Hoja Saba za Zitto Zuberi Kabwe kwa yanayoendelea nchini

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,817
2,000
Kupitia ukurasa wake wa Twitter anaandika Zitto.

1.Rais na Serikali yake wanajua wazi kuwa Mbowe Si gaidi,na hilo watanzania wote wanalifahamu kuendelea kumshikilia kwa mashtaka ya kubumba kunaenda kufuta matumaini ya dunia kwa Raisi Samia kuwa Tanzania ilianza kurudi ktk misingi ya Demokrasia na Utawala wa haki"

2. "Kitendo cha Raisi Samia kurithi serikali kandamizi kutoka kwa mtangulizi wake, ni wazi tusitegemee mabadiliko yoyote chanya.Watu walewale waliosababisha maumivu makali kwa Watanzania kwa miaka sita ya hayati, bado ndio wanaokalia ofisi za umma.Inasikitisha sana"

3. "Ni jambo la kuskitsha sana pale jamii inapokubali UONEVU kuwa tabia na mtindo wa kawaida wa maisha. Tungekuwa na jamii inayojitambua, uporaji wa fedha za Wananch unaofanywa na serkal kupitia tozo za miamala usingedumu hata kwa nusu saa.Ndio maana wapigania hak weng wamekata tamaa"

4."Siasa zilizo bora ni siasa za Ushawishi(persuasive politics). Ugumu tunaoupata TZ ni namna ya kufanya siasa bila KUHASIMIANA au KUGAWA watu. CHUKI CHUKI CHUKI. Mwenye mawazo tofauti sio ADUI. Anawaza tofauti na wewe tu. HATUKUI? HATUTAFAKARI?"

5. "Ni kama Cinema ya vichekesho kwamba watu walewale waliopinga Chanjo kwa nguvu zote pamoja na uwepo wa Corona, eti miezi michache baada ya Magufuli kufariki sasa wako mstari wa mbele kuhamasisha chanjo.Kimsingi watu hawa hawana uhalali huo hata kidogo.

6. "Kama taifa lingekuwa na watu wanaojitambua, wale wote waliokuwa wanapingana na njia za kisayansi ktk kupambana na Corona walipaswa kukaa pemben(kujiuzulu)baada ya Rais Mpya kuja na mwelekeo mpya.Wananchi wana hak ya msing kuwa na mashaka juu ya chanjo kutokama na iman mliowajaza.

7.Kama taifa lingekuwa na watu wanaojitambua, wale wote waliokuwa wanapingana na njia za kisayansi ktk kupambana na Corona walipaswa kukaa
pemben(kujiuzulu)baada ya Rais Mpya kuja na mwelekeo mpya.Wananchi wana hak ya msing kuwa na mashaka juu ya chanjo kutokama na iman mliowajaza.

NB: Kuhusu ugaidi wa mbowe tuachie mahakama itende haki , kama ikibainika ni gaidi kweli basi Sheria ichukue mkondo wake.
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
11,925
2,000
Japo ameandika kwa kupooza sana.
Zityo amekosa mvuto kisiasa sana kwa tabia zake za ukinyonga
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
12,678
2,000
Zitto nae sijui unaongea nini? Huyo Rais mwenye muelekeo mpya ndio alikuwa makamu wa rais kwenye utawala wa Magufuli ambao ulikuwa unapinga chanjo na hao akina Waziri Gwajima wakiwemo pamoja nae wote walikuwa na msimamo mmoja sasa leo anaanzaje kufikiria kuwaondoa hao watu ambao alikuwa nao pamoja?
Msimamo wa Magufuli ndio ulikuwa msimamo wa serikali hivyo viongozi wote waliufuata akiwemo huyo Mama samia hivyo na huu msimamo wake Mama samia wengine wote pia huufuata maana ndio msimamo wa serikali.
 
Mbekenga

JF-Expert Member
Jun 14, 2010
1,748
2,000
Umeandika bila kuwataja majina ingawa mi nakumbuka wafuatao:

1. Jafo alikuwa mhamasishaji wa nyungu

2. Prof. Paramagamba alihamasisha Afrika tujumuishe nguvu kupata chanjo hadi akachanja ya madagasca

3.Dr.Mollel alihamasisha jeshi lijenge na kulinda taasisi ya utafiti hadi akasababisha Ndugulile atumbuliwe na yeye akapewa unaibu waziri

4. Dorothy Gwajima alitoa demo akiwa na mmewe namna ya kufanya mazoezi, kupiga nyungu na kumpakulia mme wake.

Mpaka sasa updates tunazipata kwa Gwajiboy, Polepole na msukuma.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,634
2,000
Kama kweli Zito ameandika haya, basi elimu yake haijamsaidia kitu. Raisi anawezaje kuzuia vyombo vya usalama na mahakama visifanye kazi yake!
Ni kweli, hasa ukizingatia rais ndio ameagiza hivyo vyombo vimkomoe Mbowe.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,634
2,000
Zitto nae sijui unaongea nini? Huyo Rais mwenye muelekeo mpya ndio alikuwa makamu wa rais kwenye utawala wa Magufuli ambao ulikuwa unapinga chanjo na hao akina Waziri Gwajima wakiwemo pamoja nae wote walikuwa na msimamo mmoja sasa leo anaanzaje kufikiria kuwaondoa hao watu ambao alikuwa nao pamoja?
Msimamo wa Magufuli ndio ulikuwa msimamo wa serikali hivyo viongozi wote waliufuata akiwemo huyo Mama samia hivyo na huu msimamo wake Mama samia wengine wote pia huufuata maana ndio msimamo wa serikali.

Sasa huo ni msimamo wa serikali au wa rais?
 
Autodidacts

JF-Expert Member
Jun 9, 2021
419
1,000
Kupitia ukurasa wake wa Twitter anaandika Zitto.

1.Rais na Serikali yake wanajua wazi kuwa Mbowe Si gaidi,na hilo watanzania wote wanalifahamu kuendelea kumshikilia kwa mashtaka ya kubumba kunaenda kufuta matumaini ya dunia kwa Raisi Samia kuwa Tanzania ilianza kurudi ktk misingi ya Demokrasia na Utawala wa haki"

2. "Kitendo cha Raisi Samia kurithi serikali kandamizi kutoka kwa mtangulizi wake, ni wazi tusitegemee mabadiliko yoyote chanya.Watu walewale waliosababisha maumivu makali kwa Watanzania kwa miaka sita ya hayati, bado ndio wanaokalia ofisi za umma.Inasikitisha sana"

3. "Ni jambo la kuskitsha sana pale jamii inapokubali UONEVU kuwa tabia na mtindo wa kawaida wa maisha. Tungekuwa na jamii inayojitambua, uporaji wa fedha za Wananch unaofanywa na serkal kupitia tozo za miamala usingedumu hata kwa nusu saa.Ndio maana wapigania hak weng wamekata tamaa"

4."Siasa zilizo bora ni siasa za Ushawishi(persuasive politics). Ugumu tunaoupata TZ ni namna ya kufanya siasa bila KUHASIMIANA au KUGAWA watu. CHUKI CHUKI CHUKI. Mwenye mawazo tofauti sio ADUI. Anawaza tofauti na wewe tu. HATUKUI? HATUTAFAKARI?"

5. "Ni kama Cinema ya vichekesho kwamba watu walewale waliopinga Chanjo kwa nguvu zote pamoja na uwepo wa Corona, eti miezi michache baada ya Magufuli kufariki sasa wako mstari wa mbele kuhamasisha chanjo.Kimsingi watu hawa hawana uhalali huo hata kidogo.

6. "Kama taifa lingekuwa na watu wanaojitambua, wale wote waliokuwa wanapingana na njia za kisayansi ktk kupambana na Corona walipaswa kukaa pemben(kujiuzulu)baada ya Rais Mpya kuja na mwelekeo mpya.Wananchi wana hak ya msing kuwa na mashaka juu ya chanjo kutokama na iman mliowajaza.

7.Kama taifa lingekuwa na watu wanaojitambua, wale wote waliokuwa wanapingana na njia za kisayansi ktk kupambana na Corona walipaswa kukaa
pemben(kujiuzulu)baada ya Rais Mpya kuja na mwelekeo mpya.Wananchi wana hak ya msing kuwa na mashaka juu ya chanjo kutokama na iman mliowajaza.

NB: Kuhusu ugaidi wa mbowe tuachie mahakama itende haki , kama ikibainika ni gaidi kweli basi Sheria ichukue mkondo wake.
Huyo sio Zitto,hio ni parod ya mtu anaetafuta followers uko tweeter,sio acc ya Zitto mleta uzi punguza ujinga. Acc. ya ZZK ina followers 1.3 sio 6k
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,277
2,000
Mama SSH, Rais wa JMT inampasa kwa haraka sana afanye mabadiliko katika baraza lake la mawaziri. Wizara ambazo anazopaswa kuzifanyia mabadiliko ni pamoja na zile zenye dhamana ya fedha na uchumi, mawasiliano, mambo ya ndani pamoja na ile ya sheria na katiba.

Hizi wizara zinaonekana zimeshindwa kumpa ushauri mzuri bali kumfitinisha na wananchi. Ukiziangalia wizara hizi kwa jicho la tatu, pengine zina "subtle intention" ya matamanio ya urais kwa mwaka 2025.
 
Rhz4567

JF-Expert Member
Mar 16, 2018
3,136
2,000
Zitto kaandika point sana tatizo.lipo kwa watz wenyewe

wacha wapambane na hali zao

I'm out out
 
chase amante

JF-Expert Member
Feb 24, 2018
4,901
2,000
Zitto aache unafiki. yeye ndiye aliyezipigia chapuo hizo tozo kipindi cha magufuli, saivi anazikataa tena
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,138
2,000
Walau amesema neno juu kadhia Mbowe.Japo too low ni Kama mwandishi kamnukuu kwa ufupisho usio makini.
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,002
2,000
Kama kweli Zito ameandika haya, basi elimu yake haijamsaidia kitu. Raisi anawezaje kuzuia vyombo vya usalama na mahakama visifanye kazi yake!
Wewe unaongea kitoto sana au unaongea kama vile huishi Tanzania hii. Wewe unaamini kweli kuna mahakama ktk nchi hii.

Rais ndiye kila kitu, ndiye jaji ndiye hakimu ndiye mwendesha mashitaka na tena ndiye polisi sasa wewe unategemea nini hapo.

Lema alikaa mahabusu miezi minne bila sababu na kwa uonevu tu kisa rais ameagiza iwe hivyo. Sugu ilifungwa jela kwa uonevu kabisa kisa imempendezea rais. Magufuli hata kama amekufa yaani ngoja afe kabisa kwani alikuwa ni mnyama.

Kuna mahakimu pale Kisutu wanaulilia sana ujaji na njia ya mkato ya kutimiza ndoto yao wanajua sio weledi katika kazi bali ni kuwakomoa akina Mbowe kwa kuwafunga jela kesho unaukwaa ujaji kama fadhila. Tuko kwenye utawala wa hovyo ni hakuna mfano.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom