Homa ya Dengue Yaua Daktari Bingwa Dar

Homa ya Dengue Yaua Daktari Bingwa Dar

test kit zimeisha ila pesa za kuongezea posho wabunge na kulipa bunge la mipasho zipo

Tunaongozwa na maajenti wa shetani ambao furaha yao ni kuona watu wanakufa. Pamoja na test kits kuisha hatuna mashine ya kunyunyiza dawa kwa kutumia ndege, wanasema ipo moja tu manispaa ya Ilala nayo ni ya kwenye gari sasa mabondeni itafikaje?
Mnyika alisema vema siku ile bungeni, tumefika hapa kwa upuuzi wa CCM ambao fedha ya ufisadi haukosi, lakini ya kutibu watu haipo kabisa.
 
Hili suala Wizara ya Afya ili-address seriously baadala ya magazeti ya Udaku kuachwa pekee katika kazi ya kutoa tahadhari

Ben hii kitu ni serious sana, ila wizara yetu ya afya ni ya ajabu sana!
Wana JF, huu ugonjwa hauna tiba kamili na nafikir ndio huo huo mdau mmoja ameuelezea ka chiku... sababu mbu anaeuma na dalili ni zile zile.
Nunueni mafuta ya mosquito repellent na muwe mnapakaa asbuhi na jioni sehemu zote za mwili!!

Ila tuna laana. Haiwezekani viongozi wa serikali wakawa wazembe na kuokujali hivi hata kwa kitu ambacho wao wenyewe wako hatarini DIRECTLY maana mbu wa aedes huuma mchana hata wakiwa kwenye maofisi yao ya AC. Na unaweza kuta mtu wa usafi kaumwa na mbu na wewe waziri unakuja jitanua ofisini unaumwa.
Sasa why the non cholance!!?

Africans!
 
DDT irudishwe. Ime eliminate mbu nchi zote zilizoendelea ila eti kwetu imekua banned sababu ya residual effect hivyo kuna uhatari wa kuingia kwenye food chain!! Its bull shit, with appropriate sprayin procedures, i.e. correct dilution, sprayin away from food sources the probability of enetering the food chain to a concentration that causes body harm negligible kabisa.
A cost effectiveness analysis will surely indicate the need of DDT.

Itaokoa maisha sana.
 
Aaagh MUNGU mkubwa nimepona Leo Ndio nitaweza kwenda kazini, Hii kitu ni balaaa msiiombeee kabisa iwapate
 
jamanieee,
hii Dengue sio mkakati wa wazungu kutupunguza idadi kweli?.

Afadhali wewe umefikiri nje ya box, tena nikikumbuka yale mambu makubwa ya pale Muhimbili tunayoambiwa yalitengenezwa Lab napata wasiwasi!
 
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili nchini, Gilbert Buberwa amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa dengue.

daktarii.jpg
dengue.jpg dengue2.jpg


Kifo cha Dk Buberwa kinafanya idadi ya watumishi wa afya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo kufikia wawili baada ya muuguzi Hamida Likoti kufariki dunia wiki iliyopita. Ugonjwa huo uliolipuka mkoani Dar es Salaam, umezua taharuki kwa wakazi wake kwa sababu hauna tiba na unasababishwa na mbu, Aedes Egyptae, anayeuma mchana na anayeweza kuzaliana katika majisafi yaliyotuama. Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia alisema jana kuwa Dk Buberwa alifariki dunia saa saba usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).


Dk Buberwa alianza kuumwa ugonjwa huo akiwa kazini katika Hospitali ya Temeke na kulazwa na hali yake ilipobadilika, alihamishiwa MNH kwa matibabu zaidi. "Kadiri siku zilivyozidi kwenda alibainika kwamba viungo vyake muhimu, yaani ini na figo vimeharibika, hivyo alisafishwa figo huku akiwa amelezwa Chumba cha Uangalizi Maalumu (ICU). Dk Saidia alikumbusha kuwa virusi vya dengue havina tiba isipokuwa dalili zake ambazo ni homa, kuumwa kichwa na viungo vya mwili – ndizo zenye tiba. Dk Buberwa alianza kuugua Mei 3, mwaka huu na siku iliyofuata alipelekwa hospitali na mkewe ambako alilazwa ili kupata uangalizi wa karibu wa madaktari wenzake. Kaka wa marehemu, Wakili Nickson Ludovick alisema: "Tunasubiri ndugu kutoka Bukoba na Musoma kwa mazishi yatakayofanyika hapa Dar es Salaam katika makaburi ya Kinyerezi keshokutwa."


Dk Malima alisema hadi jana, wafanyakazi tisa wa Hospitali ya Temeke walikuwa wamelazwa kutokana na homa hiyo. Alisema wafanyakazi hao ni madaktari watano, wauguzi watatu na mtaalamu mmoja wa maabara. "Kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita tumepokea wagonjwa wa dengue waliothibitika 15," alieleza Dk Malima.
Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Temeke, Shamim Kanju alisema wafanyakazi wanaendelea kuambukizwa kutokana na kuwa katika mazingira hatarishi kwa muda mrefu. Mtaalamu wa maabara, Eliud Kishebuka ambaye ni mmoja wa wagonjwa waliothibitika kuwa na homa hiyo, alisema alianza kujisikia mgonjwa juzi asubuhi, hivyo akaamua kwenda kufanya vipimo Mwananyamala ambavyo vilithibitisha kuwa ameambukizwa.


Dk Saidia alisema wataalamu wa vipimo hawajaelekezwa ipasavyo namna ya kutambua mgonjwa huo. Alisema endapo mgonjwa atachukuliwa kipimo kamili cha damu (full blood picture) na kuona kupungua kwa chembehai mgando nyeupe za damu, wajue kwamba hicho ni kiashiria kikuu cha ugonjwa wa dengue.


Mwandishi wa Gazeti la The Citizen, Mkinga Mkinga ni miongoni mwa watu walioambukizwa ugonjwa huo. Mkinga alisema jana kwamba alianza kuhisi homa na maumivu makali ya kichwa tangu Jumanne iliyopita na alipokwenda hospitali ilibainika kuwa ni homa ya dengue. "Nilipewa dawa za kutuliza pamoja na kunywa maji mengi, kwa sasa niko nyumbani kwangu ninaendelea nazo lakini kichwa bado kinauma na homa inakuwa kama ya vipindi," alisema.


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema wagonjwa wa dengue wameongezea na kufikia 399 hadi jana. Ofisa mwandamizi wa wizara hiyo, Dk Janeth Bugamba alisema jana kuwa kuna uwezekano wa idadi ya wagonjwa kuwa kubwa zaidi kwa kuwa hakuwa amepata takwimu kutoka hospitali zote. Msemaji wa MNH , Aminiel Aligaesha alisema wagonjwa wa dengue wanaongezeka kwa kasi katika hospitali hiyo. Alisema hadi kufikia jana, wagonjwa 65 walifika katika hospitali hiyo na kutibiwa kisha kurejea nyumbani na wengi ni kutoka maeneo ya jirani na hospitali hiyo wakiwamo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili (Muhas) ambao hata hivyo, hakutaja idadi yao.


 
Hakika kila nafsi itaonja umauti...pumzika kwa amani daktari
 
Poleni wafiwa. Hakika tuombe Mungu asitishe huu ugonwa maana kwa taifa letu na huduma za afya basi ukome eee Mungu.
 
Jamani watanzania wenzangu ebu tumuombe Mungu kwa pamoja atuepushe na ugonjwa huu jamani na hizi mvua ziache kunyesha kwakweli, na wale waliolazwa hospitali Mungu ashushe uponyaji haraka
 
Wakili Nickson, pole sana "learned broza"
Mwenyezi Mungu akupeni nguvu na imani hasa katika kipindi hiki kigumu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.
 
Hapo nilipoweka Blue panajieleza wazi ugonjwa huu ni Viral Disease wakati ugonjwa wa malaria Parasitical Disease kwa hiyo kama utakuwa na Ugonjwa huu ukipimwa kwa kipimo cha malaria automatical hakiwezi kuonyesha chochote na kama ikibahatika kikaonyesha vimelea vya Malaria basi ni lazima utakuwa na vyote yaani malaria na hii Dengue.
Chikungunya is a viral disease transmitted to humans by the bite of infected Aedes Aegyptimosquitoes. Chikungunya virus (CHIKV) is a member of the genus Alphavirus, in the familyTogaviridae. CHIKV was first isolated from the blood of a febrile patient in Tanzania in 1953, and has since been identified repeatedly in west, central and southern Africa and many areas of Asia, and has been cited as the cause of numerous human epidemics in those areas since that time. The virus circulates throughout much of Africa, with transmission thought to occur mainly between mosquitoes and monkeys.

Asante mkuu. Mungu akubariki
 
hizi zoote laana za maccm,ktk nchi hii machukizo ya haya maccm,ufisadi,ukahaba wa mazee mazima tena mawaziri kwa vitoto,dhuluma,kujilimbikizia utajiri wkt watz wengi wanakufa kwa njaa ndo machukizo yaliyofika mbele za Mwenyezi Mungu na sasa tutakiona.
 
Ama ni wale mbu wanaolelewa pale jangwani washaambukizwa ili watuue waafrika,i never trust white people though they hide it ..watatumaliza na bado umaskini unatuandama Mungu wangu!
 
Kwa sasa kama unaweza kuepuka kutembelea dar hiyo ni best option in prevention, hata mikoa ya jiran sio salama sana kwa hiyo tuchukue tahadhar sana tunapopanga safari zetu. Kama si lazima sana just wait kwa kuwa kipindi fulan cha mpito
 
Back
Top Bottom