Hoja za wanaoona lockdown haifai ni zipi? Tuelimishane

Inawezekana kama nchi tumekosa watu wenye busara wanaoweza kushauri vizuri kwa mamlaka ya juu,viongozi wa dini nao pia wamekuwa mazezeta,hawawezi kuona hatari zaidi ya kushangilia kuruhusu ibada wakati wanajua fika ni hatari kubwa sana,MAAFA tunajitakia wenyewe kwa ujuha wetu kuruhusu mabasi ya dar na mikoani kuendelea kuja na kutoka dsm mahali ambapo ni kitovu cha ugonjwa.

Ni muhimu kuomba MUNGU,Ila MUNGU alitupa akili ya kufikiria.Tz ilikuwa rahisi sana kuublock huu ugonjwa tungekuwa na viongozi wenye utashi wa kunusa hatari,tulianza kufunga shule wakati hakikuwa chanzo cha ugonjwa,ilitakiwa tuanze kupambana na chanzo,ila tulidhani tuko mbali na kwenye sayari nyingine.

Mkuu ungekuwa hata mjumbe tu kwenye hizi tume zinazoongoza mapambano na ugonjwa huu hakika hadi sasa tungekuwa tumeshaanza kutangaza ushindi.

Ni mazezeta yasiyojitambua tu ndiyo yanaweza kusubiria ugonjwa huu kutoweka wenyewe huku wakihamasishana kuchapa kazi tu.
 
Mkuu nchi kama Rwanda si nchi ya magharibi.

Tunazo raslimali za kutosha tunaweza kujisimamia wenyewe kwa chakula kwenye hili gonjwa.

Wasiwasi wetu ni njaa mkuu?
Unajua Rwanda ina watu wangapi?
Au unaandika tu huduma ya watu 12m utalinganisha na takribani 50m?
 
Unajua Rwanda ina watu wangapi?
Au unaandika tu huduma ya watu 12m utalinganisha na takribani 50m?

Labda kama unamaanisha 50m waachiwe kufa. Sehemu yenye watu 50m ina maana raslimali zaidi ni fursa zaidi. Population density ya Rwanda unaijua mkuu?

Kingine usisahau si wote katika 50m wanahitaji misaada.

Ni ajabu na kweli kuwa pamoja na hili kuelezwa sana bado tu hujaelewa mkuu?

Mafanikio ya Rwanda yako kwenye jitihada za dhati zisizo na tashwishi kama hizi:
IMG-20200416-WA0000.jpg


Kwenye bold katika waraka kama huu watu kama Mwigulu unawahusu sana.
 
Rwanda wapo 12million yes lakini ujue Arusha ni kubwa kuliko Rwanda
So Rwanda wana scarcity ya resources kuliko sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sina hakika kama anafahamu population density ya Rwanda ni among the highest duniani na raslimali zao haziwezi kuwa kama zetu.
 
Najilaumu kwa nn sikununua uraia ata wa nchi nyingine.

Watanzania ss ni watu wa ajabu sana huwa wanaenda kinyume siku zote.

Wakisema kila mtu akae ndani(lockdown) hamna kutoka mtakuja na lawama umu kuwa wamekurupuka watu wanakufa njaa.

Wasipo funga napo wanalalamika kuwa kwa nn hawafungi watu wakae ndani.

Mtu unasahau kabisa raia wa nchi yetu asilimia kubwa ni kipato cha siku kufanya kazi unakula unalala, ukimfungia ndani week watu watakufa zaidi ya ugonjwa.
 
Najilaumu kwa nn sikununua uraia ata wa nchi nyingine.

Watanzania ss ni watu wa ajabu sana huwa wanaenda kinyume siku zote.

Wakisema kila mtu akae ndani(lockdown) hamna kutoka mtakuja na lawama umu kuwa wamekurupuka watu wanakufa njaa.

Wasipo funga napo wanalalamika kuwa kwa nn hawafungi watu wakae ndani.

Mtu unasahau kabisa raia wa nchi yetu asilimia kubwa ni kipato cha siku kufanya kazi unakula unalala, ukimfungia ndani week watu watakufa zaidi ya ugonjwa.

Mkuu watu kama wewe mnawafanya wengine kujutia utanzania wao. Yote haya yameelezwa mno na hata kwenye uzi huu:

" ....
1. Wapo wenye kuhitaji msaada kabisa (in totality).
2. Wapo wenye kuhitaji msaada kiasi (partial).
3. Wapo wanaojitosheleza.
4. Wapo wenye ziada na hata tayari kusaidia wengine.

Serikali pia ipo.

Ni kweli kuwa haitakuwa kipindi cha starehe. Kitakuwa kipindi kigumu cha muda mfupi ambacho hata hivyo hakuna atakaye kufa kwa njaa au kukosa kabisa mahitaji muhimu katika kipindi hicho."

Cha mbadala hamna bali visabu sababu tu jamani?

Hata mnapoambiwa hakuna atakaye kufa njaa bado tu? Au mnataka muambiwe itakuwa fursa ya kugawiwa mapesa?
 
kwa mfano ukiambiwa kesho ni lock down..
Una akiba ya kiasi gani ya chakula nyumbani kwako?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"

Mkuu umeambiwa lockdown zinatambua uwezo tofauti kiuchumi wa watu. Zaidi ukaambiwa hakuna atakaye kufa njaa.

Umeulizwa kama hutaki tupe sababu zako ikibidi njia mbadala kama unayo.

Vipi au unataka ugawiwe mapesa?

Haya uliweza kuyasoma kwenye huu uzi:

IMG_20200416_125352_093.jpg
 
HIVI WEWE kwa mawazo yako unadhani magufuli atatoa chakula bure?.
Kwa muda wote wa lockdown?
Mkuu umeambiwa lockdown zinatambua uwezo tofauti kiuchumi wa watu. Zaidi ukaambiwa hakuna atakaye kufa njaa.

Umeulizwa kama hutaki tupe sababu zako ikibidi njia mbadala kama unayo.

Vipi au unataka ugawiwe mapesa?

Haya uliweza kuyasoma kwenye huu uzi:

View attachment 1420653

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
HIVI WEWE kwa mawazo yako unadhani magufuli atatoa chakula bure?.
Kwa muda wote wa lockdown?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"

Kwa nini una mawazo mgando hivyo mkuu. Kwani Magufuli yeye nani?

Pia kwa nini unadhani kila mtu atahitaji msaada? Mbona hii kitu unataka sana kuifanya fursa?

Sababu zako za kupinga lockdown ziko wapi?

Jikite kwenye mada. Kama huna hoja hata ukikaa kimya ni sawa tu?
 
Baada kupitia comments zote na nyuzi zote zihusianazo na Corona, pia kufuatilia taarifa, kauli na machapisho rasmi na yasiyokuwa rasmi, ninakiri kuwa sijaona sababu yoyote ya maana au nzito ya kwa nini lockdown isitumike kama mbinu ya kutusaidia kuzuia maambukizi (au hata kuutokomeza kabisa ugonjwa huu) kutoka nchini.

Pasipo na kuoneana haya sote kwa umoja wetu hatupaswi kumkubalia yeyote (mtu binafsi, kampuni, jumuiya, chama nk. na hata serikali) atakaye jaribu kuutumia ugonjwa huu au jitihada za kupambana nao kama fursa yake ya kujinufaisha na kwa namna yoyote.

Cha msingi kitakuwa kuhakikisha tu hakuna mmoja wetu atakufa kwa kukosa chakula au mahitaji yake ya lazima katika kipindi chote cha mapambano.

Muda wa kuiitisha serikali kuchukua hatua hizi umekwisha pita sana (is long overdue)
 
Hivi ukiamua wewe mwenyew kujifungia kuna tatizo? Kuna makundi mawili tulio chagua kufa kwa corona na mnaotaka kufa kwa njaaa chagua wewe

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu haya mbona yameelezwa sana. Au ndiyo umefika tokea sayari nyingine? Tupe sababu za kutoitaka njia hii au tupe mbadala.

Yaliyokwisha jadiliwa ni pamoja na haya hapa chini:
IMG_20200416_125352_093.jpg

IMG_20200416_173646_378.jpg


Wewe una yapi? Ukizingatia pia mada zote hamsomi hata ni vigumu kujua mnataka nini:

IMG_20200416_174446_024.jpg


Au mnataka mfanye jitihada za kuutokomeza huu ugonjwa kuwa fursa mkuu?
 
Back
Top Bottom