Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 34,637
- 37,959
Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.
Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.
Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.
Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.
Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.
Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.
CCM umoja ni ushindi.
Viva CCM
Juliana Shonza umeandika mambo mengi sana... Lakini unaonekana huna kumbukumbu, kwamba kwenye uchaguzi huu mdogo wa nchi nzima ccm walipoteza kata nne kwa chadema.
Pia huna kumbukumbu ccm walipata kura ngapi hapa Arusha.
Uchaguzi wa juzi ungetangazwa ingelikuwa aibu yenu.
Tena walioichagua chadema walikuwa watu walioletwa na ccm kwenye vituo vya kupiga kura, wakidhani wangeichagua ccm!
Chezea chadema weweeee!!!!
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Umeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.
Magwanda yanachojua ni mitusi tu. Si ilizaliwa Kariakoo mijitu mingine humu .
Insha ndefu isiyokuwa na maana;
Analysis ni rahisi sana; hebu soma hapa chini usitusumbue na ngonjera, unajulikana kama mwanasiasa mchumia tumbo, relax endelea kuchuma, CDM iko kazini na huna lolote la maana la kutushauri.
Positions of the Parties before and After.
[TABLE="class: cms_table_grid"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD]CCM[/TD]
[TD]CHADEMA[/TD]
[TD]CUF[/TD]
[TD]TLP[/TD]
[TD]TOTAL[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wards Before[/TD]
[TD]19[/TD]
[TD]5[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD]26[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wards After[/TD]
[TD]16[/TD]
[TD]10[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]0[/TD]
[TD]26[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Gainers and Losers
[TABLE="class: cms_table_grid"]
[TR]
[TD]Losers (Former Seats lost)
[/TD]
[TD]Gainers (New seats gained)
[/TD]
[TD]Net Final position
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]TLP Lost 1 to CCM
[/TD]
[TD]CHADEMA Gained 5 from CCM
[/TD]
[TD]CHADEMA GAINED 5
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CUF Lost 1 to CCM
[/TD]
[TD]CCM - Gained 2 (From TLP and CUF)
[/TD]
[TD]CCM LOST 3
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CCM Lost 5 to CHADEMA
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]TLP LOST 1
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CHADEMA - none
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]CUF LOST 1
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Binti Juliana Shonza najua hii thread umeianzisha kwa maelekezo ya bosi wako. Pamoja na hayo na kwa faida ya vilaza wa hesabu wenzako hapo lumumba ngoja nikusaidie kufanya hesabu ya darasa la kwanza. Kwa akili yako ndogo unashindwa kujua kwamba kama ccm ilishinda kata 16 na Chadema imeshinda kata 8 basi jumla ya kata zilizofanya uchaguzi ni 24 (16+8=24!hesabu ya darasa la kwanza hii)sasa sijui kata 2 umezipeleka wapi!!??
Jumla ya kata zilizopaswa kufanya uchaguzi tarehe 16/06/2013 ni kata 26.
Kata zilizofanya uchaguzi tarehe hiyo 16/06 zilikuwa kata 22 (baada ya policcm kulipua bomu mkutano wa Chadema na hivyo NEC kuahirisha uchaguzi katika kata 4 za Arusha).
Katika kata 22 zilizofanya uchaguzi awali ccm ilishinda kata 16 na Chadema ikashinda kata 6 (Chadema ilirudisha mikononi kata zake 2 na kuchukua 4 kutoka kwenu ccm).
Katika uchaguzi uliofanyika Arusha juzi tarehe 14/07/2014 Chadema imewagaragaza vibaya ccm kwa kujinyakulia kata zote 4.
Kwa ujumla msimamo wa ushindi wa kata kwa ujumla ni kwamba Chadema 10 ccm 16. Lakini pia kwa uwiano wa wingi wa kura Chadema ina 46% huku ccm ikiwa na 49%. Sasa nataka uanzie hapo uniambie kama ccm imeongeza idadi ya wapiga kura toka 2010 au imeporomoka? sitarajii kwamba mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dsm unaweza kushindwa hata kuunga unga hesabu ndogo kama hizi, unless uniambie hiyo degree uliipata kwa mlango wa dharura.