Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
Bado sijauona huo "ujumbe mzito" unaodaiwa kuwepo kwenye "ndoto ya Mzee Mwanakijiji", au pengine "sina macho.." au "sijui maana..." lakini nimeelewa vizuri alivyoainisha mkuu Pundit, ambaye amekuwa na ujasiri wa kusema waziwazi wala si kwa gia ya "ndoto", kuhusu viongozi na nasaba zao wanavyojinufaisha.
Labda niseme hivi si makosa kwa Rais Kikwete kuwa shemeji yake Rostam Azizi, lakini kama ushemeji huo utamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake kama Rais basi hapo ndipo hiyo hoja itakapokuwa na mashiko.
Kama huu undugunization unaoudai upo chadema ndio umesaidia kuwatia tumbo moto mafisadi na sasa wanalialia kama watoto mambo poa! Na inabidi wale wote wenye mawazo dhidi ya ufisadi wa ccm waoleane watoto na kuchangiana damu ili kuwe na undugu wa kudumu na kuendeleza vita kali dhidi ya mafisadi wa ccm!
OK naomba kueleweshwa yafuatayo:
1. Huo ushemeji kati ya Jakaya Kikwete na Rostam Azizi ukoje?
2. Je, huo ushemeji umemzuia vipi Kikwete kuwajibika kama Rais wa Tanzania, kama ni huo ushemeji ndio unaosababishwa ashindwe kuwajibika?
3. Je ni makosa kwa mashemeji, au hata ndugu kuwa kwenye siasa wakati mmoja na kuwa kwenye chama kimoja pamoja?
4. Je tunazo sheria zinazotulinda na mazingira yanayoweza kusababisha conflict of interests au muonekano wake?
mwanakijiji mbona umezunguka?
JK ni shemeji ya Rostam baada ya mkuu huyo kupata mtoto na dada yake Rostam na kimsingi alikuwa amuache Salma kabla tu ya Uchaguzi 2005. Ni kwa sababu hiyo udugu na urafiki wao umeunganishwa kwa damu. Hili linajulikana karibu na watu wengi tu waliokaribu.
Ukweli ni kuwa karibu wote hawa wameingiliana hadi inatisha. Kuna walio na watoto wasio wa waume zao, na wapo waliopeana watoto wao ili "kuunganisha" familia.
Ni kwa sababu hiyo itakuwa vigumu sana kwa mfano kufukuzana pale BoT, Usalama wa Taifa, au kwenye maeneo mengine nyeti.
Lakini kama wanafanya kazi zao vizuri, wewe kinakuuma nini?
asante.
Haya piya yananikumbusha thread ya inayoishutumu chadema kwa udugunization au nyerere alikosea aliposema waTanzania wote ni ndugu? duhh!
KWAKO KADA MPINZANI!
Leo ndo nimethibitisha kuwa wewe ni kada mpinzani wa mazuri lakini mabaya kwako ni mazuri na ndo maana wadau wakipost treads zenye kujenga na kutetea maslahi ya Taifa hili we ndo wa kwanza kwa kupost comments zisizo na mvuto grow up dogo.
1- Threads inayosema Chenge jiuzulu mpaka sasa ina kurasa 10 lakini kwa sababu ameguswa mtu wako aaah umekaa kimyaaa.
Unatia aibu bwana mdogo.
FICHA UPUMBAVU WAKO USIFICHE BUSARA ZAKO.
Well, nimekuwa nikijiuliza ni kwanini wakati mwingine inakuwa vigumu sana kuchukuliana hatua serikalini na katika ngazi mbalimbali za uongozi wa Taifa letu. Mwanzoni nilidhani kinachowaunganisha ni maslahi yao ya kifedha na siri wanazotunziana.
Usiku wa leo nimeota ndoto ambayo kwa hakika ni mbaya. Tulikuwa tumesimama kwenye ufukwe wa bahari ya hindi tukishuhudia magari ya maharusi yakipita huku wakirekodi video. Mimi na wenzangu tusiohusiana na harusi hiyo tukajikuta tunarekodi video kwa kimbelembele chetu cha ndotoni.
Tulipokaa kuangalia mikanda hiyo ya video ndipo tulijikuta tunapigwa na butwaa.
a. hakukuwa na harusi moja bali zilikuwa ni nyingi
b. kuna baadhi ya watu walikuwa wanajirudia toka harusi moja (ambako alikuwa ni mkwe) na kwenda harusi nyingine (walikuwa mashemeji na wifi) na kuibuka kwenye harusi nyingine (ambako walikuwa ni maharusi).
Mwisho wa mkanda (pale penye "ze endi") maharusi wote wakajipanga mstari kupiga picha ya pamoja. Ndipo mmoja wao akainua bango linalosema "Now you know". Nilipoangalia waliosimaam katika kupiga picha naweza kusema ni "who is who" of Tanzania Political history and political dynasties...
Hata hivyo kati ya walionishtua ni ushemeji kati ya
Rostam Aziz na Jakaya Kikwete!!!
Sijui ni kweli kiasi gani au ndio "ndoto" tu..
Ukianza na BoT na Richmond utakuwa umejibu swali lako namba 2
Sasa mbona hilo linaibua maswali mwengine kama:
Je, huu ushemeji kati ya JK na RA ndio uliowezesha na kufanikisha uchotaji BOT 2004 - 2005? Kama ndivyo, tusemeje kuhusu uchotaji wa kuanzia huko nyuma, usikute akina Mkono et al. nao mashemeji mtu pia? Au ushemeji na ukwe n.k. umekuwa ukitengenezwa miaka mingi kwa malengo haya? Kama ndivyo basi sisi siyo jamhuri tena, tumeshakuwa "Sultanate of Tanzania", na anayetawala sasa hivi ni Sultan Jakaya bin Mrisho bin Kikwete.
Kama sheria tunazo halafu hazitumiki basi tuna faida ya kuwa nazo kweli?