamia hicho alicho kisema
 
CCM Zanzibar wameshashindwa,na mwaka huu watashindwa vibaya sana. Dr Hussein Mwinyi ni mtu mstaarabu amehamua kujitenga mapema na uhuni wowote ule Ila aende mbali zaidi wakimtangaza kwa mabavu akatae wampe hiyo nchi Jecha aiongoze.
 
Kumbe anajua kura za aina hiyo zipo na zimewahi kutumika. Vizuri. Lakini hayo ni maneno matamu kwani aliyeshika mpini si yeye ni JPM na watu wake.

Wengi tunasahau, Kikwete alisema CCM haitamfia mikononi mwake-akamkata Lowasa na kule Zenj wakamuibua Jecha. Mtihani mkuu wa JPM utakuwa Zanzibar.
Zenji ndiyo matokeo yanajulikana hata kabla ya kampeini kuanza kuwa ccm yupo mahututi
 
Mtu wa bara hawezi kuwa Rais wa Zanzibar Mkuu ni katiba ya SMZ inasema hivo sio maneno yangu. Baba ake amekuwa Rais wa Zanzibar maana yake na yeye ni Mzanzibari.
Anaenda kuwa kiongozi wa kwanza kuikabidhi ccm kwa upinzani
 
kweli aisee..... Mwinyi na JPM ni dhahiri wanawaangushia jumba bovu Kaijage na mwenziwe wa Zanzibar pamoja na Sirro.
wakiingia kichwa kichwa na kuharibu halafu kupelekea intervention ya ICC, wataliwa hivyo vichwa mchana kweupe!!
Wanajifanya kusahau yaliyo wakuta kina Ruto
 
kweli aisee..... Mwinyi na JPM ni dhahiri wanawaangushia jumba bovu Kaijage na mwenziwe wa Zanzibar pamoja na Sirro.
wakiingia kichwa kichwa na kuharibu halafu kupelekea intervention ya ICC, wataliwa hivyo vichwa mchana kweupe!!
Huyu JP aliyewaambia watendaji kuwa awape mshahara halafu wamtangaze mpinzani? Huyu aliyefanyia figisu vyama vya upinzani kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, au huyu aliyekataza wenzake wasifanye siasa miaka minne hata mikutani ya ndani, huyu anayenunua wabunge wa upinzani. Mmeanza kuogopa sasa, endeleeni
 
Back
Top Bottom