Hold on a minute! Mtu na shemeji yake

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,335
2,000
Well, nimekuwa nikijiuliza ni kwanini wakati mwingine inakuwa vigumu sana kuchukuliana hatua serikalini na katika ngazi mbalimbali za uongozi wa Taifa letu. Mwanzoni nilidhani kinachowaunganisha ni maslahi yao ya kifedha na siri wanazotunziana.

Usiku wa leo nimeota ndoto ambayo kwa hakika ni mbaya. Tulikuwa tumesimama kwenye ufukwe wa bahari ya hindi tukishuhudia magari ya maharusi yakipita huku wakirekodi video. Mimi na wenzangu tusiohusiana na harusi hiyo tukajikuta tunarekodi video kwa kimbelembele chetu cha ndotoni.

Tulipokaa kuangalia mikanda hiyo ya video ndipo tulijikuta tunapigwa na butwaa.

a. hakukuwa na harusi moja bali zilikuwa ni nyingi
b. kuna baadhi ya watu walikuwa wanajirudia toka harusi moja (ambako alikuwa ni mkwe) na kwenda harusi nyingine (walikuwa mashemeji na wifi) na kuibuka kwenye harusi nyingine (ambako walikuwa ni maharusi).

Mwisho wa mkanda (pale penye "ze endi") maharusi wote wakajipanga mstari kupiga picha ya pamoja. Ndipo mmoja wao akainua bango linalosema "Now you know". Nilipoangalia waliosimaam katika kupiga picha naweza kusema ni "who is who" of Tanzania Political history and political dynasties...

Hata hivyo kati ya walionishtua ni ushemeji kati ya

Rostam Aziz na Jakaya Kikwete!!!

Sijui ni kweli kiasi gani au ndio "ndoto" tu..
 
Kalamu

JF-Expert Member
Nov 26, 2006
873
0
Mzee Mwanakijiji,

Ukiongeza hapo sura ya pili na ya tatu, ni 'novel' ya kuvutia kuisoma, na sinema yake itapendeza tu! Utakuwa umempiku Chenge na kibilioni chake kimoja!

Watu wa kisasa watakwambia, kwani kuna ubaya gani? Nami nasema hakuna ubaya, hadi uhusiano huo unapoambatana na ufisadi.
 
Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,179
2,000
utaota kila ndoto, sio bure una lako.

ota na za mbbowe na mdoe na zitto na wengine.

mie nnaamini ukilala unaweweseka kwa choyo na husda
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,335
2,000
Kama kuna ushemeji kokote uonesheni sijauhukumu kuwa ni mbaya... kwa sababu wakati tatizo wengine laweza kuwa ni masuala ya fedha, naamini tatizo kubwa ni "undugunization" uliojikita kiasi kwamba Rais Mkapa mkuu wa BRELA ni Mkapa mwingine halafu Rais anataka kuanzisha kakampuni nje ya taratibu au maadili na mtoto mtu hawezi kupinga... ni mkorogano wa undugu kiasi kwamba maslahi ya Taifa kwa kweli yanatishiwa.
 
S. S. Phares

JF-Expert Member
Nov 27, 2006
2,138
1,195
CCM imetanda kama Tandabui...ukiangalia suala la "undugunization" kwenye serikali unaweza kukata tamaa kuishi Tanzania.
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
195
Mzee Mwanakijiji,
Vipi tena "hoja kwa hoja" zinakushinda unaanzana na "ndoto na hisia" sasa? Kama una hoja we iweke tu usijifiche nyuma ya ndoto kama kweli una nia ya kumkoma nyani kisawasawa...
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,738
0
upupu kama huu usiwe na nafasi humu ! uende kwenye vioja ! na mimi niliota ndoto Mnyika mtoto wa Mbowe !
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,738
0
Mzee Mwanakijiji,
Vipi tena "hoja kwa hoja" zinakushinda unaanzana na "ndoto na hisia" sasa? Kama una hoja we iweke tu usijifiche nyuma ya ndoto kama kweli una nia ya kumkoma nyani kisawasawa...

hiyo ndio base yake katika kutunga conspiracy theories zake ! USANII MTUPU !alidhani ataibuka na hoja, kumbe kaibuka na kioja !
 
Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330
1,250
Mzee MKJJ tuambie ukweli tujue maana inawezekana tumepitwa na wakati, RA na JK ni mtu na shemeji yake kivipi maana najua Mama Salma ni Mmakonde na RA ni Muirani au siku hizi RA naye antokea Mtwara?
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
2,000
Mzee Mwanakijiji,
Vipi tena "hoja kwa hoja" zinakushinda unaanzana na "ndoto na hisia" sasa? Kama una hoja we iweke tu usijifiche nyuma ya ndoto kama kweli una nia ya kumkoma nyani kisawasawa...

Si vibaya ukarudia kusoma ili uelewe vyema kama hujaona ujummbe mzito.Maana kama unasoma kama hadithi unaweza utoke kapa kama akina Kada na kundi lake hapa .Hebu rudia kusoma kaka utapata hoja ambayo iko wazi na haiko nyuma ya ndoto hata mara moja .Soma tena nakushauri kwa mara ya mwisho .Una uwezo mkubwa kuliko Kanda na kundi lake .
 
KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,738
0
Si vibaya ukarudia kusoma ili uelewe vyema kama hujaona ujummbe mzito.Maana kama unasoma kama hadithi unaweza utoke kapa kama akina Kada na kundi lake hapa .Hebu rudia kusoma kaka utapata hoja ambayo iko wazi na haiko nyuma ya ndoto hata mara moja .Soma tena nakushauri kwa mara ya mwisho .Una uwezo mkubwa kuliko Kanda na kundi lake .
mhm, haya bana mie sisemi !

NA MIMI NIMEOTA/NIMESIKUA FUNUNU BIN FUNUNU WA HABARI KWAMBA MNYIKA NI MTOTO WA NJE WA MBOWE !!
 
Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,738
1,225
Kama kuna ushemeji kokote uonesheni sijauhukumu kuwa ni mbaya... kwa sababu wakati tatizo wengine laweza kuwa ni masuala ya fedha, naamini tatizo kubwa ni "undugunization" uliojikita kiasi kwamba Rais Mkapa mkuu wa BRELA ni Mkapa mwingine halafu Rais anataka kuanzisha kakampuni nje ya taratibu au maadili na mtoto mtu hawezi kupinga... ni mkorogano wa undugu kiasi kwamba maslahi ya Taifa kwa kweli yanatishiwa.

Hapo hujaingiza mix la Mramba kuwa baba yake Peter, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mama Anna Mkapa, aliyeenda kupewa ubinafsishaji wa asset za TTCL kiajabu ajabu.

Sasa stepdad rais na baba Waziri influentcial, apewe nini zaidi?

Moreover kazi ya kuchunguza uuzaji wa assets za TTCL ilipokuja tume akapewa nani?

Who else but Mramba? Kumchunguza mtoto wake mwenyewe Peter.

Na wala hakuwa na integrity ya ku declare conflict of interest wala nini.Ndiyo nchi yetu hiyo.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,039

Mkjj unanikumbusha undugunization uliopo ndani ya chadema kama unavyoelezewa kwenye thread moja wapo humu. Duhh, au ndio mila zetu Tanzania?
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,190
0
Mkjj unanikumbusha undugunization uliopo ndani ya chadema kama unavyoelezewa kwenye thread moja wapo humu. Duhh, au ndio mila zetu Tanzania?

Kama huu undugunization unaoudai upo chadema ndio umesaidia kuwatia tumbo moto mafisadi na sasa wanalialia kama watoto mambo poa! Na inabidi wale wote wenye mawazo dhidi ya ufisadi wa ccm waoleane watoto na kuchangiana damu ili kuwe na undugu wa kudumu na kuendeleza vita kali dhidi ya mafisadi wa ccm!
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,190
0
Hapo hujaingiza mix la Mramba kuwa baba yake Peter, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mama Anna Mkapa, aliyeenda kupewa ubinafsishaji wa asset za TTCL kiajabu ajabu.

Sasa stepdad rais na baba Waziri influentcial, apewe nini zaidi?

Moreover kazi ya kuchunguza uuzaji wa assets za TTCL ilipokuja tume akapewa nani?

Who else but Mramba? Kumchunguza mtoto wake mwenyewe Peter.

Na wala hakuwa na integrity ya ku declare conflict of interest wala nini.Ndiyo nchi yetu hiyo.

Kuna mengi hapa ambayo yatawekwa wazi kwenye hii thread na kama kawaida ya JF mafisadi na watetezi wao watanyuti tu na kuishia Monduli kama alivyoanza Lowasa, amefuata Chenge, na wengine bado wako njiani kuwafuta!

Long live JF!
 
Mwakilishi

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
484
195
Bado sijauona huo "ujumbe mzito" unaodaiwa kuwepo kwenye "ndoto ya Mzee Mwanakijiji", au pengine "sina macho.." au "sijui maana..." lakini nimeelewa vizuri alivyoainisha mkuu Pundit, ambaye amekuwa na ujasiri wa kusema waziwazi wala si kwa gia ya "ndoto", kuhusu viongozi na nasaba zao wanavyojinufaisha.

Labda niseme hivi si makosa kwa Rais Kikwete kuwa shemeji yake Rostam Azizi, lakini kama ushemeji huo utamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake kama Rais basi hapo ndipo hiyo hoja itakapokuwa na mashiko.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom