Hoja za kijinga kuamuliwa kwa nguvu za kitaifa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Lugha ndio urithi wa kwanza kabisa wa binadamu na taifa lake, mtz anayedharau lugha ya kiswahili huyo ni mhaini.

Lugha sio maarifa wala usomi, bali ni nyenzo ya kuyatoa /kueleza Maarifa au jumbe mahususi ulionao. Kujua kiingereza sio Usomi ni kama kikurya na kihehe tu.

Mtu anayekucheka nakukwambia hujasoma kwakuwa huwezi kuongea kiingereza huyo ni MJINGA na mtumwa kifikra na kiroho.

Viongozi wa China, Italia, Ufaransa, Urusi nk hata wakutanapo na wajuao lugha nyingine lakini wao hutumia lugha zao, ktk hili heko Magufuli.

Hakuna taifa duniani lililoendelea kwakutumia lugha ya kigeni, ni lazima watu wetu wafunzwe kutumia lugha ya kiswahili na wahimizwe kuipenda.

Kosa kubwa la watawala ni kulazimisha kutumia lugha za kitumwa ilihali hawaziwezi wakati lugha yao ya kiswahili ina hadhi na tunu kuu kwao

Nilitaraji kuona watu wakifurahi nakutembea kifua mbele matako nyuma, pale rais wao anapotumia lugha ya kiswahili ktk meza ya kimataifa, lakini imekuwa kinyume,

Kama haujui lugha haikuzuii kujua jambo lolote duniani, utalijua tu ndio maana kuna watu wanatumia alama kama lugha mbadala. Lugha siusomi

Ni hatari kutumia lugha usiyoijua kufikisha ujumbe unaoujua. Kwa wanaoijua lugha yao watakudharau na wata dhani hauna Maarifa.
 
Watanzania sisi ni wajinga wa kuchagua na kupanga ndo maana hatuendelei.

Vichocheo vya maendeleo siyo lugha ya wakoloni
 
Unaongea kwenye mkutano wa hadhara kiinglish wakati 90% ya unaowahutubia hawakuelewi,sasa sijui ndiyo usomi au???
 
wasameheni bure ukawa hawana hoja tena sasa, utendaji wa magufuli umewaacha midomo wazi wamebaki kushadadia lugha isiyo yetu
 
kama unaowahutubia wote hawajui lugha unayowasilisha ujumbe wako unategemea nn
Nisawa na.kumpigia mbuzi gitaaa bac afatane na.mkalimani kama wanaofanya wao wanapoenda vijijini sio ujinga nikutaka ujumbe ufike
 
Yerico leo naunga nawe, lugha kwa hakika ni chombo kitumikacho kubeba taarifa au maarifa kitumike katika mawasiliano.

Ili uwe mahili au ufahamu angalau robo ya misamihati rahisi hukuchukua miaka kumi na miwili kufanya mazoezi ya lugha uliyokusudia kujifunza. Ni jambo la busara sana kuwasilisha ujumbe katika lugha unayo imudu vyema kuliko usiyo imudu.

Ilkiwa ni kweli Mh. JPM haimudu lugha ya kiingereza kwangu mimi si dhambi au ujinga ila lililo muhimu ni kwa Rais kukienzi kiswahili Lugha adhimu inayo zungumzwa mahali pengi Duniani, ujerumani wana idhaa ya kiswahi, uchina, uwingereza penyewe wana idhaa pia.

Nimekuwa nikililia kiswahili kutumika kama Lugha ya kufundishia kwenye elimu ya juu, ikiwa ufasiri wa mitaala yetu haujakamilika lakini sasa tunae kiongozi anae kithamini kiswahili na kukitumia kuwakilisha ujumbe wa kitaif kimataifa. Heko JPM

Wale wanaobeza na kudhani lugha za kigeni ni bora sana kwa msitakabali wa nchi nawasikitikia.
 
Lugha ndio urithi wa kwanza kabisa wa binadamu na taifa lake, mtz anayedharau lugha ya kiswahili huyo ni mhaini.

Lugha sio maarifa wala usomi, bali ni nyenzo ya kuyatoa /kueleza Maarifa au jumbe mahususi ulionao. Kujua kiingereza sio Usomi ni kama kikurya na kihehe tu.

Mtu anayekucheka nakukwambia hujasoma kwakuwa huwezi kuongea kiingereza huyo ni MJINGA na mtumwa kifikra na kiroho.

