Home of AC Milan, Official Thread

shukrani za pekee ziende kwa Mark Van Bommel aliyepoteza mipira miwili tu ktk second half...
tena mipira hiyo yote ilikuwa ya juu
 
brescia 1-1 Inter.
18 inter goal...Eto'o
85 Brescia goal...Calaciolo
90 Brescia miss the Penart...Calaciolo

Red Card:
Inter - Ivan Romero Coldoba
Brescia - calaciolo
 
kaka vipi...? vijana waliwashupalia.. mkachomoa dakika za mwisho.. , kweli mpira unadunda..
 
baada ya kumpa kipigo cha mbwa koko jirani, mdogo wetu, mtani wetu yaani klabu ya Inter...Jumapili hii tunaingia dimbani kupambana na timu ya Fiorentina.

Itakumbukwa kuwa Fiorentina ktk mechi zao kumi zilizopita dhidi yetu hawajashinda mechi hata moja, ila wamepata droo mechi 4 na kuchapwa mechi 6.

Forza Milan
 
katika mechi zilizofanyika #umamosi yaani jana klabu ya Inter imeweza kuifunga klabu ya Chievo magoli 2-0....

Huku AS Roma wakiwafunga vijana wabishi wa Udinese kwa jumla ya magoli 2-1.
Magoli ya AS Roma yalifungwa na Sharp Shutter Francesco Totti, na goli pekee ya Udinese lilifungwa na Antonio Di Natale.
 
katika mechi zilizofanyika #umamosi yaani jana klabu ya Inter imeweza kuifunga klabu ya Chievo magoli 2-0....

Huku AS Roma wakiwafunga vijana wabishi wa Udinese kwa jumla ya magoli 2-1.
Magoli ya AS Roma yalifungwa na Sharp Shutter Francesco Totti, na goli pekee ya Udinese lilifungwa na Antonio Di Natale.
Milan wasipochukua SCUDETO msimu huu inabidi wachezaji wapewe bakora
 
ktk mchezo ulioisha hv punde matokeo ni kuwa AC Milan wakiwa kwa Fiorentina wameweza kuifunga klabu hiyo kwa jumla ya goli 2-1.

Magoli ya Rossoneli yaliwekwa kimiani na Clarence Seedorf na Alesandro Pato na lile moja la Viola liliwekwa kimiani na Vargas.

Wakati huo huo mshambuliaji aliyeko Milan kwa Mkopo Zlatan Ibrahimovic alipewa kadi nyekundu ktk dakika za mwisho za mchezo.

Leo ilikuwa mechi ya kwanza ya Ibrahimovic kurudi uwanjani baada ya kupewa kadi nyekundu mechi 3 zilizopita.

Forza Milan
 
mapema jumamosi timu ya Soka ya Parlemo iliweza kupata ushindi dhidi ya AS Roma na kuwagalagaza kwa jumla ya magoli 3-2 ktk uwanja wa Olimpico wa AS Roma.
 
nayo Parma ikawabamiza Mabingwa watetezi wa Scudeto kwa jumla ya Goli 2-0 na kupelekea ndoto za Inter kutete ubingwa kuyayuka kama harufu yq ushuzi...
 
na ktk Barabara ya Turatti inayoingia ktk uwanja wa Sansiro palikuwa na mamia ya washabiki waliokuwa wamejipanga na mabango makuubwa yenye maandishi ya ya kumkaribisha tena uwanjani midfield Maestro Andreas Pirlo ambaye aliingia uwanjani hii leo ktk mechi dhidi ya Sampdoria na kupelekea AC Milan kupata ushindi wa magoli 3-0.

Magoli ya Milan yalifungwa na Simba dume Clarence Seedorf, Antonio Casano na Robinho.

Ktk mechi hiyo Milan tuliwakilishwa na

1. Abiati
2. Abate
3. Zambrotta
4. Yepes
5. Silva
6. Van Bommel
7. Gattuso
8. Boateng
9. Pato
10. Robinho
11. Seedorf

Forza Milan
 
Tofauti point nane kileleni.
Klabu ya soka ya AC Milan wameweza kuwavurumishia mbali Brescia na kuwakandamiza kwa jumla ya goli 1-0 goli lililofungwa na Mshambuliaji Robinho kunako dakika ya 82 ya mchezo.

Mechi nyingine zilizochezwa Mapema tulishuhudia AS Roma wakimpiga Chievo goli 1-0.

Inter wakimchapa Lazio kwa magoli 2-1.

Napoli wakikalia kifuu na kukubali kupokea kichapo cha goli 2-1 dhidi ya Parlemo.

Marehemu Juve wakasuluhu 2-2.
 
Klabu ya AC Milan imetwaa ubingwa wa ligi ya italia maarufu kama scudeto baada ya kupata suluhu ktk mechi dhidi ya AS Roma iliyopigwa katika dimba la Olimpico mjini Rome.

Kwa matokeo hayo basi naomba kwa heshima na taadhima nifungue rasmi chupa hii ya Matt Daniel na kuanza kugida na kuyabanika maini yangu mwenyewe kwa furaha.
 
Ruksa imetolewa gida tu mkuu ukimaliza nitakupa ofa nyingine ya Bacardi lichupa lizima!
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom