Homa ya Dengue Yaua Daktari Bingwa Dar

Homa ya Dengue Yaua Daktari Bingwa Dar

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

Sunday, 11 May 2014 10:51


Breaking NEWS:


Dar es Salaam, Tanzania. Daktari bingwa wa magonjwa ya akili katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam, Dk Gelbert Buberwa amefariki dunia hivi punde baada ya kuugua homa ya Dengue.


Ugonjwa wa homa ya Dengue, umevamia Jiji la Dar es Salaam kwa kasi na kusababisha baadhi ya watu kulazwa hospitalini.

Mbali na ugonjwa huo kumshambulia Dk Buberwa, vilevile msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ( Ray C)
naye aliugua na kulazwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Baada ya siku chache kupita, msanii wa Bongo Movie Dk Cheni aliugua ugonjwa huo na kulazwa katika Hospitali ya Burhan jijini Dar es Salaam.


Dalili ya Homa ya Dengue
Madaktari wanasema kuwa dalili za homa ya Dengue ni mgonjwa kuhisi kuchoka sana, homa kupungukiwa damu, na kuhisi maumivu
mwilini.


Madaktari wamesema kuwa ugonjwa huo hauna matibabu maalumu bali mgonjwa akiugua anapaswa kupelekwa hospitali mapema kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
===========================================================


daktarii.jpg

Waombolezaji wakimfariji Leticia Filbert, mke wa daktari bingwa wa Hospitali ya Temeke, marehemu Dk Gilbert Buberwa nyumbani kwake Kinyerezi, Dar es Salam jana
Dar es Salaam. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili nchini, Gilbert Buberwa amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa dengue.

Kifo cha Dk Buberwa kinafanya idadi ya watumishi wa afya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo kufikia wawili baada ya muuguzi Hamida Likoti kufariki dunia wiki iliyopita.

Ugonjwa huo uliolipuka mkoani Dar es Salaam, umezua taharuki kwa wakazi wake kwa sababu hauna tiba na unasababishwa na mbu, Aedes Egyptae, anayeuma mchana na anayeweza kuzaliana katika majisafi yaliyotuama.

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia alisema jana kuwa Dk Buberwa alifariki dunia saa saba usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Dk Buberwa alianza kuumwa ugonjwa huo akiwa kazini katika Hospitali ya Temeke na kulazwa na hali yake ilipobadilika, alihamishiwa MNH kwa matibabu zaidi.

"Kadiri siku zilivyozidi kwenda alibainika kwamba viungo vyake muhimu, yaani ini na figo vimeharibika, hivyo alisafishwa figo huku akiwa amelezwa Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU).

Dk Saidia alikumbusha kuwa virusi vya dengue havina tiba isipokuwa dalili zake ambazo ni homa, kuumwa kichwa na viungo vya mwili – ndizo zenye tiba.

Dk Buberwa alianza kuugua Mei 3, mwaka huu na siku iliyofuata alipelekwa hospitali na mkewe ambako alilazwa ili kupata uangalizi wa karibu wa madaktari wenzake.

Kaka wa marehemu, Wakili Nickson Ludovick alisema: "Tunasubiri ndugu kutoka Bukoba na Musoma kwa mazishi yatakayofanyika hapa Dar es Salaam katika makaburi ya Kinyerezi keshokutwa."

Madaktari, wauguzi walazwa

Dk Malima alisema hadi jana, wafanyakazi tisa wa Hospitali ya Temeke walikuwa wamelazwa kutokana na homa hiyo.

Alisema wafanyakazi hao ni madaktari watano, wauguzi watatu na mtaalamu mmoja wa maabara. "Kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita tumepokea wagonjwa wa dengue waliothibitika 15," alieleza Dk Malima

Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Temeke, Shamim Kanju alisema wafanyakazi wanaendelea kuambukizwa kutokana na kuwa katika mazingira hatarishi kwa muda mrefu. Mtaalamu wa maabara, Eliud Kishebuka ambaye ni mmoja wa wagonjwa waliothibitika kuwa na homa hiyo, alisema alianza kujisikia mgonjwa juzi asubuhi, hivyo akaamua kwenda kufanya vipimo Mwananyamala ambavyo vilithibitisha kuwa ameambukizwa.

Utambuzi wa ugonjwa

Dk Saidia alisema wataalamu wa vipimo hawajaelekezwa ipasavyo namna ya kutambua mgonjwa huo.

Alisema endapo mgonjwa atachukuliwa kipimo kamili cha damu (full blood picture) na kuona kupungua kwa chembehai mgando nyeupe za damu, wajue kwamba hicho ni kiashiria kikuu cha ugonjwa wa dengue.

Mwandishi The Citizen augua

Mwandishi wa Gazeti la The Citizen, Mkinga Mkinga ni miongoni mwa watu walioambukizwa ugonjwa huo.

Mkinga alisema jana kwamba alianza kuhisi homa na maumivu makali ya kichwa tangu Jumanne iliyopita na alipokwenda hospitali ilibainika kuwa ni homa ya dengue.

"Nilipewa dawa za kutuliza pamoja na kunywa maji mengi, kwa sasa niko nyumbani kwangu ninaendelea nazo lakini kichwa bado kinauma na homa inakuwa kama ya vipindi," alisema.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema wagonjwa wa dengue wameongezea na kufikia 399 hadi jana.

Ofisa mwandamizi wa wizara hiyo, Dk Janeth Bugamba alisema jana kuwa kuna uwezekano wa idadi ya wagonjwa kuwa kubwa zaidi kwa kuwa hakuwa amepata takwimu kutoka hospitali zote.

Msemaji wa MNH , Aminiel Aligaesha alisema wagonjwa wa dengue wanaongezeka kwa kasi katika hospitali hiyo.

Alisema hadi kufikia jana, wagonjwa 65 walifika katika hospitali hiyo na kutibiwa kisha kurejea nyumbani na wengi ni kutoka maeneo ya jirani na hospitali hiyo wakiwamo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili (Muhas) ambao hata hivyo, hakutaja idadi yao.
Chanzo:Mwananchi
 
Mi nilijua madaktari bingwa wa akili wapo Milembe tu ...RIP dokta
 
Dah, hali ishakuwa tete sasa, ugonjwa hauchagui huu!!
 
na hii mvua ndo mazalia yanakuwa Mengi,eeh Mungu utuepushe
 
Aisee hii ni hatari sana jamani!
Chonde chonde walevi na watu wengine msiende kwenye sehemu za starehe wala kukaa sehemu zilizogubikwa na vivuli vikubwa vya miti make mbu wa waenezao dengue wanapendelea kukaa kwenye vivuli na sehemu tulivu za miti na wanang'ata mchana na usiku.
 
Serikali inyunyuzie dawa dsm maana na hii mvua si rahisi kabisa watu katika makazi kuthibiti hawa mbu. Mungu tuonee huruma.
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Tayari tunaambiwa wameishiwa test kit za kupimia ugonjwa huu
huku Tanga ilibidi wazilete tangu wiki iliyopita lakini kimya kwani tayari
ugonjwa upo horohoro border upande wa Mombasa, hivyo tupo katikati
 
Dunia si Mahala Salama kwasasa ..

Ukimwi, Saratani, Kisukari, Malaria. Pressure sasa tena Dengue..

Mungu tunusuru na haya magonjwa ..
 
wacha tu uendelee kuua , maana hamjataka kuambiana ukweli .
google ugonjwa huu unasababishwa na nini, umetoka wapi?
 
Propaganda za ccm kuwaondoa watu kwenye kufuatilia maswala muhimu. Dengue its fake fuatilieni mtajua matatizo ya wanaokufa. There is nothing like dengue. Ccm wanaleta issue za mzee mwasapile.
 
Unasababishwa na nini huu ugonjwa

[TABLE="width: 601"]
[TR]
[TD="width: 573, bgcolor: #FFDAC1, colspan: 2"]
​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 573, colspan: 2"]
​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 573, colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 573, colspan: 2"][h=2]Introduction to Chikungunya[/h]Chikungunya is a viral disease transmitted to humans by the bite of infected Aedes Aegypti mosquitoes. Chikungunya virus (CHIKV) is a member of the genus Alphavirus, in the family Togaviridae. CHIKV was first isolated from the blood of a febrile patient in Tanzania in 1953, and has since been identified repeatedly in west, central and southern Africa and many areas of Asia, and has been cited as the cause of numerous human epidemics in those areas since that time. The virus circulates throughout much of Africa, with transmission thought to occur mainly between mosquitoes and monkeys.
[h=2]Symptoms of Chikungunya[/h][h=2][/h]Symptoms of Chikungunya includes debilitating arthralgia (joint pain), swelling of joints, stiffness of joints, myalgia (muscular pain), headache, fatigue (weakness), nausea, vomiting and rash and fever.
The incubation period (time from infection to illness) can be 2-12 days, but is usually 3-7 days. "Silent" CHIKV infections (infections without illness) do occur; but how commonly this happens is not yet known.
Acute chikungunya fever typically lasts a few days to a couple of weeks, but some patients have prolonged fatigue lasting several weeks. Additionally, some patients have reported incapacitating joint pain, or arthritis which may last for weeks or months. No deaths, neuro-invasive cases, or hemorrhagic cases related to CHIKV infection have been conclusively documented in the scientific literature.
CHIKV infection (whether clinical or silent) is thought to confer life-long immunity.
[h=2]Spread of Chikungunya[/h]CHIKV is spread by the bite of an infected mosquito. Mosquitoes become infected when they feed on a person infected with CHIKV. Monkeys, and possibly other wild animals, may also serve as reservoirs of the virus. Infected mosquitoes can then spread the virus to other humans when they bite. Aedes aegypti (the yellow fever mosquito), a household container breeder and aggressive daytime biter which is attracted to humans, is the primary vector of CHIKV to humans. Aedes albopictus (the Asian tiger mosquito) may also play a role in human transmission in Asia, and various forest-dwelling mosquito species in Africa have been found to be infected with the virus.
[h=2]Treatment of Chikungunya[/h][h=2][/h]Effective treatment for Chikungunya is available in homeopathy.
Homeopathy has very effective treatment for Chikungunya. After diagnosis of Chikungunya, homeopathic treatment should be started as early as possible. Homeopathic treatment can also be given along with conventional treatment (allopathy) if desired. Conventional treatment consists of only symptomatic treatment of fever, stiffness, joint pain etc. of this viral illness, whereas homeopathic medicines give better and comparatively long lasting relief from the disease. Effective remedy can be chosen by a homeopathic doctor according to clinical picture of that particular case. Homeopathy works effectively in all viral diseases. Homeopathic pills are simply chewed (dissolved) on tongue and are sweet in taste. Homeopathic medicines do not cause gastric irritation, are safe on kidneys and liver even when taken for long duration.
In epidemics, prevention of Chikungunya can be achieved by administering Homeopathic "Genus Epidemicus". Genus Epidemicus is a homeopathic remedy that is chosen as a preventive remedy for that particular epidemic in that particular locality. Homeopathic medicines are equally effective for post-chikungunya complaints like weakness, stiffness in joints, muscles pain etc. Infected persons should be protected from further mosquito exposure (staying indoors and/or under a mosquito net during the first few days of illness) so that they can't contribute to the transmission cycle.
Know more about Curative and Preventive Homeopathy in Chikungunya.
[h=2]Prevention of Chikungunya[/h]The best way to avoid CHIKV infection is to prevent mosquito bites. In addition we strongly recommend to have "Homeopathic Genus Epidemicus"for double protection.
Prevention tips:
• Use mosquito repellent on exposed skin.
• Wear long sleeves shirts and pants.
• Have secure screens on windows and doors to keep mosquitoes out.
• Get rid of mosquito breeding sites by emptying standing water from flower pots, buckets and barrels. Change the water in pet dishes and replace the water in bird baths weekly. Drill holes in tire swings so water drains out.
• Additionally, a person with chikungunya fever should limit their exposure to mosquito bites in order to avoid further spreading the infection. The person should stay indoors or under a mosquito net.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Back
Top Bottom