MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,482
- 20,428
Katika hali ya kustaajabisha siku ya leo jumamosi, jiji la Mwanza hasa maeneo ya Buzuruga, Nyasaka, Mahina, Mhandu, Gedeli na maeneo mengine ya jirani hali imekuwa tofauti na ilivyozeleka.
Katika maeneo tajwa katika siku nzima ya leo anga limekuwa kama lina vumbi au ukungu au vyote kwa pamoja na hivyo kuzua sintofahamu.
Kwa kawaida huwa hakuna ukungu na jua likawepo kwa wakati mmoja. Baadhi ya watu nilioongea nao wamezitaka mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo na wengine wakidai labda ni wananchi wanapiga nyungu kwa ujumla siku ya leo.
Picha na maoni zaidi ya wakazi yanakuja kadri nitakavyoyapokea.