Hoja za Kamati ya PAC zinavyokinzana kuhusu Escrow akaunti kama ni fedha ya umma

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Kuna baadhi ya watu wanalijongea sakata ya IPTL huku wakiwa wametanguliza emotions badala ya fikra na mitazamo inayojenga hoja zenye maswali yaliyoko ndani ya hoja zilizoko mbele yetu.

Wakati akiwasilisha Taarifa ya Kamati kufuatia matokeo ya ukaguzi maalum wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania, Mhe. Zitto amenukuliwa akisema, maelezo yaliyotolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA na pia Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yalidhihirisha kuwa sehemu ya pesa au pesa zote zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa ni pesa za Serikali.

Baada ya kuyapitia Maelezo ya CAG, TAKUKURU NA TRA nimegundua hayathibitishi kinagaubaga kama pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kama sehemu ya fedha au fedha zote zilikuwa ni fedha za umma.

Viongozi wa taasisi hizi katika matamshi yao wanaonekana hawana uhakika bali wanaongozwa na dhana ya kudhani ambayo kisheria haitoa majibu ya uhakika katika uharisia wake.

Ikumbukwe kuwa, Mhe. Zitto alinukuliwa akisema,

Mheshimiwa Spika,
wakati mahojiano ya Kamati na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19 Novemba, 2014 waliithibitishia Kamati kuwa kutokana na makubaliano wa Akaunti ya Tegeta ESCROW, sehemu ya fedha au fedha yote katika Akaunti hiyo ilikuwa ni fedha ya umma.

Katika mahojiano hayo, Maafisa hao walitamka yafuatayo kuhusiana na umiliki wa fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW:

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
"… Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu. Kundi la kwanza hiyo fedha ilikuwa na kodi ndani yake kwa hiyo tungesema kulikuwemo na fedha ya Serikali kwa maana ya kodi. Kwa upande mwingine, kwa sababu mpaka ESCROW inafunguliwa kulikuwa na dispute, kulikuwa na kutokubaliana juu ya charges, kwa hiyo kuna fedha ambayo inaweza ikawa ni ya TANESCO na kuna fedha ambayo inaweza kuwa ni ya IPTL …"
Kamishna Mkuu wa TRA
"… TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye
ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT. Kwa hiyo, kulikuwa na VAT Component ambayo haikutakiwa kwenda kule …"
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
"… ninachoweza tu kusema na baada ya kusoma Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ni wazi kwamba pesa zilivyotoka TANESCO kwenda Benki Kuu bado kwa maoni yetu ni fedha za Serikali kwa sababu ni fedha ya TANESCO. Huo ndiyo mtazamo ambao tunao kiuchunguzi hadi wakati huu."
Kuna sentesi katika maelezo ya viongozi wa CAG, TRA na TAKUKURU ambazo zinaacha maswali mengi badala ya majibu.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anasema,
"… Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu..''
Hoja hapa ni neno TUNGESEMA badala ya TUNASEMA/TUMESEMA. Kwa lugha nyingine, HAWAKUSEMA.

CAG anamalizia kwa kuonyesha hana uhakika kama kuna fedha ya umma au la katika Escrow akaunti.

Hoja ya msingi, Kwa nini CAG kusema, Jibu ni kwamba, CAG hakusema kwa sababu hana uhakika.

Kamishna Mkuu wa TRA katika kunukuliwa alisema,

"… TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye
ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT..''

Hoja ya msingi hapa,

Neno ILITAKIWA KULIPWA kwa lugha nyingine HAIKULIPWA.

Swali la kujiuliza, Kwa nini TANESCO walipe pesa ya TRA kwenye Escrow akaunti badala ya kulipa TRA.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yeye anadai bado wako kwenye uchunguzi lakini uchunguzi wao umejisimika kwenye maoni ya CAG, kwa lugha nyingine, TAKUKURU haijafikia uamuzi wa mwisho katika uchunguzi wake.

Hii dhana ya PAC ya kutoa hitimisho kama Tageta Escrow akaunti ilikuwa ni fedha za umma imetoka wapi wakati hata wachunguzi hawana uhakika?

NOTA BENE:
Haya maelezo nimetoa kwenye hotuba ya Mhe. Zitto ambayo iko HAPA

Tunaomba tueleweshane na kuelimisha katika mtazamo na fikra za kujenga na siyo kashfa na matusi.
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Gw'amapalala,
Katika kujisafisha Watuhumiwa wamemwaga fedha hizo za kifisadi kwa watu wanatumia mitandao ya kijaii ili wawasafishe, magazeti, tv na njia nyingine mbambali, Tutaaminije kama wewe si mmoja wao?
Mkuu Fungwe,
Una haki ya kuendelea kuwachafua/kunichafua kihoja katika msingi wa ujenzi na siyo kubomoa.

Mwaga hoja ili na mimi nipate elimu kwa sababu elimu huwa haina mwisho.
 
Bigaraone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
723
195
Mkuu maswali yako ni ya msingi sana na nafikiri tatizo tulilokuwa nalo sisi Watanzania ni kuwa tunakuwa always obsessed na events kuliko logic na wanasiasa wanalijua hilo. Wakati wa EPA na Richmond akili yetu ilihama tukaanza kuongelea watu badala ya issues.

Kila kitu kumekuwa politicized nchi hii. Ninachelea kusema hii escorw scandal is driven by vendetta and the panacea will never be obtained
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Hivi nyinyi mnaotetea madudu ya hivi ni wazalendo kweli?mnamtumikia nani?yaani hamna kabisa uchungu na nchi hii?shame on you all
Mkuu ngonani,
Hata mawakili au mahakama huwa zinatetea wanaodaiwa kutenda maovu.

Huwezi kusema mawakili siyo wazalendo kwa vile wanatetea wanaodaiwa kutenda maovu.

Ninajenga hoja ili kuutafuta ukweli.
 
kalou

JF-Expert Member
Aug 22, 2009
4,940
2,000
mlikodisha ndege kuwahi dodoma ili kupeleka ile pingamizi yenu ripoti isisomwe mkafeli vibaya..
subiri tamko la serikali,kitendo cha Seth kufoji documents za umiliki wa hisa kinaonyesha jinsi gani kulikuwa DILI la hela za wizi.
"Kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake."
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Mkuu maswali yako ni ya msingi sana na nafikiri tatizo tulilokuwa nalo sisi Watanzania ni kuwa tunakuwa always obsessed na events kuliko logic na wanasiasa wanalijua hilo. Wakati wa EPA na Richmond akili yetu ilihama tukaanza kuongelea watu badala ya issues. Kila kitu kumekuwa politicized nchi hii. Ninachelea kusema hii escorw scandal is driven by vendetta and the panacea will never be obtained
Mkuu Bigaraone za siku nyingi?

Mambo kama haya ndiyo yanasababisha hata tusiweze kupata majibu ya msingi ambayo yatatufanya kuliondoa tatizo once and for all.

Wenzetu wa nchi za Magharibu huwa wanaangalia na kuchambua kila sentensi na maana yake katika maelezo, hotuba na sheria.

Hotuba ya Mhe, Zitto ina maswali mengi yanayoibuka katika maelezo ya wakuu wa CAG, TRA na TAKUKURU yanataka majibu mbadala.
 
Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,457
2,000
Ng'wamapalala

Hakuna shaka waliiba je sandarusi na magunia yalitumika ama la, ni nani anagawa pesa kama ni zake binafsi ha bill gATES HAFANYI HIVYOO MWEEEEE
 
Last edited by a moderator:

gollocko

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
2,950
2,000
Kuna baadhi ya watu wanalijongea sakata ya IPTL huku wakiwa wametanguliza emotions badala ya fikra na mitazamo inayojenga hoja zenye maswali yaliyoko ndani ya hoja zilizoko mbele yetu.

Wakati akiwasilisha Taarifa ya Kamati kufuatia matokeo ya ukaguzi maalum wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania, Mhe. Zitto amenukuliwa akisema, maelezo yaliyotolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA na pia Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yalidhihirisha kuwa sehemu ya pesa au pesa zote zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa ni pesa za Serikali.

Baada ya kuyapitia Maelezo ya CAG, TAKUKURU NA TRA nimegundua hayathibitishi kinagaubaga kama pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kama sehemu ya fedha au fedha zote zilikuwa ni fedha za umma.

Viongozi wa taasisi hizi katika matamshi yao wanaonekana hawana uhakika bali wanaongozwa na dhana ya kudhani ambayo kisheria haitoa majibu ya uhakika katika uharisia wake.

Ikumbukwe kuwa, Mhe. Zitto alinukuliwa akisema,

Mheshimiwa Spika,
wakati mahojiano ya Kamati na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19 Novemba, 2014 waliithibitishia Kamati kuwa kutokana na makubaliano wa Akaunti ya Tegeta ESCROW, sehemu ya fedha au fedha yote katika Akaunti hiyo ilikuwa ni fedha ya umma.

Katika mahojiano hayo, Maafisa hao walitamka yafuatayo kuhusiana na umiliki wa fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW:

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali

Kamishna Mkuu wa TRA

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Kuna sentesi katika maelezo ya viongozi wa CAG, TRA na TAKUKURU ambazo zinaacha maswali mengi badala ya majibu.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anasema,
"… Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu..''
Hoja hapa ni neno TUNGESEMA badala ya TUNASEMA/TUMESEMA. Kwa lugha nyingine, HAWAKUSEMA.

CAG anamalizia kwa kuonyesha hana uhakika kama kuna fedha ya umma au la katika Escrow akaunti.

Hoja ya msingi, Kwa nini CAG kusema, Jibu ni kwamba, CAG hakusema kwa sababu hana uhakika.

Kamishna Mkuu wa TRA katika kunukuliwa alisema,

"… TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye
ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT..''

Hoja ya msingi hapa,

Neno ILITAKIWA KULIPWA kwa lugha nyingine HAIKULIPWA.

Swali la kujiuliza, Kwa nini TANESCO walipe pesa ya TRA kwenye Escrow akaunti badala ya kulipa TRA.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yeye anadai bado wako kwenye uchunguzi lakini uchunguzi wao umejisimika kwenye maoni ya CAG, kwa lugha nyingine, TAKUKURU haijafikia uamuzi wa mwisho katika uchunguzi wake.

Hii dhana ya PAC ya kutoa hitimisho kama Tageta Escrow akaunti ilikuwa ni fedha za umma imetoka wapi wakati hata wachunguzi hawana uhakika?

NOTA BENE:
Haya maelezo nimetoa kwenye hotuba ya Mhe. Zitto ambayo iko HAPA

Tunaomba tueleweshane na kuelimisha katika mtazamo na fikra za kujenga na siyo kashfa na matusi.[/QUOTE

Nadhani wewe hujaielewa vizuri na ndio maana umekimbilia kwenye huu utetezi, ni kuwa wanaposema ni dhana kuwa hela ilikuwa ya serikali kuna baadhi ya nyaraka hasa kutoka TAKUKURU ambazo ni ushahidi unaotakiwa kupelekwa mahakamani, hivyo baadhi ya nyaraka hazikupaswa kutolewa pale bungeni! Kama unakumbuka vizuri Zitto alisema kuwa DR. Hosea wa TAKUKURU alisema bado uchunguzi unaendelea, lakini ki ukweri uchunguzi ulishakamilika na ripoti walishatoa!
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
mlikodisha ndege kuwahi dodoma ili kupeleka ile pingamizi yenu ripoti isisomwe mkafeli vibaya..
subiri tamko la serikali,kitendo cha Seth kufoji documents za umiliki wa hisa kinaonyesha jinsi gani kulikuwa DILI la hela za wizi.
"Kurukaruka kwa maharage ndio kuiva kwake."
Mkuu kalou
Mimi sijawahi hata kupanda basi achilia mbali ndege!

Niko huku kijijini Bariadi ambako usafiri wetu ni mikokoteni ya kuvutwa na ng'ombe lakini tunaishi kwa furaha kwa sababu dunia yetu inaishia hapa kijijini.

Wakati tunasubiri tamko la serikali, siyo vibaya kuendelea kujiuliza maswali ya hapa na pale.
 
Rugas

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
1,048
1,195
Mkuu ngonani,
Hata mawakili au mahakama huwa zinatetea wanaodaiwa kutenda maovu.

Huwezi kusema mawakili siyo wazalendo kwa vile wanatetea wanaodaiwa kutenda maovu.

Ninajenga hoja ili kuutafuta ukweli.
Mkuu kwa mtazamo wa kawaida! Hizi ni lugha za tafsida... kumbuka hao wote wanaichunguza serikali ambayo wao pia ni sehemu ya hiyo serikali. Wametumia lugha itakayoweza kuwaondoa katika mtego wa kuonyesha kuwa wao ndio chanzo cha kuangusha serikali nzima. Hata mwanamme akifumaniwa waswahili wanasema "amekutwa". Kwa lugha rahisi kila mmoja aliogopa kumvisha paka kengere ila ukweli wanaujua!!
 
thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,344
2,000
Ripoti ya PAC iikuwa ni vibaraka tu waliotumwa na LOWASSA na Reginald Mengi kuwashmbulia mahasimu wao ambao ni PM na Muhongo. Sikuona jipya pale.
 
thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,344
2,000
Gw'amapalala,

Katika kujisafisha Watuhumiwa wamemwaga fedha hizo za kifisadi kwa watu wanatumia mitandao ya kijaii ili wawasafishe, magazeti, tv na njia nyingine mbambali, Tutaaminije kama wewe si mmoja wao?
mimi naungana na mleta mada, ile ripoti ya ZITTO sikuona jipya lililokuwemo.
 
MFUKUZI

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
934
1,000
Msitufanye hatuna akila manina zenu!! Hao wote waliotajwa wanashtakiwa kwa kosa la utakatishaji fedha,, baada ya hapo huyo gaba chol anakesi kibao, za kughushi, kukwepa kodi na kuhujumu uchumi,, hata mzee wa mabibo bia hakwep hapo,, maafisa wa serikali watashtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi na kulisababishia hasara taifa,, hao waliopata mgao walitakiwa wa-declare kama sheria ya maadili ya utumishi wa umma inavyosema,, walipewa fedha hizo za nn,, kawaambie hao jamaa zako watz tumestuka

Nyoko we!! Watu kama nyie ndiyo mnaomba kupiga pasi kwa jiran, kwako hakuna umeme, madeni yamekujaa, huku unakesha jf kusa fisa watu kwa malipo ya buku saba!!

Ungekuwa karibu ningekutia kitu chenye ncha kali makalioni!! Shame on u!!
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Mkuu kwa mtazamo wa kawaida! Hizi ni lugha za tafsida... kumbuka hao wote wanaichunguza serikali ambayo wao pia ni sehemu ya hiyo serikali. Wametumia lugha itakayoweza kuwaondoa katika mtego wa kuonyesha kuwa wao ndio chanzo cha kuangusha serikali nzima. Hata mwanamme akifumaniwa waswahili wanasema "amekutwa". Kwa lugha rahisi kila mmoja aliogopa kumvisha paka kengere ila ukweli wanaujua!!
Mkuu Rugas
Hoja yako inatupeleka kwenye matatizo yale yale ya kulindana.

Kama tuna viongozi wakuu wa vyombo kama TAKUKURU wanaogopa kuwa chanzo cha kuiangusha serikali ambayo katika uchunguzi wao wamegundua kuna makosa ya jinai yamefanyika, basi hao viongozi hawafai hata kuwa wajumbe wa nyumba mbili.

Kumbe hata dhana nzima ya uchunguzi ni kaput.

Huu ni unafiki wa kiwango cha juu kabisa kwa wananchi.
 
lebara

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
647
1,000
Mkuu kalou
Mimi sijawahi hata kupanda basi achilia mbali ndege!

Niko huku kijijini Bariadi ambako usafiri wetu ni mikokoteni ya kuvutwa na ng'ombe lakini tunaishi kwa furaha kwa sababu dunia yetu inaishia hapa kijijini.

Wakati tunasubiri tamko la serikali, siyo vibaya kuendelea kujiuliza maswali ya hapa na pale.
Kweli fedha ya SINGASINGA ni balaa, mtu akiiba bilioni 321 anagawa kama mchele tu, heri yako kwa kulipwa na hivyo kuacha akili zako na kufurahia wizi wa SETHI
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom