Hongera clouds media kuchangisha fedha yamatibabu ya Jetman

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
Wanabodi

Nisiwe mnafiki katika hili, napenda kutoa pongezi za dhati kwa clouds media group kwa kufanikisha kampeni ya "naamka na Jetman" aliyelala kwa muda wa zaidi ya miaka mitano

msanii huyo mkongwe alikua anahitaji zaidi ya Tsh milion 12 ya matibabu ili aweze kwenda kutibiwa nchini India
mpaka sasa nimemsikiliza mkurugezi wa kampuni hii Ruge mutahaba akitangaza kiasi kilichopatikana ni milion 15 mpaka sasa.

Hongera sana Clouds, mmeonesha moyo wa upendo kwa kujitoa katika hili

Pole msanii wetu Mungu akusimamie upone!
 
alikuwa naimba raga? au? asije kuwa ni mhaya? maana alikuwa anarekodi na kina Kidbwai
 
Huyu bro ,jina lake Ni ,Sammy ila kimziki alijiita Jetman kina kidbway Ni washkaji zake yeye Ni mwenyeji wa Mwanza Pasiansi ,Ni producer na mshonaji alikua Arusha kwa muda mrefu hata maradhi ameyapata akiwa huko,kwa Sasa familia ilimrudisha Mwanza !
 
Back
Top Bottom