Hongera HALIMA MDEE umeonyesha ukomavu

Hongera HALIMA MDEE umeonyesha ukomavu

Status
Not open for further replies.
Hizi zote ni mbinu za kuhamakisha viongozi wa cdm mpate cha kuandika.
 
Tuliwaambia kuwa zitto hafukuziki ndanimya chadema wakabisha ona sasa wanaishia kuvuna aibu kubwa na kulia pasipo msiba chadema ni zitto akiondoka inakufa.

Natofautiana na wewe kidogo kwenye hili,ya kwamba cdm ni zzk na akiondoka au kuondolewa cdm itakufa,hivi hujui cdm ni taasisi?na taasisi si mtu 1,uliwahi kujiuliza mwl alitutoka lakini ccm haikufa?sir alex aliondoka man u na haijafa,hata leo arsene akiondoka pale emirate arsenal haiwezi kufa,sijui umetumia falsafa gani kama great thinker,halafu niwaulize,hivi kwa mtindo huu wa kuropoka bado ZZK ni presidential material?tunaweza kuwa na rais wa nyie mkimwaga ugali sisi tunamwaga mboga?uliona ustahimilivu wa Edward Lowassa wakati wa sakata la Richmond?Alitumia busara na hekima kukaa kimya,mnafikiri alishindwa kuropoka?Anyway mi sijui bhana.Ukiona kiza kinene katikakati ya usiku mwingi uje kunakaribia kupambazuka.
 
Halima is smart lieke asha migiro,anna tibaijuka, and young ladies like me.congrats Halima

aache kula raha na ester bulaya ahangaike na migogoro ya kutaka sifa na uongozi kana kwamba viwanja vya starehe vimeisha,
 
kama baraza kuu litashidwa maamuzi ya kawaida kama haya ,,,basi CDM itakua ni tawi la CCM,,,kama washidwa kuamua kwa umoja dhidi ya kibaraka, msaliti, basi CDM itakuwa si chama makini,,,,,kama watashidwa kufanya maamuzi mepesi kabisa kwa sababu ya kuhogwa je KURA 2015 wataweza kulinda......Kama mimi mwanachama wa kawaida nahasira hivi je mtu ambaye ni baraza kuu itakuaje,,,,,Mimi ningekuwa huko baraza kuu si kumfukuza tu mimi hata MAKOFI angeyapata

Wewe nadhani akuwa Dokta wa miti shamba. Kwa ninavyojua mimi daktari hatakiwa ku conclude jambo bila kuwa na facts beyond reasonable doubt na ndio maana mgonjwa anafanyiwa vipimo maabara ili kupata uhakika kabla ya kumpa tiba.

Sasa mwenzetu unasema ungekuwa baraza kuu ungemchapa makofi, je ukiachilia mbali waraka wa kumhafua ZZK unaweza kutupa ushahidi kwa nini ZZK anaitwa msaliti, anastahili kufukuzwa na kchapwa makofi?
 
Mleta mada na suporters wake wanatafuta kupandikiza jambo fulani kutafuta thympathy ya mlengwa, lakini wameangukia pua!!
CDM iko imara, haitakubali kumbeba maharuni msaliti ZZK
lazima atoswe!!
Anapumulia pipes za mahakama!!


Mkuu hapo kwenye red umeziumiza mbavu zangu, Chonde chonde nitake radhi.
 
Mnyika katumwa kuzungumza aliyozungumza, wala hakubaliani nayo.

ukitumwa kwenda kulala na mama yako na wewe ukafanya hivyo..jamii itakuitaje? usitake kumlisha maneno...
 
Tuliwaambia kuwa zitto hafukuziki ndanimya chadema wakabisha ona sasa wanaishia kuvuna aibu kubwa na kulia pasipo msiba chadema ni zitto akiondoka inakufa.

hafukuziki kivipi wakati kwa ss ni mbunge wa mahakama km hamad rashid
 
Mnyika disapointed me katika hili sakata.

Mnyika ni mkurugenzi wa habari wa chama. Lazima atoe taarifa ambayo cc imepitisha, yeye ndo chanzo cha mawasiliano rasmi (official communication) kati ya chama na umma. Unategemea atasema nini kwenye sakata kama hili!? Lazima aseme na kutetea nini chama kimesema hata kama yeye binafsi hajaridhika. He has no choice by virtual of his position as a party prime spokesperson!! Mtamchukia bure tu
 
Mnyika hakupaswa kujiingiza kwenye hili.hakuwa na sababu ya kujiweka kwenye level ya akina Lema,Msigwa na Sugu.Ni kujidharirisha.

Bila kujua,amejishushia heshima katika hili.

Jamani eleweni mfumo wa utawala ulivo. Mnyika ni mkurugenzi wa habari wa chama, ulitegemea aseme nini katika sakata kama hili?! Lazima akisemee chama kwani ndo kazi yake. Hawezi kwenda kinyume hata kama yeye binafsi kama mnyika hapendi uamuzi ulochukuliwa na chama. Huo ndo utaratibu. Mtamchukia bure tu
 
Kwa wanaojua msimamo wa Mdee, tunaelewa kwa nini yuko kimya!. Pia ameisha jua madhambi ya Chadema kufanya fault finding cherry picking za kuwahukumu watu kwa makosa yao tuu regardless wameifanyia nini Chadema. Anajijua aliingiaje Chadema, what was her inspiration hadi kujoin Chadema. Wewe umemuona Halima tuu?!. Hujiulizi mbona Prof. Safari yuko kimya?.
Pasco

Halima amechukizwa pia na mpango wa BABU SLAA kutaka kumpeleka MCHUMBA wake JOSEPHINE kugombea KAWE wakati jimbo hilo bado linaongozwa na Halima, SLAA aka BABU ni mtu hatari sana kwa demokrasia.
 
watz ni wazuri sana wa kuongea wakati mambo yamesha fanyika na impact zake zimeonekana...Ukienda kenya wanakwaambia hapana ongea na Watz, wako na Maneno mengi,kiswahili mirefu.....Maji yakishamwagika hayazoleki pia dua la kuku halimpati mwewe....Siasa za TANZANIA NI ZA KUVIZIANA ni kama sarakasi za kichina SI ccm,cdm n.k.
 
Mnyika disapointed me katika hili sakata.

Toa sababu na tuache kuongea kama kasuku!Kwa nn unasema Mnyika kakusikitisha kwenye hii melee?

Ungekuwa ndiyo wewe msemaji wa CHADEMA na CC imeamua ww ungefanya nn tofauti na alichofanya Mnyika?

Nasubiri majibu!
 
Naungana nawe kumpongeza Halima Mdee kwa hili.Amejijengea heshima kubwa sana.

Unajua kura ya Halima Mdee kwenye maamuzi ya CC ilikuwa vipi?

Labda kwanza wala hukuwa unajua kuwa Mdee ni mjumbe wa CC nahisi!

Viroba vinamaliza sana uwezo wa kufikiri wa vijana wetu!
 
Unajua kura ya Halima Mdee kwenye maamuzi ya CC ilikuwa vipi?

Labda kwanza wala hukuwa unajua kuwa Mdee ni mjumbe wa CC nahisi!

Viroba vinamaliza sana uwezo wa kufikiri wa vijana wetu!

Ingekuwa ni viroba pekee ingekuwa nafuu, ile biasha inayofanywa na Prince inaharibu sana vijana wa limumba.
 
Tuliwaambia kuwa zitto hafukuziki ndanimya chadema wakabisha ona sasa wanaishia kuvuna aibu kubwa na kulia pasipo msiba chadema ni zitto akiondoka inakufa.

Zitto kwa miaka yake 9 ya Ubunge Kigoma na diwani wake mmoja Kigoma Kaskazini ndiyo akiondoka CHADEMA inakufa?

Zitto hafukuziki kivipi wakati jana kalindwa na Mahakama iliyomuokoa na ubunge wake?

Very poor reasoning from Zitto's left wing supporter!Mulugo kweli umetuweza na Div yako 5 maana vijana wetu uwezo wao wa kufikiri is almost zero!
 
Mnyika katika sakata hili huwezi kumlaumu kwakuwa alikuwa akiongea kama "cheo" chake ndani ya chama na si kama JohnJohn Mnyika!!:decision:
 
Kwa wanaojua msimamo wa Mdee, tunaelewa kwa nini yuko kimya!. Pia ameisha jua madhambi ya Chadema kufanya fault finding cherry picking za kuwahukumu watu kwa makosa yao tuu regardless wameifanyia nini Chadema. Anajijua aliingiaje Chadema, what was her inspiration hadi kujoin Chadema. Wewe umemuona Halima tuu?!. Hujiulizi mbona Prof. Safari yuko kimya?.
Pasco
Pasco, safati amenukuliwa na Mtanzania la jana kuwa anaunga mkono uamuzi wa CC. Halima naye amechoshwa na usaliti wa Zitto amenyamaza kwakuwa hakuna jipya atakalosema. Yote yameshasema
 
Mwalimu J.K.NYERERE """""alieleza kuwa dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu........amin msiamini huu ndo mwanzo wa kutafunana ndani ya CDM na hawatokaa salama milele......., wabunge wote wa CHADEMA kwa namna moja au nyingine tumewajua wapo upande upi! Kimsingi nampongeza Mbunge wa Kawe HALIMA MDEE kwa kukaa kimya, kutotoa neno lolote ambalo kwa namna moja au nyingine lingeendelea kukuza mgogoro! CHADEMA igeni kwa mwana Mama HALIMA MDEE kawashinda busara wanaume wote ndani ya CHADEMA upeo wa kufikiri! Nakushauri usije comment chochote juu ya hili sakata utajijengea heshima kubwa kwa nchi hiii

.
Kuna ya kunyamazia na kuna ambayo hsyafai kunyamazia. Hili a Zitto sii la kunyamazia dhambi ya usaliti ni mbaya sana ati. Hata Muumba Mungu wetu angemnyamazia shetani kwa uasi wake malaika wasingelimwelewa. Aliwaambia huyo ni adui yenu na siwapi ruhusa ya kumuua kwani namhifadhia haki ya uhai lakini mkemeeni na kujiweka mbali nae.
Zitto ni msaliti na hafai kuweko ndani ya kambi ya wakombozi maana amekuwa akichukua pesa kutoka kwa watesi wetu kwa nia ya kuhujumu movement.
Nasema tena sii busara kumnyamazia msaliti.
.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom