Wakuu zangu leo mimi nataka kuelewa kuhusu haya maridhiano ya Kitaifa yanayozungumzwa ili kuliponya Taifa letu.
Hivi maaridhiano haya ni baina ya nani na nani? Kama ni ya Kitaifa swali langu "Kwani kuna mgogoro au kutoelewana kupi na baina ya nani na nani?"
Je, Serikali haielewani na Wananchi?,
Je, ni baina ya Dola na Wananchi?
Je, ni Vyama vya siasa?
Je, ni baina ya Viongozi wa nchi na kina nani?
Mpaka leo hii mimi sielewi tunataka kuridhiana juu ya kitu gani na kwa nini? Na Maridhiano hayo yanatokana na tatizo gani linalolianhaniza Taifa? Kipi kimeajiri Maridhiano haya yanayodaiwa?
Tumewahi kuona maridhiano baina ya CCM na Chadema, na wakawekeana masharti. Yalofuata tulisikia kuna Wasaliti wamelamba Asali? Je, safari hii kuna tofauti gani na ile ya mwanzo?
Pia tumeshuhudia maridhiano ya ACT na Serikali ya Zanzibar wanajua wao hoja na madai yalokuwepo. Na pengine huo ndionulikuwa msungi wa maridhiano, wamefikia muafaka baada ya kugawana madaraka.
Huko nje tumeona maridhiano baina ya Marekani na Iran kwa sababu kuna vita baina yao, wakitafita suluhu Vita isimame na wanawekeana masharti. Huu ndio msingi wa Maridhiano yao
Sisi Tanzania tunataka maridhiano ya Kitaifa kufuatia nini na kwa matumaini gani? Kuna jambo au mgogoro gani unaohitaji maridhiano baina ya wahusika?
Je, hoja kuu ni kupata Katiba Mpya? yahusu kamata kamata na Utekaji?
Ni kutokutambua matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2025?
Ni Uchochezi wa Kisiasa unaotutenganisha?
Ni Mauaji ya October 29? Ni wapi na kitu gani haswa tunapokosana?
Au ni yote kwa Ujumla wake! Na katika yote haya nani mkosa ambae yuko tayari kukiri kufanya makosa hayo anataka kuyamaliza kiistarabu!.
Mimi sielewi naomba kuelimishwa.
Maasalaam