Hoja Maridadi: Udhaifu wa Bunge Ulishadhihirika - Nyuma ya Assad Tuko Wengi

Naona mihogo imeisha mmeanza kuibuka tena.
Hivi huko Sweden mihogo inapatikana kweli.?
Na. M. M. Mwanakijiji
Kwamba Bunge letu ni dhaifu ni mjadala wa miaka kumi na tano iliyopita. Mjadala ambao hatuwezi kuurudia sana ni kusema kuwa “Rais ni dhaifu” au “Serikali ni dhaifu”. Hatuna Rais dhaifu, au mwoga au anayejitahidi kuridhisha kila anayemkosoa. Kuhusu Rais bado mengi ya kutamani – kwamba ukali wake na usimamizi wake bado haujafikia kiwango cha kuinyosha nchi na kumweka kila mtu katika mstari wa sheria na Katiba. Lakini kwa kiasi chake ni kuwa leo si jana.
Kauli ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu (CAG) Prof. Assad akinyoshea Bunge kidole kuwa licha ya kazi kubwa inayofanya taasisi yake bado Bunge halijaweza kuisimamia serikali ipasavyo na hivyo kutoa mwanya wa mwendelezo wa madudu ambayo yalianza kuibuliwa tangu 2005. Kwamba, tangu 2005 hadi leo hii tulitarajia kuona kuwa mambo kadhaa yamefanyika kuimarisha udhibiti na usimamizi wa mali za umma pamoja na kuimarisha mfumo wa kuwajibishana. Alichosema au kudai Assad ni kuwa bado mengi yanatakiwa kufanyika kuweza kujenga mfumo sahihi wa kiutendaji wenye msingi wa uwazi, haki, wajibu na kusimamiana. Kukosena kwa hili ndio udhaifu wenyewe.

Kudhihirika kwa Udhaifu wa Bunge
Inawezekana wengi wameshasahau kuwa huko tulikotoka tumetoka kwenye utawala wenye kashfa zilizojaa hadi shingoni. Kuanzia kuibuliwa kwa kashfa kubwa ya Loliondo – labda kashfa kubwa iliyohusisha hadi Ikulu hadi kufikia kashfa za Dowans na Richmond – tumepitia kashfa za Meremeta na watoto wake Deep Green na Tangold hadi hivi sasa. Kuanzia kashfa za sukari za wakati wa kina Kiula hadi hii zile za Commodity Import Support na wenzie kama EPA n.k Tanzania ilikuwa ni zaidi ya shamba la bibi; Tanzania ilikuwa ni shamba la kijiji cha Mtakula. Kila aliyetaka kula alikula na walikula bila hata kubariki au kusema Bismillah! Walikula wao, watoto wao, na wapenzi wa watoto wao!
Kashfa zote hizi zilitokea kwa sababu chombo pekee kilichoundwa kikatiba kusimamia na kuiwabisha serikali kilikuwa dhaifu.

Si udhaifu wa Kuzungumza na Kujadili Bungeni kwa Hamasa
Ni makosa makubwa kudhania kuwa Assad na sisi wengine tunapozungumzia udhaifu wa Bunge tunazungumzia udhaifu wa watu kuzungumza Bungeni. Hatuzungumzii hata kidogo udhaifu wa kukosekana mijadala motomoto au watu kuzungumza kwa ukali Bungeni. Katika hili Bunge la Tanzania linawezekana kuwa ni bunge lenye mijadala motomoto sana. Hakuna udhaifu wa kupiga kelele “mheshimiwa Spika!” Na kwa hakika hakuna udhaifu hata wa kunyosheana vidole hadi watu wapoteze kazi. Hili ni mojawapo ya mambo rahisi sana ambayo yanafanywa na Bunge letu; kwamba, wakimnyoshea sana kidole waziri au mtendaji Fulani na yule mtendaji akaondolewa basi wao wanaamini wamefanya kazi yao sawasawa; hapa ndipo penye tatizo.
Kama kipimo cha uthabiti ni watu kujiuzulu au mawaziri kuondolewa kwenye wizara zao ni rahisi kusema kuwa “bunge linafanya kazi yake”. Hata hivyo ndugu zangu sote tunajua Bunge kazi yake kubwa na ya kwanza ni kutunga sheria. Sheria zilizotoea na zinazoendelea kutoa mianya mbalimbali ya watu kutumia madaraka yao vibaya na kutapanya mali za umma zimetungwa na Bunge.
Udhaifu uliopo kwenye serikali na utendaji wake unatokana na udhaifu uliopo kwenye Bunge na utungaji wake wa sheria. Sheria zetu nyingi zimetoa mianya mingi kiasi kwamba ni rahisi zaidi kufisadi nchi ndani ya sheria hizo hizo.

