Hongera Dr. Mwakyembe, hongera TRC

Hongera Dr. Mwakyembe, hongera TRC

Mbon hizo kazi hazikufanywa toka mwaka 2005!

Kazi zilizopo na uozo anaourekebisha Jakaya ni wa Kuanzia nchi hii ilipopata Uhuru, unafikiri kaenda Ikulu na Taa ya ajabu, akiisuguwa tu siku yapili ya tayari? Jiulize waliokuwapo kabla yake walikuwa wapi kwa Miaka yote waliokuwepo madarakani?
 
We kweli Mgomba!! Viongozi wangapi wameshindwa kubuni mbinu, ikiwa ni pamoja na Mwanaasha? Tumia muda kidogo kufikiri kabla hujachangia! Unajiaibisha.

we ndio kilaza a.k.a mburula!! hujui job description!! ipo siku utamsifia house girl wako kwa kukufulia chupi lako,wewe ni lofa tena *****!
 
Hongera Dr H. Mwakyembe na timu yako katika kufanikisha huu usafiri. Sasa elekeza nguvu katika reli ya kati hali ni mbaya na wananchi wanateseka sana. Kila la heri katika kuwatumikia Watanzania wenzio.
 
Mwakyembe alipoomba miezi sita ili treni iwe inafanyakazi, Clouds walimtukana sana, hasa Gerald Hando na PJ, leo eti wanamsifia.
Clouds acheni uzandiki na unafiki, NINAWACHUKIA


Hakuna watu wanafiki na wazandiki Kama watangazaji wa clouds. Shame on them all
 
Mwakyembe ameonge kwa vitendo!!! Kwa kweli amethibitisha kuwa yeye ni kiongozi makini na mwenye vision. Nitafurahi kama viongozi wengine watajifunza na kufanya mambo mazuri kama Mwakyembe.
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Hongera Mwakyembe kwani umeonesha njia. Kwamba tukidhamiria tunaweza. Wapo wengine watakuja na kukubeza mara hili mara lile lakini kumbukeni kuwa hata safari ya kilometer 1000 huanza kwa hatua moja. Hivyo kadili tutakavyoendelea ndivyo tutaboresha zaidi kama taifa. Ni wakati sasa wa kufungua reli za Dar -Tabora, Tabora -Kigoma. Tabora - Mwanza, Tabora- Mpanda nazingine kadili tutakavo jaliwa kupata uwezo na naamini uwezo upo. Kufunguka kwa njia hizi kutaboresha usafirishaji wa mizigo hasa ukanda wa maziwa makuu. Najua wapo hasa wale wenye magari ya kusafirisha mizigo hawatapenda kuona hili likifanyika lakini lazima tupime kama taifa kwamba ni jambo lipi lina manufaa kwa jamii na taifa letu kwa ujumla. Nakumbuka zamani Isaka ikiitwa bandari ya nchi kavu kwasababu ya mizigo iliyokuwa ikisafirishwa mpaka pale kwa njia ya reli kabla ya kusambazwa kwenye nchi za Rwanda na Burundi. Shime Mwakyembe shirikiana na Wahandisi wa karakana ya pale Morogoro ili waweze kufufua engine zinazoweza kufufuliwa. Nakumbuka wakati flani waliwahi kusema kuwa wao wakiwezeshwa wanaweza kufanya kazi hiyo na wakati flani waliwahi kufufua kichwa kimoja na wakamwita Sylvester Rwegasira (RIP), aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU).
 
we ndio kilaza a.k.a mburula!! hujui job description!! ipo siku utamsifia house girl wako kwa kukufulia chupi lako,wewe ni lofa tena *****!

We kweli Mgomba, ambao haufai hata kupikia hata kujengea kibanda! Kwani mawaziri wote, ikiwa ni pamoja na mwanaasha wako, wana job descriptions zao, lkn wanashindwa kuzitimiza!! Usikimbilie matusi, unazidi kujiaibisha! Over!
 
:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky: Hahahahahaha leteni usafiri wa treni tukisubirima basi yaendayo kwa kasi ya ajabu...:becky::madgrin::becky:
 
Right Person at the Right Job at the Right Time. Bravoo Waziri wetu. Wangekutmia tangu wakati ule leo hii hata hizi barabara zinazobanduliwa lami wasingefanya hivyo. Nadhani ungekuwa na Plan nyingine. Huku ndiko kutumia Elimu yako kwa manufaa ya wengine. Watu wanasafiri kila kukicha kwenda hizo nchi zilizoendelea lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kuonyesha njia hii au hata kuondoa Takataka Dar au Ujenzi Holela na Biashara za Ajabu ajabu kando kando ya Barabara zetu. Pse waziri hakikisha huu usafiri unakuwa Sustainable kwa kuchagua watu sahihi wa kusimamia kazi hii. Asante sana kwa juhudi zako.
 
Harrison George Mwakyembe..aka Jembe aka Dr wa Ukweli PHD...nani anabisha??!!! nchi hii watu kama hawa ndio wanatakiwa sio kuleta wasanii kuongoza kwa maneno na porojo...

Tatizo yuko chama kibovu kilichozungukwa na wachafu
 
naam huo ni mwanzo sasa nchi inahitaji usafiri wa uhakika wa treni hadi mikoani
uwezo serikali inao wa kununua mabehewa mapya na ijengwe reli mpya na njia mpya ya umeme
hii itaokoa ajali nyingi za mabasi
kwa mlio dar mtakuwa mnasave muda wa kwenda na kurudi makazini
 
Afadhali lije,nitakuwa mpiga debe wa kwanza
 
RahajipeReally anastahili pongezi kwani ameonesha creativity kwa wizara yake.tumeshuhudia viongozi wetu wapenda safari kila siku angani but tunajiuliza huwa wanakaa mahotelini tu bila kujifunza chochote huko waendako!!Mwakyembe umekuwa role model historia ya nchi hii itakuenzi. Please fungua reli zote zilizokufa nchi hii.
daah,mbona unahatarisha sembe lake bro?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom