Son Of Simon
Member
- Aug 27, 2025
- 7
- 4
Kama kweli lengo la Museveni lingekuwa mfano wa kuigwa, basi yeye mwenyewe angeonekana mnafiki, kwa sababu alimfanya mwanaye Muhoozi kuwa Mkuu wa Majeshi na wengine akawapa vyeo vikubwa serikalini. Kabla ya kumsema mwingine, Rais Museveni alipaswa kuanza kwa kutoa kibanzi kilichoko kwenye jicho lake mwenyewe.
Leo hii Polepole kila alichokuwa anakiona kibaya kwake kimekuwa keki, ili mradi tu afitishe agenda yake binafsi dhidi ya mtoto wa Rais na Dkt. Samia Suluhu. Kwa mtazamo huo, anawafanya Watanzania kuonekana kama watoto wasio na akili ya kutofautisha mambo. Hata hivyo, je, Watanzania wanapaswa kujifunza kutoka kwa Museveni? Museveni mwenyewe aanze kwanza kwa kurekebisha kwake.
Vilevile, hoja ya Polepole kudai kwamba kupostiwa picha Ikulu kulikuwa na lengo la “kufumbua macho ya Watanzania” ni hoja isiyo na msingi. Ni jambo la kawaida kabisa, duniani kote, kwamba tukialikwa Ikulu, Kitengo cha Mawasiliano kitapost picha za tukio husika kwenye kurasa rasmi. Hakuna ajabu yoyote hapo.
Kwa mantiki hiyo, Polepole anapaswa kutafuta watoto wenzake awaimbie hizo ngonjera zake, si kuwadanganya Watanzania wenye uelewa.