Hoja ya upinzani kwa sasa ni ipi hasa?

Hoja ya upinzani kwa sasa ni ipi hasa?

Kuna chama hapa tanzania hakina hoja wala wanachama wake hawezi kufikiri kwa kina na kujenga hoja, wao kazi yao ni kusubiri wale wanaowaita nyumbu wajenge hoja, na wao wazichukue ziwe hoja zao. Sasa wanaendesha serikali kwa kutumia hoja za nyumbu. Wameona hao nyumbu sasa hawataki kujenga hoja mpya, wameanza kuwachokoza, ushauri kwa nyumbu kaeni kimya hivyo hivyo, ili muwatese. Wao wanasubiri mseme wao waanze kupiga kelele kwamba hoja ni ya kwao. KIMYA CHA ADUI KINAUMIZA KULIKO KELELE ZAKE.....
 
msijidanganye kma mapimbi hoja haziishi ktk nchi yenye wimbi la matatizo kwa hyo kwa akili zenu mnadhani raic wetu ndo atamaliza kila kitu acheni kua wajinga nyie

Hoja ya katiba mpya ni muhimu kuliko vyote, ni katiba inayotoa muongozo na kuweka misingi, inchi ili iweze kuwa na maendeleo ya kudumu unahitaji katiba bora na wala sio kiongozi bora
Kiongozi ataondoka lakini katiba itabaki.
 
Tatizo la CHADEMA ni Mbowe, the guy has no any vision at all.The sooner they accept him as a liability the better for the party.
 
Vipi kuhusu kuipongeza serikali pale inapopatia?? Inaweza ikaonesha ukomaavu wa kisiasa?

Wanaitwa wapinzani sio washangaliaji au cheerleaders, au wasifiaji au wapongezaji..., wakifanya hivyo wanakuwa hawafanyi kazi zao..., kazi za kusifia wanaachiwa viti maalumu, wabunge na makada wa Chama ila sio wapinzani...
 
Ahaa kwa hiyo unanianisha kwamba wapinzani kazi yao ni kutoa negative criticism?
Sasa what if kama serikali ikiwa inafanya vizuri, ina maana upinzani ufe kwa sababu kutakuwa hakuna vitu vya negative vya wao kutuambia?
 
Tangu kuchaguliwa kwa Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dr John Pombe Magufuli upinzania umepotea kabisa katika siasa za ujengaji wa hoja.Kwa mda mrefu sasa sijasikia siasa za hoja ambazo tulitegemea wapinzania wazijenge kwa lengo la kuipa changamoto serikali ya Rais magufuli lakini kitu kama hicho hakipo yawezekana kisitokee.

Kitu ambacho nakiona yawezekana kabisa ikawa mwisho wa upinzani uchwara ambao wamezoea kufanya siasa za kudandia na kusubiri watumishi wa serikali wafanye makosa halafu wao ndiyo wapate hoja kitu ambacho serikali ya magufuli haiwezi kuruhusu kitokee.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu sijasikia wala kuona upinzania ukifanya siasa za kujenga hoja kukemea ufisadi pamoja na mambo ya rushwa jambo ambalo Rais Magufuli analifanya yeye mwenyewe na kufanya upinzani ukose kabisa hoja.

Kama wapinzania hawatajifunza siasa za hoja za kuwasaidia watanzania badala yake wakaendelea kujikita kwenye siasa za matukio ni wazi kabisa wanakwenda kupotea kwenye siasa wakubali wakatae lakini ndiyo ukweli.

Mpinzani gani anaweza kusimama leo na kutupa mipango yake thabiti ya namna gani amepanga kuliendeleza Taifa letu kwa hoja mifano na mpango mkakati wa namna ya kutekeleza aliyopanga?

Bora hata upinzani umepotea! CCM haipo kabisa!!
 
Upinzani haupo pale kusifia ni ku-criticize ili serikali iliyopo madarakani ijirekebishe..., (power corrupts) bila upinzani waliopo madarakani wanajisahau, kwahio kama kuna mtu anayewapinga inawafanya wanakuwa alert.., na kama serikali itajirekebisha basi upinzani watabaki kuwa wapinzani mpaka pale ikitokea otherwise..., na practically sidhani kama itafika siku kutakuwa hakuna negatives, wapinzani wapo pale kama sauti ya wananchi kujua mabaya ya serikali

Ndio maana mimi sina Chama ila ni mpinzani Daima..., mpaka pale CCM / Chama Tawala kinakapo pungua nguvu zake ili iwe rahisi wakifanya makosa waweze kuondolewa kiurahisi, na wanaoingia nao wakifanya makosa waondoke after 5 years
 
Swali zuri. Kwa Mazingira ya JF upinzani ni UKAWA. ZZK, Mrema,Cheyo na Kina Mkumbo tulisha wa brand kama ni vibaraka wa CCM siku nyingi. Sitaki kurudia midahalo ya nyuma na tukajiridhisha kama upinzani wa kweli upo Ukawa.Hope umenielewa.
Tuliwabrand kama vibaraka au ni vibaraka? Kama wanaoongelewa ni UKAWA basi mie nadhani UKAWA plan Yao Ilikuwa ni kushinda Urais hivyo Mipango Yao Ilikuwa kwenye ushindi na kutekeleza Ilani Yao. kwa vile hawajashinda na kuna baadhi Ya Ahadi zao ndo Magufuli anatekeleza Nina Imani UKAWA wako wanajipanga upya. Kwa nchi kama Tanzania upinzani hawawezi kosa cha Kuongea nadhani hawataki kukurupuka.
 
Upinzani haupo pale kusifia ni ku-criticize ili serikali iliyopo madarakani ijirekebishe..., (power corrupts) bila upinzani waliopo madarakani wanajisahau, kwahio kama kuna mtu anayewapinga inawafanya wanakuwa alert.., na kama serikali itajirekebisha basi upinzani watabaki kuwa wapinzani mpaka pale ikitokea otherwise..., na practically sidhani kama itafika siku kutakuwa hakuna negatives, wapinzani wapo pale kama sauti ya wananchi kujua mabaya ya serikali

Ndio maana mimi sina Chama ila ni mpinzani Daima..., mpaka pale CCM / Chama Tawala kinakapo pungua nguvu zake ili iwe rahisi wakifanya makosa waweze kuondolewa kiurahisi, na wanaoingia nao wakifanya makosa waondoke after 5 years

Safi kabisa, umeongea vizuri.
Argument yangu tangu mwanzo wa uzii ilikuwa kwamba upinzani upo wapi siku zote hizi 26. Ina maana haya maamuzi ya kina Mafuli and co yako upande wetu raia 100 kwa 100??
Jana kuna sehemu nilienda kwenye company ya ujenzi hiyo company ni ya watu wa Kaskazini. Wakati niko ofisini kwa Director , alikuwa anaongea na Director mwenzake kuhusu Makontena yaliyopotea, wao pia walibunua vifaa kutoka kwenye kampuni tajwa, wakagusia kuhusu JPM kukazia kampuni za wahisani wa UKAWA kwenye ishu ya hizo container.
Sasa huoni kwamba ulikuwa ni wakati mzuri kwa UKAWA wawe macho na kutangaza kwenye media kuhakikisha hakuna mtu atakayeonewa na rungu limpate kila aliye husika na sio kuonea wengine na kupendelea wengine.
 
Tuliwabrand kama vibaraka au ni vibaraka? Kama wanaoongelewa ni UKAWA basi mie nadhani UKAWA plan Yao Ilikuwa ni kushinda Urais hivyo Mipango Yao Ilikuwa kwenye ushindi na kutekeleza Ilani Yao. kwa vile hawajashinda na kuna baadhi Ya Ahadi zao ndo Magufuli anatekeleza Nina Imani UKAWA wako wanajipanga upya. Kwa nchi kama Tanzania upinzani hawawezi kosa cha Kuongea nadhani hawataki kukurupuka.

Lets play wait game.
 
Tangu kuchaguliwa kwa Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dr John Pombe Magufuli upinzania umepotea kabisa katika siasa za ujengaji wa hoja.Kwa mda mrefu sasa sijasikia siasa za hoja ambazo tulitegemea wapinzania wazijenge kwa lengo la kuipa changamoto serikali ya Rais magufuli lakini kitu kama hicho hakipo yawezekana kisitokee.

Kitu ambacho nakiona yawezekana kabisa ikawa mwisho wa upinzani uchwara ambao wamezoea kufanya siasa za kudandia na kusubiri watumishi wa serikali wafanye makosa halafu wao ndiyo wapate hoja kitu ambacho serikali ya magufuli haiwezi kuruhusu kitokee.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu sijasikia wala kuona upinzania ukifanya siasa za kujenga hoja kukemea ufisadi pamoja na mambo ya rushwa jambo ambalo Rais Magufuli analifanya yeye mwenyewe na kufanya upinzani ukose kabisa hoja.

Kama wapinzania hawatajifunza siasa za hoja za kuwasaidia watanzania badala yake wakaendelea kujikita kwenye siasa za matukio ni wazi kabisa wanakwenda kupotea kwenye siasa wakubali wakatae lakini ndiyo ukweli.

Mpinzani gani anaweza kusimama leo na kutupa mipango yake thabiti ya namna gani amepanga kuliendeleza Taifa letu kwa hoja mifano na mpango mkakati wa namna ya kutekeleza aliyopanga?

On the contrary, tangu kuchaguliwa rais wa awamu ya tano anatekeleza sera za upinzani maana haya ndiyo mambo wamekuwa wakiyapigia kelele bungeni na kwenye majukwaa na kubezwa na wale walioko madarakani au chama tawala. Hivyo, Rais amegundua tunu katika yale vyama vya upinzani wamekuwa wakiyapigia kelele kwa miaka mingi. Badala ya kudhani upinzani umepotea ni kwamba upinzani umeonyesha kumbe kuna watu wanaoukubali hata kama wako chama tawala. Anza na elimu bure (hii ni sera ya chadema/Ukawa) etc.
 
Mwenzao zitto anawanyoosha polepole
Zitto huyo huyo ametoa hoja ya Aliyeshinda Zanzibar atangazwe na aapishwe ili kasi ya Magufuli iende sambamba kote kote.

Hii ni hoja muhimu sana ya wapinzani.

Link https://www.jamiiforums.com/uchaguz...-aliyeshinda-uchaguzi-zanzibar-atangazwe.html

Magufuli akizembea katika kuondoa mkwamo uliobuniwa na wabaka demokrasia , kasi yake itapunguzwa kwa kasi vile vile. Ana siku 16 ya kufanya maamuzi magumu , mimi nashauri awatose CCM- Zanzibar. Siasa za kihuni zimepitwa na wakati.

Mgogoro wa zenj
 
Bora hata upinzani umepotea! CCM haipo kabisa!!
CCM hawawezi kukufahamu kwa kauli hii lakini wenye kuijua CCM na machungu ya "maisha bora" iliyowapatia kwa miaka 40 watakuelewa.

Magufuli si amegeuka. Magufuli si CCM tena. Magufuli ni kiboko ya CCM na gambaz zote. Magufuli ameamua kujivua gamba na mpaka sasa CCM walikuwa wanaimba "mtaisoma namba" wamepata tumbo la kipindu pindu.

Dereva Magufuli kanyaga mafuta bana, tuwahi kufika maeneo yetu kufanya usafi.
 
Dah yan kwahaya aliyofanya magu bas ndo upinzan ukose hoja? ingekua hivyo dunian kusingekua na upinzan
 
Safi kabisa, umeongea vizuri.
Argument yangu tangu mwanzo wa uzii ilikuwa kwamba upinzani upo wapi siku zote hizi 26. Ina maana haya maamuzi ya kina Mafuli and co yako upande wetu raia 100 kwa 100??
Jana kuna sehemu nilienda kwenye company ya ujenzi hiyo company ni ya watu wa Kaskazini. Wakati niko ofisini kwa Director , alikuwa anaongea na Director mwenzake kuhusu Makontena yaliyopotea, wao pia walibunua vifaa kutoka kwenye kampuni tajwa, wakagusia kuhusu JPM kukazia kampuni za wahisani wa UKAWA kwenye ishu ya hizo container.
Sasa huoni kwamba ulikuwa ni wakati mzuri kwa UKAWA wawe macho na kutangaza kwenye media kuhakikisha hakuna mtu atakayeonewa na rungu limpate kila aliye husika na sio kuonea wengine na kupendelea wengine.
Weka taarifa kwa uwazi. Taja jina la hilo kampuni na wanahusika vipi na magumashi. Magufuli atajisahihisha au saidia kuipa hoja UKAWA(upinzani). Domokrasia linakuzwa kwa kupaza sauti.

JMP akijua kuwa anasemwa kuwa anapendelea na akiwa na taarifa sahihi naamini atachukua hatua. Inawezekana kabisa waliompatia taarifa za awali walitaka awashe moto kwa kampuni za wahisani wa UKAWA wakiamini Magu hatopata taarifa za magumashi za Makampuni wahisani wa CCM.

Mwaga taarifa sahihi ili zifanyiwe kazi, hapanakazi tu.

Tahadhari: Ili kumsaidia Pombe wa Magufuli atekeleze kazi na dhamana yake ni lazima apatiwe taarifa sahihi sio uzushi.
 
Upinzani sio kupinga mazuri, wala sio kazi yao kusifia mazuri..., kwahio kwenye mazuri waache mazuri yaendelee ila waibue mabovu...., mbona mabovu ni mengi tu na yamejaa, sidhani kama nchi kwa sasa inafanya kazi 100 % kwahio kama bandarini mambo yanakwenda sawa upinzani unaweza kubana kwenye taasisi kama Tanesco au kwenye Katiba ya wananchi n.k...., na kama cha kupinga hakipo bora kukaa kimya kuliko upinzani kubadilika na kuwa washangiliaji wa serikali (hapo wanakuwa hawafanyi kazi yao)
 
Weka taarifa kwa uwazi. Taja jina la hilo kampuni na wanahusika vipi na magumashi. Magufuli atajisahihisha au saidia kuipa hoja UKAWA(upinzani). Domokrasia linakuzwa kwa kupaza sauti.

JMP akijua kuwa anasemwa kuwa anapendelea na akiwa na taarifa sahihi naamini atachukua hatua. Inawezekana kabisa waliompatia taarifa za awali walitaka awashe moto kwa kampuni za wahisani wa UKAWA wakiamini Magu hatopata taarifa za magumashi za Makampuni wahisani wa CCM.

Mwaga taarifa sahihi ili zifanyiwe kazi, hapanakazi tu.

Tahadhari: Ili kumsaidia Pombe wa Magufuli atekeleze kazi na dhamana yake ni lazima apatiwe taarifa sahihi sio uzushi.

Taarifa haziwezi kuwekwa hapa. Serikali itatakiwa itengeneze hotline ya kuwa watu wawe wana ripoti.
 
Back
Top Bottom