Udhaifu wa Bunge Unaakisi kwenye Sheria ya CAG
Tangu ripoti za CAG zianze kuwekwa hadharani na kujadiliwa kwa uhuru sana kuanzia 2005/2006 Watanzania wamepata nafasi ya kuona yanayofanyika ndani ya taasisi mbalimbali za umma. Madirisha yaliyokuwa yamefungwa kuchungulia wizara, idara na taasisi mbalimbali za umma yalifunuliwa na watu wameweza kuchungulia kilichomo ndani; na hawakukipenda. Katika ripoti hizi tumeona jinsi gani taratibu za matumizi ya umma hazifuatwi, tumeona jinsi gani fedha za umma zinatumiwa bila kujali (with impunity) na tumeona jinsi gani licha ya uchafu kuonekana watu wale wale wameendelea kuachwa wakifanya kazi.
Hata leo hii, CAG anaweza akaenda mahali akakagua na kukuta madudu lakini hana la kufanya isipokuwa kutuandikia kwa kina kuwa mahali Fulani kuna madudu. Huu ni udhaifu wa kisheria. CAG amekuwa ni mtu wa kunyoshea kidole tu lakini hana uwezo wa kuinua hata unyoya kushughulikia tatizo. Matokeo yake, CAG amekuwa kama yule mzee wa mikasi; kazi yake ni kutuonesha madudu tu akisubiri wengine washughulikie matatizo. Huu ni udhaifu wa kisheria.

Udhaifu wa Bunge Unaakisi kwenye Sheria ya TAKUKURU
Udhaifu huu wa kisheria unaonekana pia katika mfumo wa utendaji wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU). Siyo kusudio langu kuangalia kipengele kwa kipengele lakini ni rahisi kuona jinsi gani kupambana na rushwa Tanzania japo kunajaribiwa sana bado mfumo wa kisheria haujatengenezwa kiasi cha kuhakikisha kuwa taasisi hii ni huru zaidi, na inawajibika kwa wapiga kura zaidi. Kwamba, taasisi hii ni rahisi kuingiliwa na watendaji wa serikali (mifano ipo) kunaifanya taasisi hii kutegemea zaidi uzuri wa aliyeko Magogoni.

Bunge Lenyewe ni Mfano wa Vyombo Visivyozingatia Sheria na Taratibu
Mojawapo ya mambo yanayoonesha udhaifu mkubwa ni kuangalia ripoti za CAG na kukuta kuwa Bunge lenyewe halifuati sheria inazotunga lenyewe. Ripoti mbalimbali za CAG zimekuwa zikionesha kuwa utendaji wa Bunge si mfano wa kuigwa linapokuja suala la kusimamia mali na fedha za umma. Nitatoa mifano kadhaa.
Taarifa ya CAG ya 2010/2011 inataja mapungufu kadhaa katika ofisi ya Bunge linapokuja suala la matumizi na usimamizi wa fedha za umma:
Malipo ya Sh 94,000,000 yalilipwa kwa watumishi mbalimbali wa ofisi ya Bunge kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni 2011 kwa ajili ya kazi za ziada na poSho nyingine. Hata hivyo kiasi hiki kilionyeshwa kwenye hesabu za Bunge kama mali zisizogusika. Uainishaji huu sio sahihi na unaweza kupotosha watumiaji wa hesabu za Bunge. (Uk. 84).
Menejimenti ilinunua mashine ya uchapiShaji kwa gharama ya Sh.370, 019,894 ambayo haifanyi kazi, na matokeo yake ofisi iliamua kukodi maShine nyingine kwa gharama ya Sh.190,480,496 kwa mwaka. (Uk. 84).

Kama haya yanatokea Bungeni itakuwaje kwenye taasisi nyingine? Hata ripoti za karibuni licha ya kuwepo maboresho mbalimbali bado kuna changamoto na matatizo makubwa linapokuja suala la usimamizi wa fedha za umma kuanzia Bungeni hadi kwenye taasisi nyingine.
Tatizo hili linatokana na Bunge lenyewe na sheria yake.

Chanzo cha Udhaifu
Bunge Linaposubiri Miswada Toka Serikalini

Nimetoa mifano ya sheria za taasisi hizi mbili kwa makusudi tu. Miswada ya sheria hizi ilitoka (originated) kutoka Serikalini. Kwamba, serikali inaleta miswada ya kushughulikia matatizo yaliyoko serikalini na wabunge wanajadiliana na mwisho wanapitisha kwa kiasi kikubwa yale yaliyopendekezwa na serikali. Kwamba Bunge linasubiri miswada toka serikalini ni tatizo kubwa sana kwani mawazo na maoni yanayotolewa yanatokana na maono na mtazamo wa wale walioko serikalini. Bunge ndio hapa linapogeuzwa kuwa mhuri (rubber stamp). Watajadili mwisho wa siku watapitisha. Halafu baadaye wanagundua walichopitisha ni madudu wataitaka “serikali ilete mswada mwingine”!

Sheria zinapokosa Vifyatushi vya Uwajibikaji
Sheria nyingi zinaandikwa ni nzuri sana lakini ndani yake utaona zinakosekana vifyatushi (triggers) ambavyo vitasababisha hatua mbalimbali kuchukuliwa endapo mambo Fulani yatatimia. Kwa mfano CAG anapoenda kufanya ukaguzi (uwe wa kawaida au usio wa kawaida) anaweza kukuta mambo fulani Fulani ambayo ni mapungufu makubwa yenye kutishia mali za umma. Sheria haijaweka triggers zinazoweza kumsababisha CAG kwa mfano mara moja kumsimamisha mtu kazi au kuweka msimamizi wa dharura (emergency manager). Kutokana na upungufu huu CAG anakuwa ni kama mtu wa nje ambayo anaweza kuona mtu anachoma nyumba lakini hana uwezo wa kumzuia zaidi ya kuandika ripoti jinsi nyumba inachomwa! Huu siyo udhaifu wa CAG ni udhaifu wa kisheria! Unaotokana na Udhaifu wa Bunge!

Wingi wa Wabunge wa Chama Kimoja
Tatizo jingine ni kuwa kuwa na wingi wa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge wa chama kimoja kinachotawala ni tatizo jingine la udhaifu wa Bunge. Wabunge badala ya kuwa watumishi na wawakilishi wa majimbo yao wanakuwa ni makada wa chama tawala. Japo katika mfumo wetu wa serikali Chama tawala na serikali yake vinatakiwa kuakisiana kwa nchi yetu huku kuakisi kumekuwa ni kuwa pacha. Wabunge wa CCM kwa mfano, hata kama hawapendi sheria Fulani na wanaweza kuona matatizo yake hawatokuwa tayari kupiga kura ya hapana kwa sababu kwa kufanya hivyo wataonekana wanapingana na serikali yao. Matokeo yake, wabunge wanaweza kujikuta kwa ajili ya kuonesha kusimama pamoja na serikali yao wanaweza kupitisha sheria mbovu na dhaifu ilimradi wasije kuonekana wanapingana ama na Rais au na chama chao. Huu ni udhaifu mkubwa.
Wingi huu unaondoa ulazima wa chama tawala kuzungumza na kujadiliana na upinzani Bungeni. Hawahitaji hata kura moja ya Mbunge wa upinzani na matokeo yake wanaweza kuwaburuza wanavyotaka bila kuathiri upitishaji wa mswada au azimio lolote la Bunge. Kitu pekee ambacho wabunge wa upinzani wanaweza kukifanya ni kuzungumza kwa ukali, kwa kejeli na hata kufanya vituko ilimradi wasikike hata kama hawatasikilizwa!
Tatizo hili bila ya shaka linaweza kuondolewa na wapiga kura tu; haliwezi kuondolewa na CCM au na Rais. Wapiga kura kama wanaona wanataka kuwa na Bunge linalowajibisha serikali kweli kweli ni wao ndio wanaulazima na wajibu wa kupunguza wabunge wa CCM bungeni. Hata hivyo, hili litategemea kwa kiasi kikubwa ni wagombea gani wazuri wanaoweza kusimamishwa na upinzani kulinganisha na wale wa CCM. Kwamba, watu wampigie kura mgombea wa upinzani tu ilimradi wa CCM atakaliwe haiwezi kuwa sababu ya kutosha. Hili limejaribiwa na limeshashindikana.

Bunge Laweza Kuimarika na Kuondoa Udhaifu Wake
Bunge linaweza kuondoa udhaifu wake na kuonekana kuwa ni mhimili sawa (equal branch) wa serikali na ule wa Mahakama na Urais. Bunge likijiona chini ya Urais au Mahakama litakubali kutendewa hivyo na litajitendea hivyo na matokeo yake ni kututumia misuli kama lilivyofanya kwa Paschal Mayalla na sasa hivi kwa Prof. Assad. Bunge lisitumie uwezo wake na madaraka yake kunyanyasa watu badala yake lijiangalie lenyewe kama madai yanayotolewa dhidi yake yanasimama. Na Lisiogope kunyoshewa kidole kwani katika demokrasia ni kunyosheana vidole kunakofanya watu wajadiliana na kutafuta muafaka wa mambo mbalimbali. Kubishana bila kutishana na kupingana bila kupigana ndio msingi wa uhuru wa kidemokrasia.
Bunge linaweza kuwa imara; kwanza kabisa kwa kuimarisha sheria mbalimbali ili kuondoa mianya ambayo imekuwepo. Kwa mfano, kwanini CAG afike kwenye ofisi akute mali za milioni 50 hazipo, hakuna maelezo na vitabu vya mahesabu havipo na watu bado wanaendelea kuvaa suti ofisini. Kwanini Sheria isitake kuwa CAG akiona upungufu wa kiasi Fulani anatakiwa achukue hatua Fulani ikiwezekana hata kuwa na waendesha mashtaka wa ofisi yake (kama walivyo wale wa TAKUKURU)? Yaani, CAG agundue wizi halafu aandike ripoti ya wizi akisubiri mtu mwingine aje kumkamata? Hata kama hatutaki CAG mwenyewe akamate wabadhirifu basi tumpe nguvu ya kutoa oda au amri ya nani akamatwe kwani ushahidi atakuwa anao yeye CAG! Wengine tumechoka kusoma ripoti za ukaguzi kama riwaya za Joram Kiango na Ray Shaba!
Wananchi wenyewe wanaweza pia kusaidia kuliimarisha Bunge. Hili linaweza kufanyika kwa kuhakikisha kuwa Bunge linakuwa na wabunge wa kutosha wa upinzani ambao watasaidia kuwajibisha na kulazimisha mazungumzo na chama tawala. Lakini wananchi hawatafanya uamuzi huo kama upinzani wenyewe hautawala sababu ya kufanya hivyo.
Mwisho wa yote, Bunge la Tanzania linaweza mambo mengi na linaweza kusifiwa kwa mengi tu; lakini kwamba ni Bunge linaloisimamia serikali na taasisi yake vizuri si mojawapo. Ni bunge dhaifu na udhaifu wake ulishathibitika na unaendelea kuwepo. Si udhaifu wa kuiharibu sifa yake au kuifanya iwe duni; ni udhaifu wa kusema kuwa kuna mahali kuna tatizo na linahitaji kutatuliwa. Bunge ni chombo chetu sisi Watanzania na tunayo haki ya kusema kama hakiendi sawa au hakifanyi kinavyotakiwa. Hili ni kweli si kwa Bunge tu bali hata kwa Mahakama na kwa Urais. Hivi vyote ni vyombo vya Watanzania na Watanzania mmoja mmoja au kwa umoja wao wana haki ya kuvitolea maoni – mazuri au mabaya. Ni jukumu la vyombo hivyo kuonesha kuwa vinajali na viko tayari kukosolewa badala ya kuhamaki kwanini vinanyoshewa kidole.
Alichosema Prof. Assad kina ukweli, na siyo peke yake anayesema na nyuma yake tupo wengi ambao tunaona udhaifu huo huo.
Ni wakati wa Bunge kujichunguza na kujisahihisha.
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hoja umeeleza vizuri lakini kumbuka tanzania sio marekani au uingereza ni nchi inayoanza kujijengea misingi thabiti ya maendeleo tatizo ni hawa wasomi wetu kujaribu kufikiria kama wako kwenye nchi hizo kumbe tuko dunia ya tatu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom