Hongera Dr. Mwakyembe, hongera TRC

Dr mwakyembe ametimiza wajibu wake!
kupitia JF nawataka watanzania wote tuilinde treni yetu kwa nguvu zote,usafi uwe 100%, mama na dada zangu wangu wanaonunua samaki ferry wabuni package mpya ya samaki wao ili kuepusha shombo,harufu mbaya na uchafu kwa ujumla.
 
Naunga mkono hongera anazopewa mh mwakyembe, but guys worldwide hakuna biashara ya train inayotegemea abiria, bali biashara ya train inategemea usafirishaji wa mizigo kwani gharama za kuendesha train haziwezi kufidiwa kwa nauli za abiria bali nauli hizo huwa NI charges tu ambazo bila faida ya usafirishaji wa mizigo, hizo charges are nothing. So mapinduzi ya usafirishaji kwa njia ya train yatakuwa successfully kama tu mizigo mikubwa kutoka na kuingia bandarini na sehemu zingine za nchi zitaanza kutumia train kusafirishwa. Barabara za lami worldwide hazitumiki kusafirisha heavy cargo,ni Tanzania tu ambapo mafisadi wanamiliki malori na ndo wanalazimisha barabara zibebe mizigo mizito.
 
Mwakyembe alipoomba miezi sita ili treni iwe inafanyakazi, Clouds walimtukana sana, hasa Gerald Hando na PJ, leo eti wanamsifia.
Clouds acheni uzandiki na unafiki, NINAWACHUKIA
Mkuu hii ungeianzishia thread kabisa tuwaumbue wanafiki wote
 
Naomba nitumie nafasi hii kumpongeza Dr. Harison Mwakyembe pamoja na washika dau wenzake kwa jitihada kubwa walizozifanya hadi ahadi yake ya kutuletea usafiri wa tren hapa jijini kukamilika tangu uhuru wa nchi hii upatikane.

SHIME MWAKYEMBE.

:israel:
Ingefaa na ingependeza mabasi yote ya mikoani yaishie Chalinze abiria wote waingi kwenye traini. Ubungo - station in umbali mdogo sana wala sidhani kama huo mradi utakuweza kujiendesha (sustainability) Rahajipe
 
Last edited by a moderator:
YES WE CAN - BRAVO! Mh. Mwakyembe, Mwai-PINDA, Mwa-MATEMA BEACH, Mwa-ITUNGI PORT, Mwa-mto SONGWE!!!
 
this dude(mwakyembe) has done something good for the people and the country, in my own opinion you deserve the highest office in this land of semi-illiterates buffoons, tatizo ni hiyo sumu jamaa waliokupiga nayo inaweza kuwa imefifisha life span yako, na la muhimu kabisa uoga unakufanya unakuwa mnafiki huwezi kusimamia ukweli mpaka mwisho, otherwise wewe ni jembe.
 
Naomba nitumie nafasi hii kumpongeza Dr. Harison Mwakyembe pamoja na washika dau wenzake kwa jitihada kubwa walizozifanya hadi ahadi yake ya kutuletea usafiri wa tren hapa jijini kukamilika tangu uhuru wa nchi hii upatikane.

SHIME MWAKYEMBE.

:israel:
Kwahili.. Ni kweli anastahili pongez!!
 
DAR tu??? Huko ndiko kwenye kamisheni ya pongezi!!huku kwetu msamaria mwema kajenga daraja la miti,baiskeli zetu sasa zinavuka kwenda ngambo kuchukua chumvi,mpunga na kuwapeleka wagonjwa dispensary!!vifo vitapungua sasa!!njaa itapata msukosuko sasa,,ila pongezi ni mpaka kamisheni ya pongezi imalize kazi dar,iende arusha,mwanza ndiyo tusikie ilipita hapa last week!!haya bana! Tanzania ni dar tu.
 
we ndio kilaza a.k.a mburula!! hujui job description!! ipo siku utamsifia house girl wako kwa kukufulia chupi lako,wewe ni lofa tena *****![/QUOTE]

dUH, Mgomba1: ndugu yangu cjawahi kuona unawaka namna hii, mbona umemshushia mvua ya mawe namna hii? au amekuta umeshaingiza overdrive!
 
Mwakyembe alipoomba miezi sita ili treni iwe inafanyakazi, Clouds walimtukana sana, hasa Gerald Hando na PJ, leo eti wanamsifia.
Clouds acheni uzandiki na unafiki, NINAWACHUKIA

Duuu mkuu unakumbukumbu sana hawa jamaa ni nyoka kazi yao kubwa ni kujipendekeza kwa viongozi tu
 
hakika anastahili pongezi...ila kuna kitu ambacho kidogo sijaelewa kinakuwaje.kwa kuwa treni ina mabehewa mengi,mfano mtu anashuka mabibo na yuko behewa la kwanza zen mwingine anashuka mabibo apo apo na yuko behewa la mwisho.inakuwaje apo??
 
Safi sana Dr.Mwakyembe,maana tatizo la usafiri Dar,ni JANGA..

chanzo ni upuuzi wa kujaza kila kitu Dar. Upuuzi mtupu. Bado wanaongeza vyuo na viwanda. Upuuzi. Mwakyembe, Magufuli, Tiba nao hawafikirii permanent solution. Nusu ya vyuo vikuu Tanzania viko Dar! Pathetic! Upuuzi
 
Naomba nitumie nafasi hii kumpongeza Dr. Harison Mwakyembe pamoja na washika dau wenzake kwa jitihada kubwa walizozifanya hadi ahadi yake ya kutuletea usafiri wa tren hapa jijini kukamilika tangu uhuru wa nchi hii upatikane.

SHIME MWAKYEMBE.

:israel:

MWAKYEMBE KARIBU CDM TUKUPE NCHI HII
SLAA KESHAPOTEZA MWELEKEO,,
:target: :confused2:

:A S shade:
 
anastahili pongezi kubwa kufanikisha hili kwani yapo mengi yanaishia kwenye makaratasi HEKO MWAKYEMBE NA WASAIDIZI WAKO WOTE.
 
DAR tu??? Huko ndiko kwenye kamisheni ya pongezi!!huku kwetu msamaria mwema kajenga daraja la miti,baiskeli zetu sasa zinavuka kwenda ngambo kuchukua chumvi,mpunga na kuwapeleka wagonjwa dispensary!!vifo vitapungua sasa!!njaa itapata msukosuko sasa,,ila pongezi ni mpaka kamisheni ya pongezi imalize kazi dar,iende arusha,mwanza ndiyo tusikie ilipita hapa last week!!haya bana! Tanzania ni dar tu.

hata mimi hili linanikera! Yote haya ni upuuzi wa kuweka kila kitu cha muhimu Dar! Kuna ulazima upi wa National hospital kuwa Dar na si Dodoma, singida au Tabora? Unaweka daraja la Kigamboni huku watu hawana visima vya maji na wanakufa? Huu ni upuuzi
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom