Holstein-Friesian | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Holstein-Friesian

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Doltyne, Oct 21, 2011.

 1. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wadau naomba msaada wa mawazo na ushauri, Nimepitia pitia threads mbali mbali humu na nimehamasika na ufugaji wa ng'ombe wenye uwezo wa kutoa maziwa mengi kwa siku. Nina mpango wa kuanza na ng'ombe kama saba hivi wenye mimba.

  Kama kuna mtu anawafuga hawa Dar, naomba anialike kwake nikafanye site visit kidogo, na nimuulize maswali mawili matatu ya kinadharia kabisa ili niweze kuingia katika ufugaji huu.
  Natarajia kuwafugua Dar es salaam eneo lililo kati ya mbezi luguruni na bunju, almaarufu kama Mpiji Mahohe... Nina Heka 3 za kufanyia mradi huu, je kuna setbacks zozote au kuna challenges gani nijiandae nazo?

  Vipi kuhusu, chakula, maji, na uangalizi wao kwa ujumla.

  Naombeni msaada tafadhali.
  NB: Kama kuna mtu anaushauri zaidi wa namna ya kuwajengea mabanda madhubuti ningependa pia ushauri wake na mengineyo mengi.
  NB2: Nimeshapiga simu kwa mwalimu mmoja wa Kitulo kama alivyoelekeza Malila kwenye moja ya threads zilizopita na akanipa namba ya Muhusika na nimeshaweka booking ya kuwapata mwezi wa pili mwakani... Kama kuna mtu anajua shamba jingine naweza kuwapata kabla ya hapo ntafurahi pia akinihabarisha.

  Shukran sana.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Umeanza vizuri sana,
  Ushauri wangu wa bure ni huu, nenda Ruvu darajani pale,kuna shamba la serikali. Pale utapata utalaamu na mtalaam wa kukusaidia kwa gharama kidogo. Mpigi Magohe ni sehemu nzuri kwa kuanzia kwa sababu soko la maziwa litapatikana huko huko mpigi.

  Kila la kheri mkuu.
   
 3. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Shukran sana Malila, Ntajitahidi Jumatatu nikawatembelee, Nadhani ni pale kwenye ile ranch iliyo karibu na daraja, upande wa kulia kama unaenda moro na kushoto kama unarudi Dar, sio?
   
 4. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Najifunza mengi hapa wandugu
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ndio penyewe, ukifika omba wakusaidie kuanzia ktk hatua za mwanzo kabisa. Uliza madawa, magonjwa, watalaamu wa ujenzi wa mabanda na madakitari walio karibu na eneo lako. Swala muhimu uliza pia kama kuna mfugaji aliyekaribu na sehemu yako.

  Banda zuri linapunguza gharama za matibabu,mtalaamu mzuri atakupunguzia gharama za matibabu.
   
 6. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Shukran sana aisee. Yaani j3 tu inshaallah nipo nao. Ntatoa mrejesho hapa.
  Kweli kabisa, mambo mengi yanayoyokea baadae ni mazao ya kukata kona mwanzoni mwa mchakato mzima.
   
 7. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hongera Kaka.
  Hivi Ng'ombe mwenye mimba ,Anauzwa Tsh Ngapi,kwa DAR.
   
 8. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa Dar sifahamu, ila kitulo ni sh laki saba (700,000).
   
 9. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  nimevutiwa na bei,gharama ya usafiri to Dar?
   
 10. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Gharama ya usafiri to dar sijajua bado. Ila mi ntawasafirisha kwa usafiri binafsi. Kwahiyo ni kulipia diesel tu.
   
 11. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimepata interest sana, tafadhali, ukotoka huko tujulishe mpango unaendeleaje...
   
 12. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hakuna shaka ndugu, ntatoa mrejesho hapa, na wengine wafaidike.
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ndio tunasubiri mrejesho ulioahidi mkuu. Jumanne hii inaondoka.
   
 14. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Leo nimeenda pale Narco (ruvu darajani). Nimekutana na Meneja wa ile ranch, kwakweli ni mzee mmoja mwenye subira na werevu wa hali ya juu. Nimemsumbua sana kwa maswali lakini amenielewesha mambo mengi sana. Tuliongea kama saa zima, akanitembeza kwenye maeneo baadhi ya ranch na akaniambia kama nahitaji msaada zaidi wa kujenga mabanda nimpitie siku twende wote nane nane wana mifano mizuri pale.


  Kuhusu upatikanaji wa Ng'ombe pale kwa sasa hakuna Friesian wa kweli, wapo chotara na ni wachache hata 10 hawafiki na hawana mimba. Kwahiyo kanishauri niende kwenye ranch nyingine kama vile Ngerengere (morogoro) na mwanza, karibu na mpaka wa shinyanga.

  Ntaenda kote huko inshaallah, weekend hii ntaenda ngerengere na baada ya wiki 2 ntaenda mwanza.

  Kuhusu jamaa wa kitulo, nimempigia tena simu leo baada ya kutoka ruvu, akaniambia alivyonipa jibu nimcheki february hakumaanisha watakuwepo wa kununua, alimaanisha ndio anaweza kuchukua order yangu.

  Nadhani nimeweza kufupisha msafara wa leo. Samahanini sana sikuweza kuwaupdate jana, kwani nilitingwa na shughuli za mjini hapa nikakosa muda wa kwenda ruvu.

  Kama kuna mungine ana taarifa zaidi atusaidie.
  Nb: kutokana na safari yangu ya leo. Nimeongeza hamasa ya kuwatafuta hawa ng'ombe mpaka niwafuge. Kwani ni lulu.

  Kuna mtu anashamba mbele ya vigwaza la nyasi za ng'ombe. Nimeambiwa huyo ndio tegemezi kuu la wafugaji. Anauza nyasi kama njugu. Aisee hizi business ideas nyingine ni big soo. Sijui mzee aliwazaje wazaje....!!!
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Safi mkuu.
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu, good work

  very inspiring
   
 17. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tuko pamoja, I'll keep you updated. Tuombe uzima.
   
 18. Mwanakilimo

  Mwanakilimo Member

  #18
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini unaamini H. fresian ni lulu mkuu?

  Je, utawfahamuje ukiwaona kuwa huyu ni pure breed n sio chotara?
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Aina hii hutoa maziwa mengi sana,ushauri wa kwenda ktk mashamba ya serikali ni kwa sababu ya kutaka kupunguza uwezekano wa kubambikiwa, unadhani kama lingekuwa sio la serikali,si angeuziwa hata hao chotara kwa jina la pure breed. Ni mawazo yangu.
   
 20. Mwanakilimo

  Mwanakilimo Member

  #20
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukweli ni kwamba hakuna shamba la serikali Tz hii kwa sasa lina uhakika wa kuwepo kwa HF pure breed. Kuna ranchi moja ipo Kagera, zamani ilikuwa na pure breeds lakini hata yenyewe sasa inaaminika imeshachakachua. Kitulo pia waliopo sio pure breed, japokuwa kwa kiasi fulani wanakaribia.

  Kwa maoni yangu ni kuwa ufugaji wa ng'ombe sio kitu cha kuanza leo na kuona mafanikio kesho. kwa hiyo kama ni ng'ombe wanaotoa maziwa kwa wingi, then ni bora mtu ukjitahidi kuwazalisha mwenyewe kwa kufanya selection na planned breeding. Kwa maana hiyo, ni bora mtu ukanunua tu ngombe (chotara may be) kwenye shamba ambalo lina historia ya kuwa na ng'ombe wanaotoa maziwa mengi (hata karibu na Dar siku hizi yapo), then ukaenda kufanya breeding kwa kupandikiza kwa chupa, hadi ukapata line ya ng'ombe wanaotosheleza malengo yako...
   
Loading...