Binti Juliana, bado uko mdogo na mrembo kiasi fulani! Nakushauri ujipe likizo kidogo kwenye siasa ukafanye shughuli nyingine mpaka akili yao ipoe kwanza! Kama una nia kweli ya kufanya "siasa" kuwa "wito wako wa maisha", basi kina Nnape, Mwigulu & Co sio Model wazuri/sahihi kwako! Tafakari!
ccm ina ukomavu wa siasa au mlishindwa kuchakachua? Na bado 2015 tutalinda kura zetu msije fanya kama shinyanga mjini mliiba wazwaz! RIP ccm
Chama cha mapinduzi kingekuwa kinauwezo wa kusema baadhi ya wanachama wangeumbuka,maana CHAMA kingewakataa katika majukwaa,ukisoma katiba ya chama cha mapinduzi wachache sana wana sifa ya kuwa wanachama wa chama hiki
*Katiba ya chama mapinduzi nitanukuu
(Toleo la februari 1997) Fungu la kwanza
""Mtu atakayekubaliwa kuingia katika CCM au Kuendelea kuwa Mwanachama,ni yule anayetimiza masharti yafuatayo-
Mosi,kuwa mtu anayeheshimu watu
Pili,kuwa mtu anayefanya juhudi ya kuielewa,kuieleza,kuitetea na kuitekeleza ITIKADI na siasa ya CCM
Tatu,kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha utu,na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo
Nne,kuwa mtu anaependa kushirikiana na wenzake
Tano,Kuwa mtu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya umma,kulingana na miongozo ya CCM
Sita,kuwa wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake,kuwa mwaminifu,na kutokuwa mlevi au mzururaji
Saba,kuwa ama mkulima,mfanyakazi au mwenye shughuli nyingine yoyote halali ya kujitegemea
"VV"
Aisee nilidhani ushakufa sijakuona kitambo sana. Kumbe Upo?
Ooh my God! Faizaaaa...ooh umepotea sana hapa jamvini dada angu. Je kulikoni?
Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache wanachadema mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.
Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.
Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.
Pili napenda kutoa himizo kwa wanaccm na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.
Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na chadema tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua chadema 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.
Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.
Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.
Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.
Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.
Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.
Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.
CCM umoja ni ushindi.
Viva CCM
Katika mantiki ya kutafakari baada ya uchaguzi ana haki ya kuandika alichoandika. Ni jukumu letu sisi tumjibu ipasavyo.
Tatizo la CCM ni kulazimisha ushindi kwa lazima! Acheni wananchi wachague viongozi wanaridhika nao.
Napenda kuona upinzani ukikuwa Tz ila hiki chama chenye mashabiki wanaoacha kujibu hoja na badala yake kumtukana mtoa hoja kina rudisha nyuma jitihada za kuukuza upinzani.
Ajabu humu ndani kuna viongozi wakitaifa wa CDM na wenye heshima zao lakini wameshindwa kujaribu kuwaambia wanachama wao wajibu hoja badala ya matusi. Zitto, Slaa, Mbowe, na miamba mingine ya CDM mpo wapi na kwanini hamjaona haja ya kuzuia wanachama wenu wasitukane.
Upinzani ni utofauti wa sera kwa njia ya ushawishi. Lakini kilichopo JF ni hoja zinazojibiwa kwa kejeli au matusi. Inasikitisha.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/488642-juliana-shonza;anaota-ndoto-huku-amesimama.htmlNdugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache wanachadema mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.
Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.
Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.
Pili napenda kutoa himizo kwa wanaccm na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.
Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na chadema tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua chadema 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.
Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.
Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.
Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.
Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.
Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.
Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.
CCM umoja ni ushindi.
Viva CCM
ni kweli mkuu anamaanisha sasa mbuyu unarudi kuwa mchichaUmeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu utilization kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.
Kama vyama vyote vikiheshimu sanduku la kura...tutaenda mbele sana.