Hongera Hazina kwa kazi nzuri

Hongera Hazina kwa kazi nzuri

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
236
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Napenda kuwapongeza wahusika wote wanaohusika na hazina kwa kutoa mishahara ya watumishi mapema kabla ya tarehe stahili; wamefanya kazi nzuri sana mwezi huu ambao bado siku chache Watanzania wataungana na watu wengine duniani kusherehekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya. Hongera Mawaziri wahusika, makatibu wa Wizara, Wakurugenzi na wadau wengine pokeeni pongezi hizo na mwendelee hivyo na miezi ijayo.
 
Tatizo hazina wako bias! Sikukuu za kiislamu huwa hawawahishi kutoa mishahara na hili nina ushahidi nalo imetokea hivyo mara kadhaa kwenye sikukuu ya eid.
 
mkuu upo kitengo kipi,maana huku kwetu akaunti bado zimenuna
 
Tatizo hazina wako bias! Sikukuu za kiislamu huwa hawawahishi kutoa mishahara na hili nina ushahidi nalo imetokea hivyo mara kadhaa kwenye sikukuu ya eid.

tatizo la sikukuu ya eid ni kutokua na tarehe maalum
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Napenda kuwapongeza wahusika wote wanaohusika na hazina kwa kutoa mishahara ya watumishi mapema kabla ya tarehe stahili; wamefanya kazi nzuri sana mwezi huu ambao bado siku chache Watanzania wataungana na watu wengine duniani kusherehekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya. Hongera Mawaziri wahusika, makatibu wa Wizara, Wakurugenzi na wadau wengine pokeeni pongezi hizo na mwendelee hivyo na miezi ijayo.

Mkuu hiyo ni right yenu na sio privilege.
 
Tatizo hazina wako bias! Sikukuu za kiislamu huwa hawawahishi kutoa mishahara na hili nina ushahidi nalo imetokea hivyo mara kadhaa kwenye sikukuu ya eid.
Mohamedi Mtoi,

..hata wakati huu ambapo Katibu Mkuu ni Alhaj Ramadhan Kijjah?

..vipi kuhusu wakati waziri wa fedha akiwa ni Prof.Kighoma Ali Malima, Jakaya Mrisho Kikwete, Zakhia Meghji, na Mustafa Mkulo??

..hao mawaziri wote Waislamu nao walikuwa wakiwakandamiza Waislamu wenzao??
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo mnataka Eid ikiangukia tarehe 10 basi mshahara nao utoke? Kuwahisha mshahara Krismasi ni reasonable kwa kuwa sikukuu ipo wiki la mwisho la mwezi. Sasa nyie mnatakaje?
 
hapo napo pa kujiuliza....ina maana hata Waisilamu wanakandamiza wenzao,...``utasikia MFUMO KRISTO``

Mohamedi Mtoi,

..hata wakati huu ambapo Katibu Mkuu ni Alhaj Ramadhan Kijjah?

..vipi kuhusu wakati waziri wa fedha akiwa ni Prof.Kighoma Ali Malima, Jakaya Mrisho Kikwete, Zakhia Meghji, na Mustafa Mkulo??

..hao mawaziri wote Waislamu nao walikuwa wakiwakandamiza Waislamu wenzao??
 
Mohamedi Mtoi,

..hata wakati huu ambapo Katibu Mkuu ni Alhaj Ramadhan Kijjah?

..vipi kuhusu wakati waziri wa fedha akiwa ni Prof.Kighoma Ali Malima, Jakaya Mrisho Kikwete, Zakhia Meghji, na Mustafa Mkulo??

..hao mawaziri wote Waislamu nao walikuwa wakiwakandamiza Waislamu wenzao??

Mkuu JokaKuu
kwanza hongera kuja na haya majina ya walio wahi kuwa makatibu na mawaziri wa wizara ya fedha. Natamani nikugongee like 1000 hivi.

Hata hivyo bias niliyoisema si kumaanisha eti kwa kuwa hazina pana wakristo wengi! La hasha (mimi sio muumini wa udini) ni kwa kuwa wanawahi kutoa mishahara kwenye xmass lakini hawafanyi hivyo kwenye sikuu za eid, hapo haijalishi kuwa katibu au waziri ni muislamu ama laa. Nilicho kiangalia hapo ni double standard peke yake mkuu sio ka ulevi ka udini.

Hongera tena great thinker JokaKuu kwa comment yako ambayo inajibu vizuri hoja ya mtu ambae labda angeuliza akiwa na tingasi la udini kichwani.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hazina wako bias! Sikukuu za kiislamu huwa hawawahishi kutoa mishahara na hili nina ushahidi nalo imetokea hivyo mara kadhaa kwenye sikukuu ya eid.

mkuu. Zanzibar huwa wanatoa mishahara kabla tu ya sikukuu za kiislam?
 
tatizo hazina wako bias! Sikukuu za kiislamu huwa hawawahishi kutoa mishahara na hili nina ushahidi nalo imetokea hivyo mara kadhaa kwenye sikukuu ya eid.

sikuku hazijulikani ni tarehe gani hadi mwezi utoke
 
Back
Top Bottom