Anayelipa VAT ni end user, invoices zote zinakuwa raised na IPTL na wana raise two invoices, ya capacity charge, na ya utility. Kwa mujibu wa mkataba wa Richmond, all local taxes zitalipwa na Tanesco!. Hapa Tanesco ndie collecting agent wa TRA. Invoice ya IPTL ikienda Tanesco, inakuwa na VAT ambapo hao Tanesco, ndio wakati wa kulipa IPTL, walitakiwa kulipa ile invoice na VAT kuipeleka TRA. Sasa kama Tanesco waliremit kila kitu kwenye escrow, kosa ni la nani?!.
Siku zote ikitokea kodi stahiki hazijalipwa, huwa zinalipwa tuu wakati wowote, TRA watakuita, watakupa mpaka tarehe fulani uwe umelipa, muda huo ukifika kuna penalty fulani unalipishwa, hizi ni kesi za madai na sio jinai!.
Pasco
Kwa nini watu wanashindwa kusema kuwa VAT ilikuwa inakatwa moja kwa moja na Tanesco. Huu siyo utaratibu wa kawaida. Unataja Richmond lakini mbona Richmond ni ya juzi na IPTL ni kongwe.? Naomba tupewe uhakika kabisa kama kwenye pesa iliyokuwepo Escrow Account ndani yake mlikuwa na VAT.
Hata kama pesa zilizokuwa Escrow Account zilikuwa na VAT kulipwa IPTL sioni tatizo kabisa kwani kwa utaratibu wa kawaida kabisa IPTL ndiyo wanabidi walipe hiyo kodi baada ya kuikusanya Tanesco. VAT siyo withholding tax
Kitu kibaya kabisa katika hii report ni kuwa wachunguzi wameshindwa kuja na definite figure ya pesa inazosemekana siyo mali ya IPTL au VIP. Kwa nini.? Hata CAG ameshindwa kupambanua mahesabu ambayo ndiyo kazi yake na anaishia kuandika kisiasa.?
Ni aibu kabisa.