Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia haikufafanua waziwazi na kwa kina vitendo halisi walivyovifanya.Hii habari nimeiona inasambazwa na watu wa CHADEMA. Bado sijajua hii kampeni inalenga nini. Sababu nimefuatilia sipati chanzo sahihi.
Mtu inifafanulie. Je, nii propaganda za kisiasa au taarifa za kidini?
Sababu taarifa haijakamilika. Haijataja tukio limetokea lini na mahakama gani wala kosa walofanya la kubusu sijapata walihukumiwa kwa sheria gani. Bado nafuatilia hiki kisa.. Anayejua vizuri anielezee
Kubusiana tu ndio kufanya mapenzi!🙄Saudi Arabia katiba yao inasema ukifanya mapenzi msikitini adhabu yake ni kifo unakatwa kichwa, uki retard yaan ukihama Uislamu ukaenda Ukristu adhabu yake ni kifo unakatwa kichwa, na zingine zote zimeorodheshwa kosa na adhabu na hawana mswalie Mtume wao wanadeal na Allah tu
Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba, hata leo, tunaendelea kusambaza uongo kuhusu suala hili bila aibu yoyote.Huu ni ukweli wa tukio hilo
Watu wawili kutoka Bangladesh, Nazrul Islam na Sathi Akhtar.
Wote wawili walifanya kazi katika Kampuni ya Bin Laden na walikuwa wafanyakazi wa usafi katika Masjid al-Haram, Makka Mukarramah. Msichana aliishi katika Villa Batha Quraish, huku mvulana akiishi katika Villa Hayy al-Iskan.
Wakiwa kazini, uhusiano wa kimapenzi ulianza kati yao, na walifanya zinaa katika chumba kisicho na watu kilichokuwa kwenye ngazi kati ya milango/maget 85 na 87 (kuna milango/gates 357) ya Masjid al-Haram.
Nazrul Islam alikuwa amemwagiza mmoja wa marafiki zake wa Kihindi kusimama chini ya ngazi ili kulinda eneo hilo. Rafiki huyo alirekodi video ya tukio hilo. Baadaye, alipoonyesha nia ya kufanya zinaa na msichana huyo mwenyewe lakini akashindwa, au pale ambapo hakuna aliyekubali, aliiweka video hiyo hadharani.
Baada ya hapo, tukio hilo lilijulikana kwa umma.
Mamlaka za Saudi Arabia zilifanikiwa kuwakamata watu wote watatu. Kijana huyo wa Kihindi alihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani na bado yuko gerezani. Wale wengine wawili pia waliwekwa gerezani.
Nazrul Islam aliwasili Saudi Arabia akitokea Bangladesh kati ya tarehe 10 na 13 Novemba 2022. Alitenda kosa hili mwezi Mei 2023, baada ya hapo mamlaka za Saudi Arabia zikamkamata. Alibaki gerezani kuanzia Mei 2023 hadi Oktoba 2026. Mchakato wa kimahakama wa kesi hii ulidumu takribani miaka mitatu na nusu hadi minne.
Katika kipindi hicho, ni wajibu wa serikali ya Saudi Arabia kumjulisha mdhamini wake (sponsor) na kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi. Si wajibu wao kuwajulisha watu kutoka nchi nyingine kuhusu jambo hilo.
Watu wengi wanadai kwamba wawili hao walikuwa wamekwenda kufanya Umra na kwamba walibusiana tu huko. Habari hizo zote ni za uongo na zimebuniwa kabisa.
Ni kweli kwamba wote wawili hawakuwa wameoa wala kuolewa. Lakini swali hapa ni hili: ikiwa hawakuwa wameoa wala kuolewa, kwa nini walihukumiwa adhabu ya kifo?
Je, unajua sababu?
Kwa sababu eneo husika ni Masjid al-Haram.(Msikiti mtakatifu)
Fikiria eneo la kijeshi lenye usiri mkubwa au eneo la mpaka wa nchi huru. Ukiingia bila ruhusa katika shamba la kawaida la mtu binafsi, unaweza kuonywa au kutozwa faini.
Lakini ukipuuza maonyo ya kiusalama na kuingia katika eneo la siri la kijeshi lililozuiwa, ambako bango linaonyesha wazi kwamba matumizi ya nguvu ya kuua yameruhusiwa, walinzi watakupiga risasi kwa nia ya kukuua.
Hupigiwi risasi kwa sababu kutembea ni kosa. Unakabiliwa na nguvu ya kuua kwa sababu umevunja kwa makusudi mpaka wa mwisho kabisa uliowekwa na dola. Uadilifu wa mpaka huo ni muhimu zaidi kuliko maisha yako.
Hii ndiyo hali halisi ya kilichotokea hapa. Hivi ndivyo Masjid Haram (Takatifu) ya Makka ilivyo.
Si mji tu.
Nazungumza kwa uzoefu wa kupita eneo hilo na kukaa zaidi ya mwezi kwa ibada ya hijja
Ni patakatifu zaidi duniani kwa waIslam
Ni eneo takatifu la Mwenyezi Mungu lenye mipaka mikali sana. Unaweza kuwinda mnyama sehemu nyingine yoyote duniani, lakini ndani ya Haram, huruhusiwi hata kuelekeza kidole kwa ndege ili kumtisha.
Unaweza kusafisha msitu katika nchi yako, lakini ndani ya Haramain (maeneo 2 takatifu, Makkah na Madina) huruhusiwi hata kung'oa jani au mmea. Huruhusiwi kubeba silaha. Huruhusiwi kuokota kitu kilichopotea kilichopo sakafuni isipokuwa unatafuta kwa dhati mmiliki wake ili umrudishie.
Ukiwa ndani ya vazi la ihram hutakiwi hata kukata kucha au kunyoa nywele
Hupaswi kumuingilia hata mkeo wa halali mpaka mtakapotoka ndani ya Ihram (hilo vazi jeupe kwa wanaume na wanawake siyo lazima wao nyeupe, wanavaa mavazi yao ya stara kawaida) baada ya kutekeleza ibada mahsusi kama ni umra au hijja
Ukikiuka masharti unalipa fidia ya kufunga siku 3 au kutoa kafara ya kuchinja au kulisha maskini na hata kurudia ibada ya hijja au umra
Ni msikiti pekee ambapo wanawake na wanaume wanachanganyika wakati wa ibada ya tawaf (kuzunguka kaaba) na kufanya ibada zote za hijja au umra isipokuwa wakati wa swala lazima utaratibu wa kutenganisha kufuatwa
Pia kuna undani zaidi wa kiteolojia katika jambo hili.
Makkah ni eneo linalokuza uzito wa matendo ya kiroho. Tunafundishwa kwamba swala moja ndani ya Masjid Haram ina thamani ya swala 100,000 zinazotekelezwa mahali pengine popote. Lakini kipimo hicho hakipimi matendo mema pekee. Unapoleta dhambi kubwa ndani kabisa ya patakatifu hapo, uzito wa dhambi hiyo pia huongezeka kwa kiwango hicho hicho.
(Na yeyote atakayekusudia kufanya uovu humo kwa dhuluma, tutamuonjesha adhabu chungu.”
— Qur’an 22:25)
Jambo hili halihusu tu adhabu ya zinaa; (hakuna adhabu ya aina hiyo kwenye Uislam, walipaswa kuchapwa kwa kuwa hawajaoana) bali mhusika pia alikiuka utakatifu na heshima ya Masjid al-Haram.
Kwa sababu hiyo hiyo, kwa lengo la kutoa adhabu itakayokuwa mfano kwa wengine, majaji wakuu wa Mahakama ya Juu waliona adhabu ya kifo kuwa inafaa kama njia ya kuzuia wengine wasitende kosa kama hilo, na wakatoa hukumu hiyo hiyo. Adhabu hii inalingana na Qur’an na Sunnah lakini wameongezea maamuzi ya kimamlaka ya serikali yao.
Mahakimu wanatumia Ta’zir , mfumo unaowaruhusu mahakimu kutoa adhabu kwa hiari yao kwa mujibu wa sheria ya Sharia ya Kiislamu
Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba, hata leo, tunaendelea kusambaza uongo kuhusu suala hili bila aibu yoyote.
Kila nchi na kila sehemu ina sheria na utaratibu wake
Sahihi kabisaJambo la kushangaza zaidi ni kwamba, hata leo, tunaendelea kusambaza uongo kuhusu suala hili bila aibu yoyote.
Kila nchi na kila sehemu ina sheria na utaratibu wake
Waliwashtaki kwa kufanya mapenzi msikitini, nikajua wamedinyana kumbe wamekiss forehead tu?? Sharia zipitiwe upyaSi kila safari ya maisha huanza kwa furaha na kumalizika kwa furaha.
Kwa wanandoa wawili kutoka Bangladesh, safari yao kuelekea Makka ilipaswa kuwa mwanzo wa kumbukumbu nzuri ya maisha yao ya ndoa.
Walikuwa wameanza ukurasa mpya wa maisha, wakielekea katika mji mtakatifu wa Makka kwa matumaini na furaha lakini mambo yalibadilika ghafla.
Wakiwa huko, Nazrul Islam Abdul Basir na Siti Akhtar walikumbwa na tukio lililobadilisha kabisa hatima yao.
Ndani ya msikiti huko Makka, Nazrul alimbusu mkewe Siti kwenye paji la uso, busu hilo lilikuwa ishara ya upendo na shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya mwanamke aliyekuwa amekuwa sehemu ya maisha yake.
Badala ya wakati huo kuwa kumbukumbu ya upendo, uliishia kuwa mwanzo wa matatizo makubwa, wawili hao walikamatwa, wakafikishwa mbele ya vyombo vya sheria na baadaye kuhukumiwa kifo kwa kosa lililohusishwa na kitendo cha maadili yasiyofaa ndani ya msikiti.
Hatimaye, hukumu hiyo ilitekelezwa safari iliyokuwa imeanza kwa matumaini ya wanandoa wapya ikageuka kuwa safari ya mwisho ya maisha yao.
Miili yao ilirejeshwa Bangladesh ikiwa katika majeneza mawili tofauti, huku familia zao zikikabiliwa na maumivu makubwa ya kumpoteza watu wao wa karibu katika mazingira ambayo ni vigumu kuyasahau.
Wakati mwingine maisha yanaweza kubadilika ndani ya muda mfupi sana, safari iliyokuwa ya fungate, ikaishia kuwa safari ya mwisho.
Somo ambalo nimejifunza kwenye hili jambo ni kwamba usiende kwenye nchi ambayo haujui mila, desturi na Utamaduni wake.View attachment 3694831
Ongeza nyingine 6Mshana mshana mshana nimekuita mara tatu tupe chanzo cha habari hii la sivyo uombe radhi kwa habari za kuokoteza kama hizi
JamiiCheck
Eneo la mungu lipo Saudi..?Ni eneo takatifu la Mwenyezi Mungu
UnazinguaHii habari nimeiona inasambazwa na watu wa CHADEMA. Bado sijajua hii kampeni inalenga nini. Sababu nimefuatilia sipati chanzo sahihi.
Mtu inifafanulie. Je, nii propaganda za kisiasa au taarifa za kidini?
Sababu taarifa haijakamilika. Haijataja tukio limetokea lini na mahakama gani wala kosa walofanya la kubusu sijapata walihukumiwa kwa sheria gani. Bado nafuatilia hiki kisa.. Anayejua vizuri anielezee
Chuki zako zitakufanyisha wengine tukuone hopeless we mzeeOngeza nyingine 6
Kwamba habari hii imesambazwa na watu wa CHADEMA?Hiki ni kiwango cha chini cha kufikiriaHii habari nimeiona inasambazwa na watu wa CHADEMA. Bado sijajua hii kampeni inalenga nini. Sababu nimefuatilia sipati chanzo sahihi.
Mtu inifafanulie. Je, nii propaganda za kisiasa au taarifa za kidini?
Sababu taarifa haijakamilika. Haijataja tukio limetokea lini na mahakama gani wala kosa walofanya la kubusu sijapata walihukumiwa kwa sheria gani. Bado nafuatilia hiki kisa.. Anayejua vizuri anielezee
Hata wewe ukileta habari za kuokoteza bila kuleta chanzo nakuzingua tu. Mimi siko interested na kusambaza chuki za kidini. Au kushabikia vitu vinavyofanya dini moja sio sahihi. Dhumu la kusambaza hii taarifa ninkiwaattack Waislam na kueneza Chuki.Unazingua
Madai yako yamefanya niingie CHATGPT. Naona mambo mengi umeongeza chumvi au una taarifa za mitaani.Saudi Arabia katiba yao inasema ukifanya mapenzi msikitini adhabu yake ni kifo unakatwa kichwa, uki retard yaan ukihama Uislamu ukaenda Ukristu adhabu yake ni kifo unakatwa kichwa, na zingine zote zimeorodheshwa kosa na adhabu na hawana mswalie Mtume wao wanadeal na Allah tu