Viongozi wa China, Italia, Ufaransa, Urusi nk hata wakutanapo na wajuao lugha nyingine lakini wao hutumia lugha zao, ktk hili heko Magufuli.

Hakuna taifa duniani lililoendelea kwakutumia lugha ya kigeni, ni lazima watu wetu wafunzwe kutumia lugha ya kiswahili na wahimizwe kuipenda.

Kosa kubwa la watawala ni kulazimisha kutumia lugha za kitumwa ilihali hawaziwezi wakati lugha yao ya kiswahili ina hadhi na tunu kuu kwao

Nilitaraji kuona watu wakifurahi nakutembea kifua mbele matako nyuma, pale rais wao anapotumia lugha ya kiswahili ktk meza ya kimataifa, lakini imekuwa kinyume,

Kama haujui lugha haikuzuii kujua jambo lolote duniani, utalijua tu ndio maana kuna watu wanatumia alama kama lugha mbadala. Lugha siusomi

Ni hatari kutumia lugha usiyoijua kufikisha ujumbe unaoujua. Kwa wanaoijua lugha yao watakudharau na wata dhani hauna Maarifa.
chadomo wakikusikia, mimi simo
 
Lugha ni sehemu ya utamaduni na utambulisho wa watu. Kukumbatia lugha za wakoloni ni kuendeleza ukoloni mamboleo na matakwa yao ya kututawala hadi kiakili. Tujivunie lugha yetu, utamaduni wetu ili tukate hii minyororo ya ukoloni na unyonyaji. Ukisema Kiingereza in maana ni lugha ya waingereza halafu unaona ni ufahari fulani. Ujinga tu.
 
Lugha ndio urithi wa kwanza kabisa wa binadamu na taifa lake, mtz anayedharau lugha ya kiswahili huyo ni mhaini.

Lugha sio maarifa wala usomi, bali ni nyenzo ya kuyatoa /kueleza Maarifa au jumbe mahususi ulionao. Kujua kiingereza sio Usomi ni kama kikurya na kihehe tu.

Mtu anayekucheka nakukwambia hujasoma kwakuwa huwezi kuongea kiingereza huyo ni MJINGA na mtumwa kifikra na kiroho.

Viongozi wa China, Italia, Ufaransa, Urusi nk hata wakutanapo na wajuao lugha nyingine lakini wao hutumia lugha zao, ktk hili heko Magufuli.

Hakuna taifa duniani lililoendelea kwakutumia lugha ya kigeni, ni lazima watu wetu wafunzwe kutumia lugha ya kiswahili na wahimizwe kuipenda.

Kosa kubwa la watawala ni kulazimisha kutumia lugha za kitumwa ilihali hawaziwezi wakati lugha yao ya kiswahili ina hadhi na tunu kuu kwao

Nilitaraji kuona watu wakifurahi nakutembea kifua mbele matako nyuma, pale rais wao anapotumia lugha ya kiswahili ktk meza ya kimataifa, lakini imekuwa kinyume,

Kama haujui lugha haikuzuii kujua jambo lolote duniani, utalijua tu ndio maana kuna watu wanatumia alama kama lugha mbadala. Lugha siusomi

Ni hatari kutumia lugha usiyoijua kufikisha ujumbe unaoujua. Kwa wanaoijua lugha yao watakudharau na wata dhani hauna Maarifa.
Wana JF wengi wanashadidia sana hoja hii lakini zinapotokea mada za Kiingereza mchango wao unakuwa chini sana ambapo ndiyo wangeonyesha umahili, weledi na kubobea kwao kwenye lugha ya Kiingereza. Hii ni fursa pekee kuonyesha wanamudu lugha ya Malkia zaidi ya Magufuli. Mod naomba utupe takwimu ya mada za kiingereza na avatars za wachangiaji kama watatokea wengi waliobebea bango hoja hii.
 
Watanzania sisi ni wajinga wa kuchagua na kupanga ndo maana hatuendelei.

Vichocheo vya maendeleo siyo lugha ya wakoloni
Na tatizo la watanzania hupenda kung'ang'ania mambo yasiyo na tija kwetu na kuacha maslahi yetu nyuma. Kwani kiingereza, kifaransa, n.k zingekuwa lugha za kimataifa leo hii kama wao wenyewe wasingezitangaza na kuzipenda kila waendako? Ujinga kweli upo kwa mtu anayekana lugha yake na ukimwita mtumwa anakataa.
 
Back
Top Bottom