Mabibi na mabwana naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Tumekabiliwa na ugonjwa ambao unatishia maisha yetu kama taifa. Mengi yameelezwa yakiwamo ufafanuzi wa nini maana ya lockdown na kwa nini ni muhimu katika kupambana na Corona. Imeelezwa pia, kwa nini hakuna kitu kama lockdown ya mtu mmoja mmoja.
Mifano imetolewa kuonyesha lockdown haina maana ya mtu kufungiwa chumbani au nyumbani, bali watu wote katika eneo husika kusalia majumbani. Shughuli zilizo muhimu tu ndiyo pekee huruhusiwa kuendelea.
Imeelezwa kwa mifano, tahadhari huchukuliwa kuona kuwa hakuna atakaye athirika kufikia hatua kufa kwa njaa au kukosa kabisa mahitaji muhimu kwa wakati wote wa lockdown. Hata hivyo ni kweli kuwa mtu hata kula au kupata kile ambacho 100% angependa kula au kupata katika kipindi hicho cha mapambano.
Njia hii imethibitika kuwa madhubuti kabisa katika kuivunja minyororo ya maambukizi ya Corona ambayo ni lazima ivunjwe ili kuudhibiti ugonjwa huu.
Bila ya minyororo hii ya maambukizi kuvunjwa, ugonjwa huu utaendelea kuenea kwa kasi. Watu watazidi kufa. Hakutakuwa na natumaini ya lini mashule yatafunguliwa wala ya lini tutarejea kwenye shughuli zetu zote za kawaida.
Kwisha kuweka utangulizi huu, ingependeza kufahamu wanaopinga kutumia njia hii ya lockdown kutanzua janga la ugonjwa huu unaotukabili, hoja zao hasa ni zipi na pengine wanao mbadala upi? Ni muhimu kama jamii tukawa na njia mbalimbali mezani tukijiridhisha kuwa ni ipi tunayoifuata na kwa matumaini yapi.
Ukiangalia kinachotokea Ecuador sasa ni majuto. Hivi wanajilaumu kwanini hawakuchukua hatua kali mapema.
Serikali inaomba msamaha kwa kuchelewa mno kuchukua hatua wakati mitaa tayari imejaa maiti za ugonjwa wa Corona:
Pamoja tutaushinda ugonjwa huu.
Humbly nawasilisha.