Nimekumbuka kuwa mmoja ya Ahadi za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia CHADEMA ilikuwa ni kulinda Ardhi ya wananchi wa Singida kutoporwa na kampuni ya Kifisadi ya Wind East Africa Ltd, iliyokuwa inasaidiwa kwa nguvu zote na Mkuu wa Mkoa wa singida ndg. Perseko Kone. Kampuni hiyo ilifikia hatua za mwisho za kujimilikisha isivyo halali ardhi ya wananchi masikini. Tunampongeza Josephat Isango kwa kusimama kidete kuhusu suala hilo na kupambana na Mkuu wa Mkoa, mpaka sasa siku hizi Mkuu huyo hawezi hata kufanya mikutano ya hadhara kwa jinsi alivyoumbuka. Sakata hilo sasa limeisha wananchi ardhi yao imelindwa na kweli kijana amepambana. Tunatoa changamoto kwa wagombea wengine wa CHADEMA hata kama walishindwa wajaribu kutekeleza ahadi zao kwa wananchi hasa zile ambazo ziko chini ya uwezo wao. Bravo vijana wa CDM.