Hongera CCM

Hongera CCM

We si ndo ulisema CCM itashinda kwa kishindo Arusha..???

Dada Juliana Shonza siasa is all about kusoma alama za nyakati... Mwenzio Chris Lukosi kasema CDM hawatakiwi kushangilia ushinda wa Arusha kwa vile ni sawa na wanakwaya kumchagua padri wao... Nilimshangaa sana, na nikamuuliza kwa nini sasa walisimamisha wagome, huku wakijuwa Arusha ni kwaya inayochagua mapadri wao wanne..??

Nikionacho ni kwamba Arusha inawachanganya sana, sasa hivi mnahofia umeya maana Nape Nnauye naye kaanza kuzungumzia CDM na ndoto za kumuondoa meya Arusha

Hayo yote ni mahangaiko na kuweweseka na kushindwa uchaguzi.... MORE WILL COME... you just wait
 
Ok, katika Africa hakuna hata sehemu moja mvulana/mme akawa rafiki wa mke/msichana wa karibu zaidi wanakesha gest, wanalala wote kwenye gari, wanaiba wote bila kugusa chini ya 'Umblico kodi'. Siasa hizi za savimbi zitazalisha watoto wengi sana
 
Ukibeba mzoga unafuatwa na NZI tu.Hivi munazungumziaje huu mpasuko mkubwa na wa wazi uliopo ndani ya CCM yenu? Na Nini hatima ya CCM baada ya kikao munachoenda kupendekeza jina la mgombea wenu wa uraisi pale KIMWAGA soon?.CCM haitarudi salama kimwaga nyie misukule mukae mukijua na mukiamini hilo na hata mukipinga kwa sasa ila muda utawaambia na utawathibitishia hilo.Labda ni busara mutuambie nyie mutakuwa upande wa nani! Teh teh teeeeeee
 
Kamanda uliyepandikizwa na kushindwa Shonza,kwanza pole maana naona umechanganyikiwa mpaka unakilinganisha ccm na mchicha wakati lilishakuwa mbuyu siku nyingi na limezeeka karibia linajifia pole. Unajisikiaje kuzunguka na mume wa mtu,je unamtendea haki mkewe? Au mafundisho ya Mabibo yalishakutoka kabisa?!!!
 
Kwa nini ukiwa CCM uwezo wa kufikiria na kupambanua mambo unaporomoka gafla???? Duh kweli kazi ya kutetea mafisadi ni ngumu kweli.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
SHonza hayo madhara kutumikishwa na Nchemba siku si nyingi na wewe utaonekana mweu kama yeye,Hivi ni kweli hukumbuki CDM walipata kata ngapi kwenye uchaguzi na hawali na sasa wamefikisha jumla ya kata ngapi,huwezi CCM inakua na wakati iliwahi kuwa na vyote ngazi zote kwa asilimia 100,na sasa wanapoteza,Ni rahisi sana kuhituhumu CDM kwa sababu matumizi yake yako wazi,Kwa CCM ni ngumu sana kwani hakuna anajua walitumia nini kwa kwanza matumizi yenyewe ni makubwa(kwa ushaidi wa mazingira),lakini pia kila mmoja anatoa kivyake na kutokea kwenye vyanzo vyake
 
Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.

Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.

Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.

Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.

Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.

Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.

CCM umoja ni ushindi.

Viva CCM

Dada yetu, NIkushauri siku nyingine usiamke asubuhi kabla hata ya chai na kupitia walau kile ulichokuwa umerekodi (Data bank yako) na kuanza kudhihirisha udhaifu wako hadharani. Hii haikuaibishi wewe pekee bali na chama kongwe unachokiwakilisha.

Hebu angalia Takwimu ulizoweka za idadi ya kata zilizokuwa katika uchaguzi (RED). Je ndizo hizo pekee, au chama gani kingine kilishinda zingine ambazo hujaziweka hapo?. Umenitia aibu, kama ulitembelea kata zote kupigia upatu chama chako halafu hata haujui ulipita kata ngapi na matokeo yakoje. Ama kweli wewe ndio unachongo.

Pia tuwekee takwimu za mwaka 2010 za uchaguzi katika hizo kata tena kwa asilimia kwa kila chama ili ututhibitishie kuwa ccm imeongeza idadi ya kura.

Other wise umeandika ukiwa na hangover au umeamua kuendelea kupotosha wanajamii makusudi, Ikiwa hiyo ndio uhalisia wa kile unachokinadi kila kukicha. Ulitudanganya ukasema Misukule wa CDM wanajidanganya arusha kwa ushindi, leo unawapa hongera kwa kushinda halafu takwimu kitaifa umekosea kuzinukuu.

Jamani hili taifa majanga kila kona.
 
Juliana Shonza umeandika mambo mengi sana... Lakini unaonekana huna kumbukumbu, kwamba kwenye uchaguzi huu mdogo wa nchi nzima ccm walipoteza kata nne kwa chadema.
Pia huna kumbukumbu ccm walipata kura ngapi hapa Arusha.
Uchaguzi wa juzi ungetangazwa ingelikuwa aibu yenu.
Tena walioichagua chadema walikuwa watu walioletwa na ccm kwenye vituo vya kupiga kura, wakidhani wangeichagua ccm!

Chezea chadema weweeee!!!!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

yaani huyu dada ni bonge la "kishoia" nilikaona siku moja kwenye kampeni zao pale ilboru ka ovyoo sawa sawa na akili zake kabisa, huwa sipendi kukosoa but huyu dada nilivyomuangalia tu akipaza mayowe yake ya fitina nilikahurumia haswaaaa
 
Umeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.

atuambie pia kipofu gani aliona mawingu akadhani mbingu, kipofu anaona? hata matumizi ya lugha yako hujui, afu eti msomi!
 
Insha ndefu isiyokuwa na maana;
Analysis ni rahisi sana; hebu soma hapa chini usitusumbue na ngonjera, unajulikana kama mwanasiasa mchumia tumbo, relax endelea kuchuma, CDM iko kazini na huna lolote la maana la kutushauri.
Poor juliana unazungumzia kishindo gani?! tafuta mtu mweledi akufafanulie maana ya takwimu hizo hapo chini.

Arusha peke yake kwa kata:
Elerai: Kura halali 3828: CDM kura 2047 - 53%; CCM kura 1047 - 38%
THEMI: Kura halali 1307: CDM kura 674 - 52%; CCM kura 326 - 25%
KALOLENI: kura halali 2077: CDM kura 1470 - 71%; CCM kura 330 - 16%
KIMANDOLU: kura halali 3924: CDM kura 2761 - 70%; CCM kura 1163 - 30%

ARUSHA AGGREGATE:
Kura halali: 11136: CDM kura 6952 - 62%; CCM kura 3290 - 30%


Overall positions of the Parties before and After.
[TABLE="class: cms_table_grid"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]CCM
[/TD]
[TD]CHADEMA
[/TD]
[TD]CUF
[/TD]
[TD]TLP
[/TD]
[TD]TOTAL
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wards Before
[/TD]
[TD]19
[/TD]
[TD]5
[/TD]
[TD]1
[/TD]
[TD]1
[/TD]
[TD]26
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wards After
[/TD]
[TD]16
[/TD]
[TD]10
[/TD]
[TD][/TD]
[TD]0
[/TD]
[TD]26
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Gainers and Losers
[TABLE="class: cms_table_grid"]
[TR]
[TD]Losers (Former Seats lost)

[/TD]
[TD]Gainers (New seats gained)

[/TD]
[TD]Net Final position

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TLP – Lost 1 to CCM

[/TD]
[TD]CHADEMA – Gained 5 from CCM

[/TD]
[TD]CHADEMA GAINED 5

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CUF – Lost 1 to CCM

[/TD]
[TD]CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)

[/TD]
[TD]CCM LOST 3

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CCM – Lost 5 to CHADEMA

[/TD]
[TD]

[/TD]
[TD]TLP – LOST 1

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CHADEMA - none

[/TD]
[TD]

[/TD]
[TD]CUF – LOST 1

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Juliana Shonza, mimi nimeipenda sana timu yenu ya kampeni. Bila shaka mafanikio hayo unayoyasema yanaonesha kazi yenu nzuri.

Tafadhali mrudi kama mlivyokuwa wakati wa kampeni za kata ya Sombetini: yaani Mwigulu Nchemba, Mtela Mwampamba, wewe na yule anayeitwa Tesha.

Pia ajenda yenu ya kampeni iliwavutia sana wana Arusha, mje mmalizie kazi, itakuwa Septemba. Mtaigaragaza Chadema vibaya sana.

Hongera sana Shonza.
 
Wamerudi kuwapotezea watu muda humu mitandaoni baada ya kushindwa kwenye reality world.

Upuuzi tu.
 
Napenda kuona upinzani ukikuwa Tz ila hiki chama chenye mashabiki wanaoacha kujibu hoja na badala yake kumtukana mtoa hoja kina rudisha nyuma jitihada za kuukuza upinzani.

Ajabu humu ndani kuna viongozi wakitaifa wa CDM na wenye heshima zao lakini wameshindwa kujaribu kuwaambia wanachama wao wajibu hoja badala ya matusi. Zitto, Slaa, Mbowe, na miamba mingine ya CDM mpo wapi na kwanini hamjaona haja ya kuzuia wanachama wenu wasitukane.

Upinzani ni utofauti wa sera kwa njia ya ushawishi. Lakini kilichopo JF ni hoja zinazojibiwa kwa kejeli au matusi. Inasikitisha.
 
Pamoja na kwamba unatumika vibaya, leo umejitahidi kuandika. Lakini bado una endekeza ushabiki wa kijinga na wa kitoto sana. Jambo la maana ulilotakiwa kusema kama bosi wako Nape, ni kukubali kushindwa na kujitathimini upya ni wapi mmeteleza, na siyo kuleta vioja hapa na kebehi kibao!

cc Juliana Shonza "...CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita."
 
Insha ndefu isiyokuwa na maana;
Analysis ni rahisi sana; hebu soma hapa chini usitusumbue na ngonjera, unajulikana kama mwanasiasa mchumia tumbo, relax endelea kuchuma, CDM iko kazini na huna lolote la maana la kutushauri.

Positions of the Parties before and After.
[TABLE="class: cms_table_grid"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]CCM[/TD]
[TD]CHADEMA[/TD]
[TD]CUF[/TD]
[TD]TLP[/TD]
[TD]TOTAL[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wards Before[/TD]
[TD]19[/TD]
[TD]5[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]26[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wards After[/TD]
[TD]16[/TD]
[TD]10[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]26[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Gainers and Losers
[TABLE="class: cms_table_grid"]
[TR]
[TD]Losers (Former Seats lost)
[/TD]
[TD]Gainers (New seats gained)
[/TD]
[TD]Net Final position
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TLP – Lost 1 to CCM
[/TD]
[TD]CHADEMA – Gained 5 from CCM
[/TD]
[TD]CHADEMA GAINED 5
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CUF – Lost 1 to CCM
[/TD]
[TD]CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)
[/TD]
[TD]CCM LOST 3
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CCM – Lost 5 to CHADEMA
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]TLP – LOST 1
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CHADEMA - none
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]CUF – LOST 1
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Kimsingi CDM hawajapoteza bali wame-gain tano huku CCm wamepoteza tano na kugain 2, hence they have lost 3... mmepata hasara nyie akina Juliana Shonza
 
Binti Juliana Shonza najua hii thread umeianzisha kwa maelekezo ya bosi wako. Pamoja na hayo na kwa faida ya vilaza wa hesabu wenzako hapo lumumba ngoja nikusaidie kufanya hesabu ya darasa la kwanza. Kwa akili yako ndogo unashindwa kujua kwamba kama ccm ilishinda kata 16 na Chadema imeshinda kata 8 basi jumla ya kata zilizofanya uchaguzi ni 24 (16+8=24!hesabu ya darasa la kwanza hii)sasa sijui kata 2 umezipeleka wapi!!??

Jumla ya kata zilizopaswa kufanya uchaguzi tarehe 16/06/2013 ni kata 26.
Kata zilizofanya uchaguzi tarehe hiyo 16/06 zilikuwa kata 22 (baada ya policcm kulipua bomu mkutano wa Chadema na hivyo NEC kuahirisha uchaguzi katika kata 4 za Arusha).
Katika kata 22 zilizofanya uchaguzi awali ccm ilishinda kata 16 na Chadema ikashinda kata 6 (Chadema ilirudisha mikononi kata zake 2 na kuchukua 4 kutoka kwenu ccm).
Katika uchaguzi uliofanyika Arusha juzi tarehe 14/07/2014 Chadema imewagaragaza vibaya ccm kwa kujinyakulia kata zote 4.

Kwa ujumla msimamo wa ushindi wa kata kwa ujumla ni kwamba Chadema 10 ccm 16. Lakini pia kwa uwiano wa wingi wa kura Chadema ina 46% huku ccm ikiwa na 49%. Sasa nataka uanzie hapo uniambie kama ccm imeongeza idadi ya wapiga kura toka 2010 au imeporomoka? sitarajii kwamba mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dsm unaweza kushindwa hata kuunga unga hesabu ndogo kama hizi, unless uniambie hiyo degree uliipata kwa mlango wa dharura.

mods unganisha hii post pale juu ili kuondoa upotoshaji!
Cc. Invisible
 
Last edited by a moderator:
Ila ni aibu sana kwa CCM kama ndio wamekutuma wewe ambaye wanakuona ni msoni halafu ukatoa analysis ya kipumbavu kama hii ndio ccm wajue wameingizwa chaka na wahuni toka chadema. Kama kata nchi nzima zilikuwa 26 na wewe unasema ni 24 basi ccm wameumia. Yaani hata hujui chadema wamechukua ngapi basi ccm kweli wameumia kwa kukuona kichwa mpaka kudharau vijana wao wengine mliowakuta na nyinyi kuonekana ni vichwa kwakuwa mmetoka chadema. Hata ccm wanasikia aibu kwa wewe kuwaita mchicha wakati wenyewe wanajifanya ni mbuyu.
 
unatumika kwa maslahi ya WACHACHE, labda ulikuwa hauijui ccm vizuri, wanakutumia ,ukichokwa wana ku damp!!! utakosa pa kwenda, utakuwa nahali mbaya sana, CDM UTAONEKANA MSALITI, CCM UNAONEKANA YOU HAVE NO USE, TAFAKARI CHUKUA HATUA!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom