Home of AC Milan, Official Thread

hongeri kwa jukwaa lenu jipya.lipakeni rangi basi wakuu lol.

Wenger hii ni nyumba ya AC Milan na si jukwaa.
Majukwaa yapo ukicheki vizuri utayakuta yameandikwa ''HAPA JAMANI TUTAKUWA TUNAJADILI TIMU YETU. NA PIA TUNAWAKARIBISHA WATU WOTE KUCHANGIA''.

Lakini hapa ukija utakaribishwa na historia, mafanikio, uongozi na yaliyomo.

Karibu sana ndugu yangu ktk Nyumba ya ACMilan.
 
Leo huyu Msierra Leone Sidney Strasser ametutoa kwa goli lake ktk ushindi wa 1-0 dhidi ya Cagliari. Goli hili limepikwa na supa straika Antonio Cassano. Sasa tunapeta ktk msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi 5.

Sforza Rossoneri

Napoli hoi, Lazio hoi, Juve ndo kabsaaaaa...
 
Napoli hoi, Lazio hoi, Juve ndo kabsaaaaa...
Nimeangalia gemu ya Juve, dk ya 17 Melo akampiga mtu kiatu cha uso baada ya kuchezewa rafu. Refa akampa red card hapo ndio goli zikaanza kumiminika..jamaa huenda anavuta bange si bure yule hakyanani. Mdogo Giovinco akapiga bao mbili safi na kuwasuta la Vecchia Signora kwa kumuuza.
 
Milan kama Milan ndio timu inayoongoza kwa kuchezewa na nyota mahiri Duniani...
 
pia Milan ndio timu ya kwanza kuchukua Champions League back to back 1989 na mwaka 1990.

Ikumbukwe kuwa ktk msimu wa mwaka 1989 Milan walitoa wachezaji watatu waliogombea na kushinda nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu ya mwanasoka Bora wa Dunia.
1. Marco Van Barsten
2. Franco Barresi
3. Frank Riijkhard.

Hilo ndio Milan dume.
 
Da hawa watoto wa Udinese ni balaa, wamebahatika kuchukua kapoint kamoja bana kutoka Stadio Giussepe Meanza. Sare ya 4-4 ni ushindi kwao. Mzee Allegri inabidi aimarishe mabeki maana tumepigwa kaunta attack kama tumesimama. Seedrof sasa umri umefikia tamati na amekuwa slow kama konokono. Kutokana na uzembe wake tukawa nyuma 3-1. Bahati Pato na Ibra wameonesha juhudi binafsi na huyu dogo Strasser anakuja vizuri.
 
Dah mbadala wa Nesta anahitajika haraka sana.
Coz huyu bwana ni muhimu sana kwetu.

Kuhusu Swala la Seedorf ni kweli jamaa ni slow sana, na kama tungekuwapo na kina Boateng, Pirlo na Flamini basi game ingekuwa nyepesi sana.

All in all Milan still tuko on top...
 
@ Companero...
Leo namuhofia sana jamaa.
Ni kichwa cha ukweli.
Huyu mtu anaona mbali sana.
Binafsi naamini Ligi bado kuisha ila moto utawaka
 
33yrs Mark Van Bomel anahitajika na klabu ya AC Milan ili akaungane na nguli wenzie na kuhakikisha Chama linasonga...
 
ilitugharimu dakika takriban 90+4 kuibuka na ushindi dhidi ya Cecena.
Goli la kwanza la Dakika 45 walijifunga wenyewe kabla ya Zlatan Ibracadabra kupiga msumali wa mwisho dakika ya 90+2...


Ktk uwanja wa nyumbani wa Udinese jirani zetu Inter wakala za Chembe baada ya kupokea kipigo cha goli 3-1 toka kwa sungusungu hawa wa Udinese waliokuwa wanaongozwa na Di Natale.

Juve wakasuluhu 0-0
Lazio akapigwa 3-1
Napoli akashinda 2-0


Wakati huohuo klabu ya AC Milan imemsajiri beki mahiri wa kushoto toka shule ya vipaji yaani klabu ya Ajax Amsterdam.
Beki huyo mwenye miaka 25 anauwezo wa kucheza winga ya kushoto na pia ana uwezo wa kukava vizuri mbavu ya kushoto.
 
Kutoka kwa Van Barsten, Gullit mpka Rhiijkard, tukaja kwa Kluivert na Edgar Davids, kisha kwa Seedorf, Stam na sasa ni zamu ya Holding Midfield...


kiungo mkabaji na mwenye uwezo wa kumiliki Mpira na kutoa pasi zenye Upako na anayeaminika kupiga mashuti Mark Van Bommel amewasiri klabuni Hapa na hivi punde ametoka kupewa jezi namba 4 na ametambulishwa rasmi kuwa ni mpambanaji mpya wa klabu ya AC Milan.

Forza Milan
 
sampdoria 1-2 Milan
Thanx to Alesandro Pato.
Hapo jana klabu yenye mafanikop zaidi kuliko yoyote hapa ulimwenguni yaani AC Milan wameweza kutinga nusu fainali ya kombe la Copa Italia baada ya kuwachapa Sampdoria magoli 2-1 magoli yaliyowekwa kimiani ktk kipindi cha kwanza na Mbrazil Pato.

Milan pia ilipata kuwatambulisha na kuwachezesha viungo wake wapya urby Emanuelson na Kamanda Midfield General Mark Van Bommel ambao walicheza kwa dakika zoote 90.

dimba lilikamata na Mark Van Bommel sambamba na Thiago Silva.
Van Bommel ambaye amesajiliwa juzi hakuweza kupata muda wa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake lakini alipojumuisha nao hiyo jana walionekana kama vile walikuwa woote kwa misimu 10 iliyopita.

Forza Milan
 
Kaka GC, umeona mambo ya van Bommel? mechi ya pili tayari keshakula red card moja. Huo ndio mwendo wa van Bommel, mechi 2 red 1 kudadeki..sijui kaa tutafika kwa mwendo huo. Bahati tumeshinda 2-0 dhidi ya Catania.
 
Rafu ni sifa ya kiungo mkabaji kama yeye...
Amedhihirisha kuwa yeye ni wa aina gani...
 
tumepata Point moja usiku huu...
Mechi imekwisha kwa Goalless.
Milan 0-0 Lazio
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom